The less you know, the happier you are!

Khaa!! Bana kwahiyo huyo Dr alifanya haya ili alipwe kwa kupewa ubunge?
 
Usipoteze muda kuhuzunika. Hakuna kisicho na gharama duniani. Ni juu yako kujipima kuhusu gharama ipi uko tayari (unaweza) kuimudu - kati ya ujinga na maarifa. Ukitaka kuzama zaidi kwenye falsafa hiyo hapo ndipo utakapogundua nguvu rasmi ya Mwenyenzi Mungu ilipo na kwa nini inabidi uitafute na kuitumaini zaidi ya vyote.
 
Ni kweli mkuu ni bora usijue kwamba tume ya taifa ya uchaguzi si huru, bora usijue kwamba katiba ya Tanzania imekaa kidikteta, ni bora usijue kwamba kinachofanya tanzania isiendelee ni mfumo mbovu wa kuanzia chini....utaishi vizuri na utashabikia vitu hivyo hivyo na maisha yatakua vizuri ila ukijua tu....inakua shida
 
Nafikiri ni uamuzi mzuri wa kuacha kusaidia watu ambao wamepewa nafasi ya kujikomboa wakaiacha, halafu mwakani wakidaiwa ada za shule wanaazna kuomba misaada...tuwachinjie baharini.
 
Tru that....ndio maana wehu na machizi wanaishi kwa raha sana....
 
Hakuna haja ya kutaka kuwa mjinga na mpumbavu.

Tatizo watanzania tunaishi kijamaa sana, hata kiongozi tunamuona kama ndugu yetu.

Ndio maana tunampa kura kwasababu ametupa kanga na kofia.

Watanzania tunakosa 'exposure'. Hatuna ile hamu ya mabadiliko.
Hatuna wivu wa kimaendeleo.

Tumeridhika na ujinga na umasikini wetu.

Kwasasa sishangai kwanini kuna watu ulaya wanalala nje na wengine wanalala angani kwenye jets zao.
 
Aisee mtoa mada umenigusa mana hata mimi nna huzuni sana yani watu wote wenye shida zilizopitiliza ndo wanachagua wale ambao hawatawakomboa kutoka walipo na mimi nimedhamiria sana kuwa nikimsikia mtu analalamika kuhusu mfumo mbovu afu analia shida sitamsaidia kabisa afu bora tuzidi kupata shida ili tukumbuke makosa yetu aiseee hadi najionea huruma
 
umenena,me nahic kupasuka kabisaaaaa naomba tu kila kitu kiishs amani irudi.Sina raha kbsa!
 
Khaa!! Bana kwahiyo huyo Dr alifanya haya ili alipwe kwa kupewa ubunge?
Lengo la kuwasaidia siyo kupata Ubunge bali Yeye aligombea Ubunge ili aweze kuwasaidia vizuri zaidi Wananchi kwa kuwasemea huko kwenye vyombo vya maamuzi m.y.ni kwamba kuwasaidia kwa kuwapa misaada ya kijamii peke yake haitoshi km hujawasemea huko mjengoni.
 

tunapoitwa wanywa vloba sio tunapenda kwa upande wangu sioni kabisa cha kupunguza strees!! nilie nae ndio kabisa anazidi pasuwa kichwa naona kabisa upendo ushapunguwa na sina cha kumlaumu uvumilivu umemchosha kila cku labda keshe!!angalau jamii forum huwa inanifarijisha kimtindo japo kuna manyumbu huwa yanazinguwa.mziki haupenyi tena masikioni maana ukifungulia tu mwenyenyumba kafika anadaichake ni bola uludi magetoni kimya kimya uondoke kimyakimya du!!
 

Serikali za kidemokrasia ndizo hazina habari na mwananchi mmojammoja,

Leo VOA nimesikia wakenya wanalalamikia serikali yao kuwa ufisadi umezidi kipimo, Nigeria napo kesi ni ileile. Kwa kagame hatusikii kelele za kifisadi, serikali ya Gadafi ililea watu wake kama familia moja.
Tatizo si mfumo tatizo ni mtu anayesimamia mfumo.
 
Nakumbuka kabla ya uchaguzi wa 2010 nikawa namshawishi dada angu amchague Chadema.alinijibu 2005 alienda Mbowe kijijini kwao Singida akawaahidi maji,sista alimpa kura Mbowe awe rais lakini mpaka 2010 Mbowe hakuleta maji licha ya yeye kumpa kura,kwa hiyo hawezi kuipa chadema
 
Mi nashangaa sana watu hisia zao kuita ndio elimu,yani mtu kufuata hisia zake ndiyo anajiona ameelimika. Hivi ni kuelimika gani huko ambako kunamfanya mtu aseme bora hata jiwe awe muongozaji wake kama sio hisia? Yani kama wale wengine hutumia ujinga wa watu kama isemavyo basi hawa wengine hutumia hisia za watu,hakuna tofauti hapo.
 
Nimeumia sana, mm nahisi kuna baadhi ya watu wanashindwa kuhusianisha siasa na maisha.
 

Usipende kujishughulisha na mambo ambayo unadhani ukiyajua kwa undani na ukweli yatakutesa!mfano,wewe unajua kabisa ukijua mpz wako anachepuka utaumia sana pengine kufa kwa presha,ya nini umchunguze?!Ukitaka kuijua hasara ya kutokuwa na maarifa endelea na ujinga wako yani utakuwa lofa milele!Pia ili uwe na furaha ni lzm ujue unataka nn,vinginevyo utahuzunika kwa kila jambo!Ukiona siasa zinakuvuruga achana nazo sio lzm ufuatilie siasa km zinakuvuruga na ww hutaki kuvurugikiwa!
 
Ni kweli mkuu. Kadri unavyojua ndo unavyojilimbikizia huzuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…