masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,828
- 14,981
- Thread starter
-
- #21
Hili tatizo la Panya Road liko juu ya uwezo wa Polisi peke yao kulitatua.Hata hapa kwangu napoishi, muda mfupi uliopita tulikuwa tunazungumzia swala hili na mwanamama mmoja na nikamueleza chanzo kimojawapo cha matukio kama haya ni watu kukosa ajira na kukata tama.
Bahati mbaya sana,kama ilivyo kwa wana-CCM wengi,mama huyu alipinga hoja yangu na kutoa sababu zake kama vijana kuvuta bangi n.k.
Huyu mama angekuwa na akili angejiuiliza kwanza ni kwanini vijana hawa wavute bangi n.k.
Najua kuna wengine hata akiwa na maisha mazuri kuvuta bangi na mambo ya aina hiyo ndio hulka yake.Lakini je,wote hawa kwa makumi au mamia wanafanya vitendo kama hivi kutokana na hulka zao tu?
Polisi kama wana akili,vijana waliowakamata wawahoji kistaarabu ili wawape sababu za wao kufanya walioyafanya na taarifa wazipeleke serikalini kwa utatuzi kama tunataka haya yasijirudie tena.Tofauti na hapo ni kujidanganya tu.
In short,civil disobedience in our country is around the corner.
Very good...umeandika maneno mazito sana mkuu....inaonyesha jinsi gani ulivyojawa na shauku ya kuiona TANZANIA MPYA........tutafika tu hata kwa mwendo wa konokono ili tu tunasonga mbele na sio nyuma na mapambano yanaendelea.....ALUTA CONTINUA...........Very true mkuu!!
Inasikitisha kuwa watu hawaendani na utatuzi wa yanayotukabili kitaalam
In actual fact we are sowing the seeds of our own social disharmony.
Mipango yetu haiwafikirii wanyonge the we expect the best!!!!
mipango yetu ya kisiasa na kiuchumi ina matatizo ambayo sasa ni kama ina fuel social conflicts.
Huu uzi ungetakiwa uwe na page zaidi ya arobaini....kutokana na hali halisi ya hapa nchini mwetu...Watanzania ni kama tuna mitindio wa ubongo.....bado watu wanajionea sawa tu kwa namna mambo yanavyoendeshwa nchini...wanajionea kuwa umaskini na dhiki zinazotukabili ni mipango ya Mungu..na wameamua kumuachia mungu....wakati Mungu kawapa ufahamu wa kuyatafakali mambo kwa kina.....
Watanzania wengi vichwa vyetu tumevielekeza kwenye mahaba na umbea pekee....huu uzi kama ungekuwa wa mapenzi au unamzungumzia mtu flani sasa hivi ungekuwa kwenye page ya mia na......
Bado tuna safari ndefu sana kuelekea ukombozi wa mtanzania...kibaya zaidi hata mfumo mzima wa elimu yetu inatufanya tuzidi kuwa kama mazezeta kwa kuwa hautupi tafakuli na maarifa ya kujiuliza maswali ya msingi yanayotugusa...zaidi kukariri vya kujibia mtihani na kukabidhiwa vyeti vizuri huku kichwani kukiwa hakuna maarifa.....
MABADILIKO YA NCHI YETU YANAANZA NA MIMI NA WEWE.....
Ni kweli hili jambo la Panya Rd lazima litazamwe kwa nia ya kutatua matatizo yanayojitokeza katika jamii.Wenye nacho watakwambia Panya Roads ni Wahuni tu,Wazembe wa kutopenda kufanya kazi ila kupora Mali.Hawalioni Tatizo la ajira wao kila kitu ni ktk Mtizamo wa Kisiasa tu.
Wasio nacho kwa upande wa pili wanaliona tatizo la Panya Roads kama kushindwa kwa serikali kuweka mikakati ya kuwawezesha vijana.
Wanaina serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Imewatelekeza vijana na watanzania kwa ujumla, Maisha bora kwa kila Mtanzania waliyoahidiwa yameyeyuka ka barafu na Kuacha simanzi ya Sintofahamu kwa Vijana.
Vijana wanasema Serikali ya CCM imewatapeli na Kilichobaki kwa sasa ni Hasira zao kwa CCM 2015, watakapokuwa wakifanya maamuzi yenye busara,kwa Kuzijaribu sera za UKAWA zenye kulejesha matumaini ya kushiriki kufaidi Keki ya Taifa, ambayo kwa sasa ni Kwa matajiri na Wanasisa Uchwara ( wapiga dili).
Mkuu kwa kweli lazima tuione Tanzania YOTE kama watanzania.Very good...umeandika maneno mazito sana mkuu....inaonyesha jinsi gani ulivyojawa na shauku ya kuiona TANZANIA MPYA........tutafika tu hata kwa mwendo wa konokono ili tu tunasonga mbele na sio nyuma na mapambano yanaendelea.....ALUTA CONTINUA...........
Asante kwa kuchangia mada hii na kuitazama from an abstract point of view.Hujapatia sana chanzo na hitimisho lako. Kwanza, ubepari haukwepeki kabisa bali unatakiwa kusimamiwa kwa vigezo vilivyo wazi na kukubalika kwa wote. Vigezo hivyo ni pamoja na vile vinavyotoa fursa na haki sawa kwa wote huku maadili na sheria vikisimamiwa kwa uwazi na bila kuyumbishwa na chochote kile (blind justice). Aidha, uchumi wa kibepari unaoendeshwa inavyostahili na kwa uwazi, huwatupi kabisa wasiojiweza; hujitahidi kuimarisha huduma za kijamii kama vile za afya na elimu ya msingi kiasi cha kuweza kuwafikia wote. Cha muhimu zaidi, wananchi wakiona mambo yanaeleweka; fursa zipo na zinatolewa kwa haki; matumizi ya rasilimali yako wazi na jitihada za kuhakikisha kuwa zinachangia vilivyo katika ustawi wao zinafanyika - hawapati taabu na tofauti zilizoko kati ya vipato na tofauti za madaraja ya utajiri binafsi.
Kilichopo Tanzania leo hii sio mfumo wa ubepari bali ni kleptocracy (sijui neno sahihi kiswahili). kwa kifupi, ni kuwa uchumi wetu unaendeshwa kwa kutegemea matakwa ya walioko madarakani. Hao ndio wenye kauli ya mwisho. Wanaweza kujitahidi kuonyesha kuwa wanafuata sheria na taratibu (ambavyo navyo vinapindishwa kirahisi) lakini wanachotaka ndicho hatimaye huwa. Wizi wa mali ya umma na rushwa ni mambo ya kawaida. Katika mazingira hayo, uwazi haupo, fursa, haki vinategemeana na ukaribu wako na watawala, ukubwa wa mfuko wako na utayari wa kugawa vijisenti. Falsafa maarufu ni za "mtu kula mezani kwake", "mtu kula kulingana na urefu wa kamba yake", n.k.
Hakuna class struggle ya ukweli hapo. Kinachotutokea ni vurugu zinazotokana na kukosekana kwa uongozi kukiambatana na mfumo uliokithiri wizi na rushwa vikichochewa na unafiki na ubinafsi uliopitiliza (blind greed) wa wengi wetu. Nadhani wanaojali kwa dhati mustakabali wa Taifa hili wamepungua sana. Panya road ni viashiria tu vya kupotea kwa mwelekeo katika jamii hii.
Tumesoma lakini hatujifunzi kutokana na masomo hayo.Naamu! Mawazo ya Karl Marxi bado yanaishi.
Mkuu kwa kweli lazima tuione Tanzania YOTE kama watanzania.
Haipendezi kuona kuna wananchi wanashindwa kupata huduma za lazima kutokana na muundo wa uchumi ulivyo, tukiendelea na muundo uliopo tunajitengenezea an underclass inayoweza kuleta mapinduzi ya kudai hako zao tupende tusipende.
Hivi kama hawa huwa wanaishia wapi? au how much does it take to influence to do something evil considering only he know the survival of the fittest. Mtoto keshabakwa, keshatumiwa vya kutosha kwa namna moja ama nyingine, ukute kesha lazimishwa kuiba tayari au kufanya shoplift na hana pa kukimbilia akiwa mdogo, utamwambia nini ukubwani wakati bado fursa hana.
Ingawa serikari inaweza kuwa na majukumu ya asilimia 70% na sisi kama jamii tuna majukumu ya kuwaelimisha marafiki zetu wasio nacho uzazi wa mpango, tuna majukumu ya kuishinikiza serikari kuchukua hatua za kutatua kero, tunamajukumu ya kuchangia taasisi za misaada ili waongeze huduma wanazotoa, tuna majukumu ya kuchagua viongozi wenye muono wa kero za jamii.
It is a matter of time before proper gangs are formed ambapo vijana wanaishi by the code. Si kwamba ni maajabu kwa sababu hali inapofikia pabaya hayo ndio madhara yake.
Kwakweli lazima viongozi wetu wajipime kama kweli changamoto za leo wanaziweza, hata ukiacha hawa watoto wa mtaani hali ya umaskini kwa Tanzania inatisha basi tu wengine utapeli wa hapa na pale kwa ndugu, jamaa na marafiki unapeleka siku.
Asante kwa kuchangia mada hii na kuitazama froma an abstract point of view.
Haya ndo mawazo mbadala ambayo ningependa kujadiliana nayo mtandaoni.
Hiyo ni licha ya kwamba sikubaliani moja kwa moja na mawazo haya.
Tukubali kuwa sasa hivi kuna matabaka yanayojitokeza kutaokana na uwezo wa kipato na hata kiuongozi.
Na hapa siongelei chama wala itikadi, hizi zinazoanza kujitokeza ni social dynamics.
Kutokana na tofauti zilizopo katika classes za kipato (socioeconomic interests), makundi haya ni lazima yatakinzana.
Na yatakinzana kwa sababu mwenye kipato cha juu, kwake mtu wa kipato cha chini ni just an expendable labour resource.
The driving force kwa mfano sasa hivi kwa the ruling class, economic driving force ni pripitive accumultaion of wealth.
Primitive in the sense kuwa kuna wafanya biashara/viongozi wanaiba, wanapata faida kwa rushwa, wanauza rasilmali isivohhalali(wanyama mbugani), wanafilisi mali za umma-EPA etc.
wakati huo huo mtu masikini na wa kipato cha chini struggle zake zinasukumwa na magonjwa, mishahara midogo isiyokidhi , ukosefu wa makazi, kukosa kazi,vifo vinavyoweza kuzuilika n. k.
Hivyo basi ukisema hakuna class struggle wakati tunaona low level conflicts ambazo hatukuwahi kuziona nchini zinajitokeza kwa kasi, ni kuto appreciate kuwa class struggle ipo na inaendelea kwa kasi.
Mifano ni mingi
Tuna Panya Road, tuna mapigano ya wafugaji na wakulima, wafanya biashara ya mabasi wanaua wananchi kila kukicha-to maximise profits,proloiferation of squatters etc
Hizi ndo dalili zenyewe kuwa tunakoenda ni bomu, tena kubwa tu.
Asante kwa kuchangia mada hii na kuitazama from an abstract point of view.
Haya ndo mawazo mbadala ambayo ningependa kujadiliana nayo mtandaoni.
Hiyo ni licha ya kwamba sikubaliani moja kwa moja na mawazo haya.
Tukubali kuwa sasa hivi kuna matabaka yanayojitokeza kutaokana na uwezo wa kipato na hata kiuongozi.
Na hapa siongelei chama wala itikadi, hizi zinazoanza kujitokeza ni social dynamics.
Kutokana na tofauti zilizopo katika classes za kipato (socioeconomic interests), makundi haya ni lazima yatakinzana.
Na yatakinzana kwa sababu mwenye kipato cha juu, kwake mtu wa kipato cha chini ni just an expendable labour resource.
The driving force kwa mfano sasa hivi kwa the ruling class, economic driving force ni pripitive accumultaion of wealth.
Primitive in the sense kuwa kuna wafanya biashara/viongozi wanaiba, wanapata faida kwa rushwa, wanauza rasilmali isivohhalali(wanyama mbugani), wanafilisi mali za umma-EPA etc.
wakati huo huo mtu masikini na wa kipato cha chini struggle zake zinasukumwa na magonjwa, mishahara midogo isiyokidhi , ukosefu wa makazi, kukosa kazi,vifo vinavyoweza kuzuilika n. k.
Hivyo basi ukisema hakuna class struggle wakati tunaona low level conflicts ambazo hatukuwahi kuziona nchini zinajitokeza kwa kasi, ni kuto appreciate kuwa class struggle ipo na inaendelea kwa kasi.
Mifano ni mingi
Tuna Panya Road, tuna mapigano ya wafugaji na wakulima, wafanya biashara ya mabasi wanaua wananchi kila kukicha-to maximise profits,proloiferation of squatters etc
This class conflict is seen to occur primarily between the bourgeoisie and the proletariat, and takes the form of conflict over hours of work, value of wages, division of profits, cost of consumer goods, the culture at work, control over parliament or bureaucracy, and economic inequality.
(Wiki)
Hizi ndo dalili zenyewe kuwa tunakoenda ni bomu, tena kubwa tu.