The Haya Vocabulary

The Haya Vocabulary

Capt Nemo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Posts
1,445
Reaction score
681
Nadhani si vibaya kushare maneno mbalimbali na machimbuko yake kwenye lugha zetu za asili

Kwa leo mimi naanza na neno "sandauna" kutoka kwenye lugha ya kihaya

Kimsingi hili neno linamaanisha "simple function" yaani kijisherehe ambacho hakina makeke (not complicated)

wengine wanalitumia kwa minajili ya kumponda mtu na sherehe yake kwamba haikufana. Utasikia "sherehe yenyewe ilikuwa sherehe basi? Ni kiji-sandauna tu cha kimtindo!"

Asili ya neno
Enzi zile za ukoloni wazungu (waingereza) walikuwa na utamaduni wa kukusanyika pamoja jioni aidha nyumbani kwa mtu mmoja au popote walipoona panafaa na kujipatia vinywaji kidogo pamoja na bites wakati jua linazama na walizoea kualikana kwa kusema "lets go have some sun-downer" wakimaanisha viburudisho vya kuwapush wakati wa kuona/kuangalia jua linavyozama (sun downing)

sasa mababu zetu walichukulia mkusanyiko huo kama kijisherehe fulani na hapo walitoka na point ya kuhusisha simple drinks na bites na sherehe simple na ndipo lilipozaliwa neno hilo la sandauna likisimama badala ya "sun-downer"

Naomba kushare
 
english sundowner = bantu sandauna
What a linguistic breed!
Thanks Capt Nemo nikilitumia hili neno hapa jf siku za usoni usinikabe koo la copyright tasafali!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom