The Hague: Huwezi kuikwepa

The Hague: Huwezi kuikwepa

2kimo

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
2,029
Reaction score
2,072
Kwa jinsi ilivyo, na ukiangalia matendo na kauli zao wafuatayo the Hague inawahusu sana!
1. Chadema na mwenyekiti wao

Chama hiki hakijawahi kuhubiri amani au upendo. Kama yupo mtanzania amewahi kusikia neno upendo ndani ya kauli za viongozi wa chadema au neno amani likitumika in a positive way, naomba anirushie hiyo reference, naweza kubadili mawazo!
Lakini walipoanza tu kampeni walikuja na haya:-

a. Ccm ni wezi wa kura lkn sasa Yule mwizi tumemchukua "mr. Mwizi" yupo upande wetu. Kauli hii tata inatosha kufanya vyama vingine vikishindwa kujenga dhana kuwa ushindi wa chadema si halali Bali ni ule wa Mr. Mwizi

B. Kauli za kichochezi juu ya kutoiamini tume, wasimamizi wa kimataifa na vyombo vya usalama kuwa vinaibeba ccm! Kauli hizi maana yake ni kuwa hakuna mamlaka inayoweza kuwasimamia cdm isipokuwa chadema, Mbowe na Lowasa tu, huu ndio mwanzo wa mpasuko Mkuu kati ya polisi na wanachama au mashabiki wa CDM kiasi kwamba hadi sasa polisi inawawiu ugumu kudeal nao.

C. Kukaidi sheria, kanuni, taratibu na katiba ya nchi karibu muda wote. Hakuna SAA chadema wamewahi kukubali kufuata jambo kinyume na wanavyotaka wao hata pale walipokuwa wanajua kuwa wamekosea. Wamepindisha taratibu makusudi ili kuleta vurugu! Mfano. Kuvamia mikutano ya wenzao na kuleta ugomvi (rejea- Kyela) kuzomea ktk mikutano au kusimama barabarani na kumzomea mgombea wa chama kingine (rejea- Magufuli Mbeya, Dar na mkuranga) bila ya vitendo hivi kukemewa na chama. Kukaidi kanuni za uchaguzi za kutoa nafasi na Uhuru kwa wapiga kura kupisha vituoni kwa kutakuwa na misongamano hata baada ya mahakama kuamua vinginevyo! Kutoheshimu katiba ya Jamhuri ya muungano kwa kuidharau tume halali ya uchaguzi na kukaidi matokeo ambayo yanapewa nguvu kikatiba.

D. Kutoingilia kati matendo yanayofanywa na mashabiki na wanachama wake hasa ktk maeneo yenye mashabiki wengi kwa kuwadhuru au kuharibu mali za raia wengine.

2. CUF na Maalim Seif
Vitendo cha Maalim kujitangazia ushindi ni kinyume na utaratibu wa uchaguzi na ni kitendo kinachohatarisha usalama wa taifa. Hakuna hadi sasa aliyekemea kitendo hicho kibaya katika historia ya uchaguzi! Tuendelee kuomba Mungu hali ibaki salama kwa Zanzibar lkn kwa vitendo hivyo kulikuwa na dalili mbaya kwa ustawi wa nchi!

3. Mwenyekiti wa uchaguzi Zanzibar (Jecha)
Huyu jamaa ametoa maamuzi ambayo hayakupitia mchakato wowote wamjadala halali. Kweli alikitana na matatizo makubwa labda na mashinikizo ya ndani na nje lakini ulipaswa kutumia tume ya uchaguzi kufikia maamuzi na sio kukamilisha matakwa yake kwa kujenga hoja ambazo athari zake sio kubwa kuliko maamuzi aliyoyafikia.

4. Ccm na Nape
Ccm ilipoanza kampeni ilikuja na kauli tata ya goli la mkono. Kauli hii haikuumgwa mkono na viongozi wengine wa ccm Ila ilitolewa na kiongozi wa juu wa ccm ndugu nape. Si kauli njema ktk kuimarisha usalama wa nchi, ni kauli ambayo imeweza kuleta taharuki na kubakia katika akili za watanzania kwa zaidi ya siku 60.

Kwa kifupi. Ukitazama jinsi hali ilivyo, hadi sasa viongozi wakubwa wafuatao wananafasi kubwa ya kutakiwa kujielezea the Hague(sio lazima wawe na hatia):-

1. Nape

2. Mbowe

3. Jecha

3. Maalim
 
Wee bwabwaja tu.......

Last edited by a moderator:
Usiamshe hasira za watu na kuchokoza vidonda vilivyoanza kupona tafadhali.
 
Kila mtu kasikia na kaona kilichotokea haina haja ya wewe kujifanya umeona au umesikia mpaka uwe unatoa maelezo ya ajabu kiasi hiki.
 
Kwa jinsi ilivyo, na ukiangalia matendo na kauli zao wafuatayo the Hague inawahusu sana!
1. Chadema na mwenyekiti wao
Chama hiki hakijawahi kuhubiri amani au upendo. Kama yupo mtanzania amewahi kusikia neno upendo ndani ya kauli za viongozi wa chadema au neno amani likitumika in a positive way, naomba anirushie hiyo reference, naweza kubadili mawazo!
Lakini walipoanza tu kampeni walikuja na haya:-
a. Ccm ni wezi wa kura lkn sasa Yule mwizi tumemchukua "mr. Mwizi" yupo upande wetu. Kauli hii tata inatosha kufanya vyama vingine vikishindwa kujenga dhana kuwa ushindi wa chadema si halali Bali ni ule wa Mr. Mwizi
B. Kauli za kichochezi juu ya kutoiamini tume, wasimamizi wa kimataifa na vyombo vya usalama kuwa vinaibeba ccm! Kauli hizi maana yake ni kuwa hakuna mamlaka inayoweza kuwasimamia cdm isipokuwa chadema, Mbowe na Lowasa tu, huu ndio mwanzo wa mpasuko Mkuu kati ya polisi na wanachama au mashabiki wa CDM kiasi kwamba hadi sasa polisi inawawiu ugumu kudeal nao.
C. Kukaidi sheria, kanuni, taratibu na katiba ya nchi karibu muda wote. Hakuna SAA chadema wamewahi kukubali kufuata jambo kinyume na wanavyotaka wao hata pale walipokuwa wanajua kuwa wamekosea. Wamepindisha taratibu makusudi ili kuleta vurugu! Mfano. Kuvamia mikutano ya wenzao na kuleta ugomvi (rejea- Kyela) kuzomea ktk mikutano au kusimama barabarani na kumzomea mgombea wa chama kingine (rejea- Magufuli Mbeya, Dar na mkuranga) bila ya vitendo hivi kukemewa na chama. Kukaidi kanuni za uchaguzi za kutoa nafasi na Uhuru kwa wapiga kura kupisha vituoni kwa kutakuwa na misongamano hata baada ya mahakama kuamua vinginevyo! Kutoheshimu katiba ya Jamhuri ya muungano kwa kuidharau tume halali ya uchaguzi na kukaidi matokeo ambayo yanapewa nguvu kikatiba.
D. Kutoingilia kati matendo yanayofanywa na mashabiki na wanachama wake hasa ktk
Well said..wao wanazani hatuna kumbukumbu ya matukio yao kwa sauti na video kama Watanzania..wenye fikra sahihi.

Waliokuw wana rekodi na kutulushia wakiwazalilisha baadhi ya watanzania ambao ni wana ccm waliona fahari
 
yaani nyie kina mama ndiyo hovyo kabisa,ebu acheni unafiki humu ndani,wakati lowassa anatukanwa mlikuwa wapi?wakati magufuri anafanya kampeni mpaka usiku mlikuwa wapi?wakati mkapa anasema hatowapa wapinzani nchi mlikuwa wapi?wakati matokeo yanachakachuliwa mlimani city mlikuwa wapi?msitoneshe mioyo ya watanzania.
 
Naskia sku hiz mnalala palpale Lumumba, au posh imeongezeka!
 
Hii ccm hovyo kabisa wao wanayataka madaraka upinzani wakitaka kugombea utasikia kila aina ya tusi walafi wa madaraka oh wavunja amani vita inakuja
 
Back
Top Bottom