The Grand Egyptian Museum

The Grand Egyptian Museum

Polycarp Mdemu

Senior Member
Joined
Jun 2, 2019
Posts
166
Reaction score
209
Juzi hapa Tuliona Misri ikifanikiwa Kujenga Jengo lake Refu Africa nzima lililoitwa THE ICONIC TOWER ambalo litafunguliwa rasmi mwaka huu 2022.

Hapa tupeane taarifa kuwa mwakani 2023 Misri atafungua Jengo La makumbusho ya Kiakiolojia atayoiita THE GRAND EGYPTIAN MUSEUM, Jina ambalo wengi wameanza kulitumia ni GIZA MUSEUM.

Makumbusho hii itapofunguliwa itakua ndio Makumbusho Kubwa Duniani, Makumbusho hii imejengwa ndani ya Plot yenye Mita square 480,000 na inapatikana Kilomita 2 tu kutoka kayika Pyramid za Giza, Ujenzi wake utagharimu zaidi ya Dola Bilioni 1.

Waliosanifu Jengo hili walipatikana kutokana na kufanya shindanisho la wasanifu majengo (architectural competition) ambalo lilitangazwa 7 January 2002, Misri ilipokea Design zaidi ya 1,557 kutoka nchi 82 hili lilitajwa kuwa moja ya shindano kubwa la usanifu wa majengo kuwahi kutokea duniani likishika nafasi ya pili, huku likipitwa na lile shindano la Kudesign Jengo la World Trade Center huko Marekani.

Architect Róisín Heneghan kutoka nchini Ireland ndio alishinda Shindano hilo kupitia Kampuni yake ya Heneghan Peng, Hii ikamfanya huyu jamaa kuwa moja ya wasanifu mahiri, maana ndio alisanifu jengo la Makumbusho la Palestine,Irish Pavilion, na Airbnb's European Operations Hub, Ushindi wa Usanifu huo uliambatana na Kitita cha Dola 250,000 sawa na Milioni 575 za Kitanzania.

Katika Ujenzi wa jengo hili kiasi cha Dola 330 ni mkopo kutoka Japan na kiasi kilichobaki kitalipwa na Clients ambaye ni Baraza kuu la mambo ya Kale (Supreme Council of Antiquities) pia kutakua na michango mbalimbali na mifuko ya Kimataifa.

Makumbusho hii ikikamilika ndio itakua kituo kikuu cha mawasiliano baina ya Makumbusho zote duniani za Kiakiolojia na ndani yake kutakua na Makumbusho kwa ajili ya watoto na Itaendana na tamaduni za kale za misri.

Kumbuka niliwahi kupostia hapa Meli ya Khufu ikihamishwa kutoka Makumbusho ya Cairo kuja hapa, pia kuna sanamu ya Ramesses II ilihamishwa kuja hapa, vitu hivi kwakua ni vikubwa ilibidi viwekwe kisha jengo ndio liendelee, Na katika Makumbusho hii itapatikana sanamu ya Tutankhamun ambayo hutajwa kuwa Artifact Inayovutia zaidi, Hii ilikua haioneswhi popote, Hata sanamu zilizokua hazioneshwa hapa zitaonekana mubashara, Kiufupi inasemekana artifact zaidi ya 100,000 za utamaduni wa Kimisri zaitakua hapa.

Na Misri imesema inataka ufunguzi wa Makumbusho hii uvunje rekodi ya vitabu vvya Guinness maana ufunguzi utafanyika kwa siku 12 mfululizo.

Mwisho tusimsahau mkandarasi anaetekeleza ujenzi huu BESIX Group hawa ni wakandarasi kutoka nchini Ubelgiji, BESIX Group hutajwa kama Kampuni yakwanza kwa ubora Duniani kwa mujibu wa ENR, Hawa ndio walijenga Jengo la Bunge la Ulaya, Hawa ndio walijenga Jengo refu duniani Burj Khalifa, wakajenga Dubai Canal, kiufupi majengo mengi Dubai wamejenga wao.

Lakini katika Kazi ya Kujenga makumbusho hii Mkandarasi huyo atashirikiana na Wakandarasi wa Kimisri wanaoitwa Orascom Construction, Hawa ni mabingwa wa Kuzalisha zege, wanamiliki pia mitambo ya kutengeneza Cement huko Uhispania, Algeria, Uturuki, N.Corea.

From PinterestView attachment 2228284View attachment 2228283View attachment 2228285View attachment 2228286View attachment 2228282
3db0b4f7b9cc95bd0f945c9c4f47f1f6.jpg
 
Back
Top Bottom