The Golden Words of Hitler

...hebu nionyeshe kiongozi mpigania UHURU mwafrika ambaye hakusukumwa na changamoto za Hayati Garvey!
Si rahisi kwa sababu karibuni wote walimsoma Marcus!
 
mi naomba hitler azaliwe tena kwenye nchi yetu tu basi sio kwa dunia nzima
Samahani, sidhani ya kwamba unajua unachojadili.

a) Ukitaka nchi yako awe na "Hitler" tazama huyu alifanyia nchi yake alichotawala: mamilioni ya watu walikufa, mamilioni wajeruhiwa kwa maisha, robo ya nchi imechukuliwa na majirani, wakazi (milioni 10 Wajerumani kutoka majimbo ya mashariki yaliyotwaliwa na Poland/Urusi) kufukuzwa kama wakimbizi, nchi yote kugawiwa kwa miaka 40. Halafu wanasayansi bora kufukuzwa, kuuawa au kufanywa wakimbizi (tangu Hitler Kijerumani si tena lugha ya sayansi no.1 duniani) Je, una chuki kubwa dhidi ya nchi yako kuitakia "Hitler mpya"??

b) Je unajichukia kama Mwafrika?
Hitler kwa Afrika inamaanisha fundisho katika shule eti watu weusi ni nusu-wanyama, wanafaa kwa kazi ya mkononi ngazi ya chini pekee na ukoloni wa kudumu (ila tu si ukoloni tamu kama Waingereza!).
 
Kuna mkondo wa mawazo kwamba ingawa Adolf Hitler alisababisha maafa makubwa kwa kuanzisha vita kwa sisi waAfrica hiyo ilikuwa kama baraka kwa sababu baada ya vita nchi za wakoloni zilielemewa kiasi cha kwamba ilikuwa rahisi kwa waAfrica kupigania uhuru. Je hii imekaaje?
Sidhani ni vile. Vita Kuu ya Pili iliharakisha kushuka jwa nguvu ya Uingereza na iliharakisha 1) kutokea kwa Marekani iliyoona ukoloni kama mchezo bila faida 2) ilifanya Urusi ya Kikomunisti kuwa nguvu ya kimataifa na kuongeza wasiwasi juu ya ukoloni shauri ya tishio la ukomunisti.

Hakika ukoloni usingedumu hadi leo; kwa sababu kinyume na kile kinachoaminiwa na wengi kwa sehemu nyingi ukoloni haukuwa na faida kwa Uingereza na Ufaransa ulileta gharama zaidi kwa nchi hizi ni kundi la watu tu lililotajirika.
Wasoshalisti ktika nchi hizi walipina ukoloni vikali wangechukua hatua ya kuikomesha hata bila vita ile.

Kwa hiyo Hitler labda aliharakisha mwisho wa uwezo wa kiuchumi wa Uingereza - basi hivyo ndivyo mara nyingi ya kwamba matukio upande mmoja yanaweza kuleta mabadiliko yasiyotegemewa na mtu yeyote kwa upande mwingine. Ila tu historia inaenda jinsi inavyoenda - "Nini ingekuwa kama..." bi swali la kuvutia lakini bila majibu ya hakika.
 
Hapo sijakupata vizuri Mkuu

Mbona bado kuna ukoloni mamboleo?

A) Kuhusu Marekani: Soma hii taarifa ya majadiliano kati ya raisi Roosevelt (Marekani) na Churchill mwaka 1941 walipokutana kabla ya Marekani kuingia vitani.
Roosevelt VS British Colonialism
Ukipenda unaweza kuiita "ukoloni mamboleo" alichomaanisha Roosevelt alkini ni wazi aliona ukoloni wa Uingereza muundo uliopitiwa na wakati na uliokosa faida ya kiuchumi.

B) Ukoloni ni jina kwa muundo maalumu jinsi ilivyoenea wakati wa karne ya 19. Muundo huu umekwisha haupo tena. Kile kinachoitwa "ukoloni mamboleo" machoni pangu ni jina kwa hali mbalimbali za mataifa huru zilizopo katika hali tegemezi na mataifa makubwa. Nadhani ilipotungwa watu waliona kumbe athira ya Uingereza haukupungua. Nani anaona leo tena umuhimu wa Uingereza (nchi isiyo na uwezo kujenga magari tena - viwanda vyote vya magari vya Uingereza ni vya makampuni ya nje) ?
Mimi naona muundo huu uneanguka pekee yake. Gharama zu kuudumisha zilipita mapato yake tayari tangu vita kuu ya kwanza ya dunia.

Afadhali kuwa na nchi tegemezi na faida za kiuchumi badala ya kulazimishwa kuwa na jeshi katika pande mbalimbali za dunia (hasa kwa sababu za nchi za ukoloni kati yao.)
Hata Marekani isiyotaka kuwa na koloni za muundo wa kale ikiwa na jeshi kote duniani kwa kutunza malighafi za lazima imeshagonga mipaka ya uwezo wake.
 
Samahani, sidhani ya kwamba unajua unachojadili.

a) Ukitaka nchi yako awe na "Hitler" tazama huyu alifanyia nchi yake alichotawala: mamilioni ya watu walikufa, mamilioni wajeruhiwa kwa maisha, robo ya nchi imechukuliwa na majirani, wakazi (milioni 10 Wajerumani kutoka majimbo ya mashariki yaliyotwaliwa na Poland/Urusi) kufukuzwa kama wakimbizi, nchi yote kugawiwa kwa miaka 40. Halafu wanasayansi bora kufukuzwa, kuuawa au kufanywa wakimbizi (tangu Hitler Kijerumani si tena lugha ya sayansi no.1 duniani) Je, una chuki kubwa dhidi ya nchi yako kuitakia "Hitler mpya"??

b) Je unajichukia kama Mwafrika?
Hitler kwa Afrika inamaanisha fundisho katika shule eti watu weusi ni nusu-wanyama, wanafaa kwa kazi ya mkononi ngazi ya chini pekee na ukoloni wa kudumu (ila tu si ukoloni tamu kama Waingereza!).
kwa ufupi nataka nchi itawaliwe na dikteta hata kwa miaka mitano tu kwa sababu wakubwa wamejisahau au unabisha?
 
kwa ufupi nataka nchi itawaliwe na dikteta hata kwa miaka mitano tu kwa sababu wakubwa wamejisahau au unabisha?
Si nchi karibu zote za Afrika zilitawaliwa na madikteta tangu uhuru - imesaidia nini? Kinyume chake!
HAlafu: Kwa nini unasema jina la mtu "Hitler" ukitaka kujadili muundo wa siasa?
 
Soma hii taarifa ya majadiliano kati ya raisi Roosevelt (Marekani) na Churchill mwaka 1941 walipokutana kabla ya Marekani kuingia vitani.
Sidhani kama ni sahihi kukubaliana na hawa watu katika kuchambua swala zima la ukoloni manaake wao ndio walikuwa wenyewee!

Tatizo nilionalo ni kwamba zile vuguvugu za kuhamasisa kujitambua na kujikomboa kifikra zilizokuwepo mara baada ya uhuru hivi sasa zimeyeyuka na badala yake akili mgando inatawala barani Africa! Nawasilisha tu.
 
Kwangu hatua kubwa ni kuendeleza Kiswahili. Fikra zinafuata lugha na maneno tunayotumia.
 
Sidhani kama ni sahihi kukubaliana na hawa watu katika kuchambua swala zima la ukoloni manaake wao ndio walikuwa wenyewee!.
Sujui kama umesoma. Sijawahi kusikia ya kwamba kusoma na kuelewa ni kukubaliana.
Ni mfano mzuri jinsi gani wakati ule milki kubwa ya Waingereza iligonga ukuta kutokana na udhaifu wa ndani na upinzani wa Marekani.
 
Sijawahi kusikia ya kwamba kusoma na kuelewa ni kukubaliana.
Hayo majadiliano ya Roosevelt & Churchill sijayasoma. Nadhani ni vyema kukubaliana kutokukubaliana katika swala hili. Hii itasaidia kutokupotezeana muda.
 
Hitler alikuwa mnyama sana na wajerumani wenyewe hawataki hata kumsikia manake kawachafulia historia dunia nzima. Cha kushukuru ni kwamba alishindwa vita zote mbili na kupelekea ujerumani kugawanywa kwa mataifa manne. Kama ageshinda vita nadhani wafrika tungeuwawa wote kama wayahudi halafu Africa ageuze mashamba au holiday camps. Kwa hitler binadamu ni mzungu mwenye mwonekano wa Arier peke yake, kama huna muonekano wa ki arier wewe kwake ni trash. Japo yeye mwenyewe hakuwa Arier... lol

mzee hitler hakushindwa vita kwa uwezo, its just by number of allied soldiers, sometime germans were running out of bullets then they get killed, they had the best weapons and best generals, there tactic are used even by today by major powers! yes hitler was bad on one side only of killing jews apart from that he was just a good leader who believe in super-race theory. its not bad kila kitu kina level yake, mbona hata hapa tz wahaya na wachaga wanajiona ni watu wa superior race kuliko labda watu wa pwani etc

hitler never thought of colonising africa even a bit! he never wanted some cheap labor like other European countries he wanted pure german breed ( aryan race-considered to be superior race of people)
 
Habari zako kuhusu Hitler ni haba sana.

1) Tangu mwanzo wake chama cha Hitler NSDAP kilidai kurudishwa kwa koloni za awali za Ujerumani zilizoondolewa katika mkataba wa Versailles baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya dunia. Katika programu ya madai 25 namba 2 ilidai kufutwa kwa mkataba wa Versailles (iliyoondoa koloni za Ujerumani) na namba 3 ilidai "nchi na ardhi (koloni) kwa kulisha taifa letu na kuwa nafasi wa ajili ya ziada ya watu"

2) Hitler mwenyewe alitafuta ardhi ya koloni katika Ulaya ya MAshariki alipopanga kuvunja Urusi na kuwapa walowezi Wajerumani maeneo makubwa kama mashamba yao ilhali wenyeji Warusi walipangwa kuhudumia kama wafanyakazi nusu-watumwa.

3) Hata hivyo katika chama chake wengi waliota ndoto za koloni kubwa katika Afrika na Asia; mipango hii ilisababisha tukio la ajabu kidogo; hadi 1941 Wajerumani waliwahi kuwa na andiko yao yaani umbo maalumu ya herufi za kilatini; serikali ilipotegemea kushinda vita mwaka 1941 iliamua kubadilisha elimu shuleni na kuwanfundisha wanafunzi wa shule alfabeti ya kawaida kwa nia ya kurahisisha utawala wa dunia maana waliona ingekuwa vigumu kudai mataifa yote yatakayokuwepo chini ya Ujerumani kujifunza alfabeti ya Kijerumani baada ya vita!

4) Kuhusu ubora wa jeshi la Hitler: tumshukuru Mungu wewe si mwanajeshi. Dai langu la kwanza kwa jenerali ni asianzishe vita kama hana uhakika ya kwamba atashinda; vita kuu ya pili haikuwezekana kushinda kwa Ujerumani ilikuwa tendo pumbavu kuianzisha. Sioni ni sifa kama jenerali Wajerumani waliitikia amri za kichaa Hitler. Walisubiri miaka 5 hadi walijaribu kumwua Julai 1944 - hata hii walitekeleza vibaya alijeruhiwa tu.
 
Garvey na UNIA wali-lobi Umoja wa Mataifa wa wakati ule(league of nations), kuwapatia UNIA makoloni yaliyokuwa chini ya Ujeremani .Walisafiri sana kufuatilia hili na pia waliyataka makoloni yaliyo-dorora wapewa(Belgium Congo kama sikosei), UNIA kilikuwa siyo chama repatriation peke yake, repatriation ilikuwa ni sehemu ndogo sana katika itikadi ya UNIA.
Ndugu Rungu hivi nitawezaje kupata nakala ya ' The Black Man' na rekodi za Garvey ?
 
Hayati Kenyatta na Nkuruma walimsoma, kama sikosei Kenya kulikuwa na ukumbusho wa Garvey -jina la mtaa au kitu kama hicho, bahati mbaya Hayati Garvey alijichumia maadui wengi sana ndani na nje ya watu weusi, na watu hawa walimzamisha Garvey hata kabla ya kifo chake weusi hakuwa wakimfuatilia sana. Jina la UNIA lilishuka sana wakati nchi nyingi za AFRIKA zikiomba uhuru, isipokuwa changamoto zake (Garvey) zilikuwa bado juu, alipenda kusema - 'piga galagaza angusha ukweli,ukweli utaamka na ushindi daima'
 
Kwa ninavyofahamu mimi kwanza Hitler akuwa hana niya ya kutawala Africa yote.
kama sikosei aliipenda sehemu ya north africa [Tunusia,moroco na Egypti kidogo.
Huko alimweka kibarakawake fulani aliyeitwa Romel na kuliongoza jeshi la kinazi
kuwaondoa wakoloni wengine ili yeye awe kwenye pawa kwa faida ya Hitler.
Pili pamoja na ukatili wake wote aliyowafanyia wayahudi milioni 6,Hitler aliipenda sana nchi yake
na raia wake. Watu kama HIMLER,GORGO,ROMEL na Hitler mwenyewe walihakikisha kwanza Ger
many na watu wake wanakuwa safe na mengine baadae. Na alikuwa na future ya kuona nchi yake
oneday inakuwa super power. Sema uchokozi wake kwa poland,rusia,france,italy na marekani ndiko
kulikomponza. Stallin,Mousalin,Chuchirl na Nicksoni waliamua kuungana na kumtoa kwenye uso wa
dunia!. Tafauti na viongozi wetu wa kiafrica wanaochukia raia wao na kuzitafuna mali zote ndani ya nchi
kwa faida yao! enzi ya Hitler hawa wote wangenyongwa tu pummmmbffffu
 
Hitler alikuwa na ndoto za "Third Reich" unaelewa hili? Alitaka kutawala dunia nzima.

Hitler alikuwa na ndoto za kutengeneza a "master race" na kuondoa watu asiowataka, alianza na Wayahudi, alichukia weusi, kwa nini unafikiri asingetaka kuua weusi na wengine kuwafungia katika utumwa wakiwafanyia kazi hawa wa "master race" ?
 
Wanaweza kuwepo watu kama yeye, lakini kama watakuwepo kwa Afrika basi watakuwa mafisadi au vibaraka wa nje
 
Hitler alikuwa na ndoto za "Third Reich" unaelewa hili? Alitaka kutawala dunia nzima.

Hitler alikuwa na ndoto za kutengeneza a "master race" na kuondoa watu asiowataka, alianza na Wayahudi, alichukia weusi, kwa nini unafikiri asingetaka kuua weusi na wengine kuwafungia katika utumwa wakiwafanyia kazi hawa wa "master race" ?

Sasa Hitler yeye mwenyewe hakuwa mjerumani hata kidogo, alihamia from Austria. Sielewi kilichofanya achukie watu ambao hawakuwa pure german race yaani Arier...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom