EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,118
Kwa wale wapenzi WA series, kuna series mpya imetoka Kwa sasa ina episodes 2 Tu Ila inaonekana kuwa Moto Sana inaitwa THE ENDGAME.
Bado hatujajua hasa kiini cha matukio haya lakini hii ni sehemu ya utamu WA series hii. Series hii ina ule mfumo WA kwenda mbele then inakurudisha nyuma kupata sababu ya kwanini tukio Fulani linatokea sasa.
Kwa ufupi inaonyesha kuwa kuna binti WA ki Belarus ambaye alikuwa anaishi na Baba yake ambaye alimtrain namna mbalimbali ya kusurvive ikiwemo combat trainings pamoja na kutumia silaha. Sasa siku moja kwenye hayo mafunzo linatokea gari ambalo anaambiwa alilipue Kwa Bomu. Analilipua lakini kunatokea nusura ambaye ni binti mwingine. Sasa baada ya kugundua Hilo wanaanza kumsaka mpaka wanampata, sasa huyu binti anataka kwenda kummalizia Yule binti aliyenusurika ambapo anamchoma kisu tumboni lakini kumbe Yule nusura Yuko vizuri kweli kweli kwahiyo anawaua Yule binti na Baba yake.
Huyo binti jina lake ni Elena Federova ambaye Kwa sasa ndio Queen WA biashara haramu zilizokuwa zinamilikiwa na familia iliyomuokota na kumlea kama mtoto wao. Mwisho anakuja kutaka kufunga ndoa na kijana WA familia hiyo anayeitwa Sergey Vodianov. Lakini siku ya kufunga ndoa kunategwa Bomu kanisani na linapolipuka wanakufa watu wote kasoro wao yaani Elena na Sergey. Mmoja WA marehemu ni mama yake Sergey anaitwa Sophia ambaye pia ndio mama mlezi WA Elena. So wanaapa kulipiza kisasi.
Sasa Elena Yuko mikononi mwa FBI Kwa Siri Sana lakini michezo anayowafanyia wanachoka maana inaonekana hata kukamatwa kwake alikupanga mwenyewe..... Hapo ndioo series inapokuwa tamu
Itafute na hutajuta