The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja

Kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa ccm huko Singida tar 5/2/2016 alisema atahakikisha anafuta vyama vya upinzani nchini.

Kwa hali ya kisiasa nchini kwa sasa haiitaji elimu ya chuo kikuu kulibaini hilo kuwa Magufuli ni adui wa mfumo wa vyama vingi nchini.

Ukiangalia hizi chaguzi ndogo zilizopita pamoja na figisu zake kwa wapinzani unaiona kabisa dhamira mbaya na ovu ya magufuli dhidi ya vyama vya upinzani nchini.
 
Wanabodi,
Hili Jarida la The Economist, kama kawaida yake, kila likiandika kuhusu Tanzania, kwanza lazima limtukane rais wetu, pili lazima litunge vitu vya uongo kuhusu Tanzania, tatu lazima litunge uongo kumsingizia Rais Magufuli jambo lolote na kutangazia ulimwengu.

Katika toleo lake la leo Machi 16, limekuja na kubwa ya mwaka, sio tuu kumsingizia Rais Magufuli kuwa ametamka kufuta vyama vingi, na kuiresha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja ifikapo mwaka 2020, bali pia wamemnukuu na kumlisha maneno kwa quotation kuuaminisha ulimwengu kuwa maneno hayo ni kweli rais Magufuli ameyasema.

Japo mimi sio mfutiliaji wa karibu wa kila hotuba za rais Magufuli, lakini ni msomaji mzuri wa kila kinachoandikwa kuhusu nchi yetu na kumhusu rais wetu, hivyo sikumbuki kuwahi kumsikia maneno haya ya The Economist, aliyatamka lini na wapi?.

Kama kuna mtu yoyote aliwahi kumsikia Rais Magufuli akisema atafuta vyama vingi, mwisho ni 2020, naomba anisaidie.

Kama huu ni uwongo mwingine wa Jarida hili la The Economist, kama kawaida yao na mauongo kuhusu nchi yetu Tanzania na Rais wetu Magufuli, lazima tufike mahali sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali, rais wetu anatukanwa, tunakaa kimya, nchi yetu inatukanwa, tunakaa kimya
Mkuu hilo gazeti ni la wanasiasa walioshindwa mbinu na Magufuli,nilitegemea lihoji kwa serikali kauli hiyo kabla ya kutoka hadharani,ku-balance story,matokeo yake wamechukua maelezo ya chadema inayojifia kwa kukosa ubunifu iwe excuse ya wanachadema.

Naishauri serikali isihangaike kujibu huo uzushi,kwa sababu hata ikijibu the economist halita -publish kanusho hilo,lina ajenda ya siri dhidi ya utawala huu(vita ya kiuchumi).

Ila na imani, nchini kuna wawakilishi wao ,wana balozi zao nchini ,zitatoa ufafanuzi kwa nchi zao kwa haki ,na pia balozi zetu huko nje zisikae kimya kuhusu upotoshaji wowote dhidi ya rais Magufuli na nchi kwa ujumla,ni kazi yao wakiongozwa na nguli wa sheria professor Palagamba Kabudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UONEVU SASA BASI!!!
Twendeni Tukamchangie TUNDU LISSU sasa.

TUNDU LISSU RAIS 2020.
IMG-20190315-WA0024.jpg

"Mopao Mokonzi"
 
Wanabodi,
Hili Jarida la The Economist, kama kawaida yake, kila likiandika kuhusu Tanzania, kwanza lazima limtukane rais wetu, pili lazima litunge vitu vya uongo kuhusu Tanzania, tatu lazima litunge uongo kumsingizia Rais Magufuli jambo lolote na kutangazia ulimwengu.

Katika toleo lake la leo Machi 16, limekuja na kubwa ya mwaka, sio tuu kumsingizia Rais Magufuli kuwa ametamka kufuta vyama vingi, na kuiresha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja ifikapo mwaka 2020, bali pia wamemnukuu na kumlisha maneno kwa quotation kuuaminisha ulimwengu kuwa maneno hayo ni kweli rais Magufuli ameyasema.

Japo mimi sio mfutiliaji wa karibu wa kila hotuba za rais Magufuli, lakini ni msomaji mzuri wa kila kinachoandikwa kuhusu nchi yetu na kumhusu rais wetu, hivyo sikumbuki kuwahi kumsikia maneno haya ya The Economist, aliyatamka lini na wapi?.

Kama kuna mtu yoyote aliwahi kumsikia Rais Magufuli akisema atafuta vyama vingi, mwisho ni 2020, naomba anisaidie.

Kama huu ni uwongo mwingine wa Jarida hili la The Economist, kama kawaida yao na mauongo kuhusu nchi yetu Tanzania na Rais wetu Magufuli, lazima tufike mahali sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali, rais wetu anatukanwa, tunakaa kimya, nchi yetu inatukanwa, tunakaa kimya
Pascal, hawa jamaa tatizo lao ni kupokea kitu{ habari} pasipo kuifanyia UTAFITI.
Kuna wakati wanaandika mambo mazuri na kuna wakati WANABORONGA kwa manufaa wanaojua wao wenyewe na ma bwana wao.

Kumbuka waandishi wa gazeti hilo 75% wako Uingereza not real on the ground.
Hivyo basi wanaandika kile WANACHOPELEKEWA waandike!
Unless MHARIRI mkuu Ms {Susan} Zanny Minton Beddoes ABADILIKE bado watazidi kuandika MAUONGO!
Jambo la kufanya ni ku ignore uongo wao na kuchukua yaliyo POSITIVE kwetu.
 
Nimejaribu kuitafuta nakala ya economist inayoongelea USA kufumbia macho global leadership halfu walivyomchora trump kalala na wigi lake wakati huko kwengine watu wanatupiana mabomu.

If anything kwa economist serikari ya sasa inaipa Tanzanania the headlines for the wrong reasons, hila wanaokiona chamoto kila siku ni viongozi wa mataifa yaliyoendelea wish I could find the image namna walivyomchochora trump na wigi lake kalala wakati USA imejivika jukumu la global leadership.

Mambo kama hayo ayawezi kuwa headline news in USA wakati economist kila siku inakosoa serikari yao
 
Unajua ndugu yangu Pasco unapoteza kabisa focus linapokuja suala la The Economist na matokeo yake hivi sasa umeamua kuwazulia uongo!

Walichoandika The Economist ni hiki:-Hapo kwenye BLUE wameweka hadi quotation mark kuonesha hiyo sio kauli yao bali kuna mtu wamemnukuu!

UKiangalia hapo juu, utaona The Economist wamemnukuu Tundu Lissu ambae ni kweli alitamka hayo maneno!

Na ukisoma hiyo nukuu, Tundu Lissu hajasema Magufuli anataka kufuta vyama vya upinzani lakini maoni ya Tundu Lissu yametoakana na uhalisia wa kisiasa hapa nchini!!

Ni Rais Magufuli ndie alityangaza kupiga marufuku shughuli za kisiasa at national level! Marufu hii inatekelezwa barabara dhidi ya upinzani lakini CCM na serikali yake bado wanaendelea kufanya siasa katika ngazi ya kitaifa!!!

Sote tumeshuhudia assassination attempt dhidi ya TL let alone unknown whereabouts za mtu kama Ben Saanane!

Hivi kuna mjadala kuhusu manyanyaso wanayopitia viongozi wa upinzani?! Sote tumeshuhudia Mheshimiwa Mbowe akifanyiwa fitina na kuwekwa ndani kwa zaidi ya miezi 3 huku akifutiwa dhamana!!

Haina sababu ya kurudia kuelezea matukio! Kila mwenye kutaka kufahamu anafahamu ugumu wa upinzani kurudi bungeni hapo 2020! Itakuwa ngumu sana si kwa sababu CCM na utawala wake wamegeuka kuwa bora bali kwa sababu kuna jitihada za makusudi za kuhakikisha wapinzani hawafurukuti kwa sababu Magufuli anataka bunge litakalopiga mihuri kila agenda yake pasipo na kuhoji!!

NI nini basi tafsiri ya hali hiyo kama sio nia ya Magufuli kutotaka upinzani?! Hivi kweli hata wale wana-CCM wasiopenda unafiki wa kisiasa hawaoni nia hii ya utawala wa Magufuli?!
Lakini kwenye Sherehe za CCM Rais Alisema ifikapo mwaka 2020 kutakuwa hakuna upinzani Tanzania.
 
Wanabodi,
Hili Jarida la The Economist, kama kawaida yake, kila likiandika kuhusu Tanzania, kwanza lazima limtukane rais wetu, pili lazima litunge vitu vya uongo kuhusu Tanzania, tatu lazima litunge uongo kumsingizia Rais Magufuli jambo lolote na kutangazia ulimwengu.

Katika toleo lake la leo Machi 16, limekuja na kubwa ya mwaka, sio tuu kumsingizia Rais Magufuli kuwa ametamka kufuta vyama vingi, na kuiresha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja ifikapo mwaka 2020, bali pia wamemnukuu na kumlisha maneno kwa quotation kuuaminisha ulimwengu kuwa maneno hayo ni kweli rais Magufuli ameyasema.

Japo mimi sio mfutiliaji wa karibu wa kila hotuba za rais Magufuli, lakini ni msomaji mzuri wa kila kinachoandikwa kuhusu nchi yetu na kumhusu rais wetu, hivyo sikumbuki kuwahi kumsikia maneno haya ya The Economist, aliyatamka lini na wapi?.

Kama kuna mtu yoyote aliwahi kumsikia Rais Magufuli akisema atafuta vyama vingi, mwisho ni 2020, naomba anisaidie.

Kama huu ni uwongo mwingine wa Jarida hili la The Economist, kama kawaida yao na mauongo kuhusu nchi yetu Tanzania na Rais wetu Magufuli, lazima tufike mahali sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali, rais wetu anatukanwa, tunakaa kimya, nchi yetu inatukanwa, tunakaa kimya
Kwani sasa tuna vyama vingi?!!...... Kama vipo weka sera tume kama siyo hiyo hiyo ya CCM!
 
Mkuu Paskali tunakushukuru sana kwa kuyaumbua hayo mabeberu ya ze ikonomisti,
Ki ukweli kabisa haya mabeberu yamezidi kumsingizia uongo raisi wetu mtukufu,
Yaani tokea raisi wetu alivyoyazibia mianya ya kuendelea kuinyonya nchi yetu basi hasira zao wamegeuzia kwenye kumsingizia kipenzi chetu, raisi wa wanyonge asiekubali ufisadi na wizi katika taifa letu.
manengelo njoo ujionee mwenyewe leo jinsi Paskali anavyo yashushua mabeberu ya ze ikonomisti.

Maendeleo hayana chama
 
Maongo sana hayo maEconomist, Rais wetu mtukufu,mtakatifu,mungu mtu na kiongozi wa malaika hajawahi sema atavifuta vyama vya siasa ila alisema kufikikia 2020 atahakikisha hakuna vyama vya upinzani Tanzania........sasa hatujui atatumia njia gani ila tunaona VIONGOZI WA UPINZANI WAKIPIGWA RISASI,WENGINE MAGEREZANI MIEZI MITATU ETI WAMEKWEPA DHAMANA,WENGINE WANAUAWA,WENGINE WANAPOTEA WENGINE WANATEKWA, MaEconomist yaache uongo kwani kufanya hivyo ni kufuta vyama vya upinzani
CCM OYEEE
MAENDELEO HAYANA CHAMA.
Sina hakika kama Pascal atahitaji ufafanuzi zaidi.
 
Back
Top Bottom