Fahamu kuhusu kundi la De plow Matz

Fahamu kuhusu kundi la De plow Matz

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
36
Reaction score
55
Tha De-Plow-Matz (mara nyingi hufupishwa kwa: DPT) lilikuwa kundi la muziki wa hip hop lililotamba sana katika miaka ya tisini .

NI Kundi linaundwa na Saigon (jina halisi Saleeh Mzee), Dolasoul (jina halisi Ahmed Dola), Trip Dogg (jina halisi Philip Mwinmanji) na Storm (jina halisi Amour Shamte).

Katika familia hii kulikuwa pia na msimamizi wao aliyejulikana kwa jina la Nkwessa. Awali nyimbo zao walikuwa wanaimba Kiingereza tu. Baadaye wakawa wanaimba Kiswahili huku wakitia maneno ya Kiingereza katika mistari yao.

Asili ya kundi hili lilianza katika mwaka wa 1992 pale Saigon na Tripp Dog walipokutana shule na kuanza kufanya rap kwa kujifurahisha tu. Tangu hapo vijana kadhaa walijihusisha na DPT aidha kwa muda mfupi au muda mrefu.

Katikakati mwa miaka ya tisini Saigon na Stigo wakaungana na DolaSoul ambaye alikuwa amerudi tu kutoka mjini Lagos, Nigeria, ambako huko ndiko alikokulia. Walianza kurekodi nyimbo kadhaa baadaye wakaenda studio kwa P-Funk na Master Jay.

Hili lilipelekea kutengenezwa albamu ya kina De-Plow-Matz. Mtindo wao na hoja zilikuwa zinaburudisha, na hivyo basi wapenzi wa mtindo huo wakaanza kuongezeka. Saigon akiwa anaenda zake nchini Uingereza mnamo 1999.

Na Dola anaamua kuwa msanii wa kujitegemea, kimtindo tu kundi likavunjika bila taarifa kamili ya kufa kwa kundi. Mnamo mwaka wa 2002, Saigon amerudi Tanzania, anakutana na kina Trip Dog na Dola kwa minajili ya kurudisha kundi hai lakini bila mafanikio.

De-Plow-Matz -- 2Rough 2 Tough
Studio : Bongo Records
Producer : Professor ludigo & P funk majani

Chorus:

Two Rough , Two Tough
Two Rough , Two tough
Two Rough , Two Tough
Two Rough , Two Tough
Two Rough , Two Tough

Verse: 1.

Mapambano Bado Yanaendelea/
Fute Nikufute Ni Maisha Ya Kibongo/
Vichaa Wengi wanachacharika Mtaa Wa Congo/
Manzese Mpaka Kariakoo/
Wote Wanapiga Mizingo/
Zote ni Sawa Ingawa Wote Nahesabu Sio Sawa Sawa Sawia/
Ukweli Sasa Mimi Nakuambia/

Saigoni :

Yoh..!!
Siku zinapita , Vita Vinaita/
Ndo Maisha Ya Mtanganyika/
Mwenye Hakika ya Kusikika/
Kweli Nafarijika/
"Mic" Nashika Mshika Mshika Mshika mshika/
Miminika PanapoFika NavyoNudhulika kifo cha udhunika/
Na kipa Na kita kwenye Fani Ka Muzika..

Chorus:

Two Rough , Two Tough
Two Rough , Two tough
Two Rough , Two Tough
Two Rough , Two Tough
Sinza
Two Rough , Two Tough
Kinondoni
Two Rough , Two Tough
Every Where

Verse.. 2.

Balozi:

Niko Taff, Niko Ruff/
Msela kama Mzaliwa , Lakini bado sijajaliwa/
Siku zinazindi kwenda kama Luku , Na check Huku na kule
Wap ninapoweza Kupata Dili Ya chap chap
Kubwa kama Panya Buku/
Huku Nakula Kubwa Nasema Yarabi Toba /
Mshakaji kaniTonya Oya Msela Twende Town kuna Hela/
Moja Chini Mpaka Mjini Speed Mia Moja Ishirini/
Imepaki Gari Nacheck Gari Mshikaji Ameshuka Baada Ya Dakika Ameruka/
Kupata Changu ishia kivyangu Mbele Kwa mbele /
Bila kele Nimepitia kwenye Mitaa sikujua kama leo hii kuna Balaa /
Mateja wamenizungukia kama Pia walitaka kunifanyinzia lakini Tu Ubabe...

Chorus:

Two Rough , Two Tough
Two Rough , Two tough
Ubabe
Two Rough , Two Tough
Arusha na Mikoa Yote
Two Rough , Two Tough
Sinza
Two Rough , Two Tough
Kinondoni
Two Rough , Two Tough
Every Where

Saigon:
endeleeeee mdau...

Baadhi ya nyimbo zao zingine kama kundi ni Turuke kwa furaha ilitoka mwaka 1996 na Are You Down ilitoka Mwaka 1996

Tha_De-Plow-Matz.jpg
 
Inasimitisha sana siku hizi Saigoni kachanganyikiwa.Kurap hawezi tena.Anajifabya anafreestyle hatungi.Matokeo yake akiimba anaharibu kazi alizoshirikishwa.Minato hamna,ladha hamna,ushauri hamna,utulivu hamna.Saigoni wa Sasa ki uwezo wa kurapnsiyo yule wa kipindi kile.
Sijui jamaa ni drug addict
Anyway,things are never the same again.
 
Inasimitisha sana siku hizi Saigoni kachanganyikiwa.Kurap hawezi tena.Anajifabya anafreestyle hatungi.Matokeo yake akiimba anaharibu kazi alizoshirikishwa.Minato hamna,ladha hamna,ushauri hamna,utulivu hamna.Saigoni wa Sasa ki uwezo wa kurapnsiyo yule wa kipindi kile.
Sijui jamaa ni drug addict
Anyway,things are never the same again.
Bangi nyingi mara ya mwisho nmekutana naye mitaa yao ya sinza nlienda msibani,alinifata alikuwa anaongea vitu hata haeleweki ...yule aliporudigi tu toka UK basi ni kama alidata

Ova
 
Back
Top Bottom