The Crisis In Congo..What Can Tanzania Do?

Rubabi

Senior Member
Nov 30, 2006
170
12
Tuwasaidieje majirani wetu Congo?

Thousands flee fresh DRC violence

DR Congo's army is trying to contain a rebellion in the east
Some 28,000 displaced people are on the move in eastern Democratic Republic of Congo after rebel forces attacked nearby army positions, the UN has said.
"They're packed onto the road carrying whatever they can," said Aya Shneerson of the UN World Food Programme in Goma.

The Congolese military said it repelled the dawn raids on targets in Nord Kivu province which provoked the exodus.

The army blamed the attacks on troops loyal to Gen Laurent Nkunda, but the rebels denied they were responsible.

Some 370,000 people have fled three-way clashes this year between the Congolese armed forces (FARDC), the ethnic Tutsi forces of renegade Gen Nkunda and the ethnic Hutu Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR).

Many of the displaced villagers had taken refuge in a string of camps outside Goma, close to the border with Rwanda.

Potential threat

Correspondents say Gen Nkunda has repeatedly failed to live up to promises to integrate his men into the FARDC, under the terms of previous peace deals, arguing that he is defending the Congolese Tutsis, known as the Banyamulenge, from ethnic cleansing.

Gen Nkunda says he is protecting the Tutsis from attack by the Hutus

He has also alleged that the FDLR - made up mainly of Hutus who fled into DR Congo after the 1994 Rwandan genocide - was fighting alongside the Congolese army, a claim the army denies.

At the weekend, the governments of Rwanda and the DR Congo agreed in talks in the Kenyan capital to disarm the FDLR - by force if necessary - in what is seen by the Rwandans as a "change of attitude".

The Congolese government in Kinshasa now considers the FDLR (an amalgamation of former Rwandan armed forces and Interahamwe militia) "a genocidal military organisation in the DR Congo", said a joint statement.

The statement said the DR Congo would "launch military operations, as a matter of urgency, to dismantle the ex-FAR/Interahamwe" .

"I witnessed a change in attitude and language on the part of Congolese officials. There seems to be a new resolve to deal with the FDLR problem," Rwandan Foreign Minister Charles Murigande told a news conference in Kigali.

On Monday he told the BBC that disarming the FDLR would be a "quantum leap towards peace, security and stability".
 
Where does Nkunda get arms to fight?

What happens is spotted and killed like what happened to Savimbi? Will this lead to peace to prevail?
 
Huyu bwana Nkunda ni kibaraka wa Rwanda.Na lengo lake hasa ni kuimega eneo la congo mashariki na kuifanya kuwa nchi kamili nakisha kuiunganisha na Rwanda na kuwa nchi kubwa zaidi.
Mpaka sasa Rwanda inanufaika sana na biashara haramu za rasimali za congo kupitia huyu bwana Nkunda ambaye wanamgambo wake wanamiliki baadhi ya machimbo ya madini na rasilimali nyingine nyingi zikiwemo ngozi za wanyama,timber na madini mengine yenye dhamani kubwa.
Rwanda kwa kupitia wafanyabiashara wake wenye asili ya kitusi ambao wako eneo la Kivu na wengine walioko karibu nchi zote za maziwa makuu wanaelekea kupata faida kubwa katika mfarakano huu na kusema ukweli hawapendi vita hii iishe na ambayo imeacha wacongo wengi ama wakiwa vilema ama kufa kabisa.
Sasa huyu bwana anapata wapi silaha na kiburi chote hicho ni swali zuri sana...huyu jamaa anasaidiwa na serikali ya Rwanda na pia na wafanya biashara wa kitutsi ambao wako eneo lote la maziwa makuu kuanzia Rwanda kwenyewe,Uganda,Congo, Tanzania,Ulaya na marekani.
Sasa ili kuifanya issue kuwa complex zaidi huyu jamaa anatumia hicho kigezo cha kuwalinda hawa wacongo wenye asili ya Rwanda ambao wanajulikana kama banyamulenge ili wasidhuriwe na wale wacongo wenye asili ya kihutu na wale wanamgambo wengine wa Rwanda wenye asili ya kihutu ambao walikimbilia congo baadaya ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa kifupi ni kwamba huyu bwana yeye ndio tatizo kuu la another genocide in congo.Yuko pale kama proxy ya Rwanda na anataka sana mapigano yale kati ya watutsi na wahutu yahamie nchini congo ili atumie fursa hiyo kuiba rasilimali za congo.
Sasa nini kifanyike ni kuisupport serikali ya congo ambayo kusema ukweli imechaguliwa kihalali ili iwalinde raia wake wote wakiwamo wale wenye asili ya Rwanda na nchi nyingine na siyo huyu bwana Nkunda.

Wembe
 
Wembe,
A long term solution is to incorporate DRC in EA Co-operation. Kama Rwanda wanaona wako wengi- when we have a Federation they can easily migrate to other places such as Tz, DRC etc. Angalia Wachagga they have no land at Kilimanjaro- leo wametulia wako kila sehemu popote Tanzania. The same applies to Warundi, Wakenya, Waganda etc. Migration has been a driving force ya maendeleo duniani kote! Leo hii haya mambo ya kisema – mimi Mtusi, Mimi Mluo, mimi Nyiramba- we reach somewhere we call ourselves- East Africans!

Haya mambo ya kupigana for territorial expansion- si mambo ya zamani!
 
Mzalendo, Wembe, bravo!
Haya mawazo ni mazuri lakini nadhani mimi na ninyi sio watunga sera na sheria, huenda kuna mahali panatakiwa marekebisho kidogo katika hili. Kwamba, DRC iwe na ushirikiano na nchi za Afrika ya Kati kama ilivyo sasa. Suala la kuiweka Rwanda ama Burundi katika EAF halikwepeki, ni suala la muda tu, na nadhani kwa mtazamo wangu kama mlivyoshauri hapo juu, litasaidia sana kuondoa chuki ya ukabila iliyopo katika nchi hizo. Wanyarwanda na Warundi wakiruhusiwa kujichanganya na Watanzania Waganda na Wakenya nadhani watajifunza mengi na watasahau chuki zao. Hala kadhalika Wakongo tunaishi nao vizuri tu Tanzania, hebu angali wale wanamuziki pale Dar na kwingine. Binafsi nimeishi nao hao watu, kuanzia hule mpaka maskani, naona wanajichanganya vyema tu na Wabongo wengine.
Labda kikubwa cha kujadili hapa ni kuwa, "Tufanyeje na Watu wa Jamii ya Nkunda"?

Nini kifanyike ili ndugu zetu Wakongo wajisikie wako kwao?
 
Tanzania tumekuwa na amani sio kazi ndogo ambayo Mwalimu aliifanya tena single handed leo hii mnataka miungano mingine mbona huo wa Zanzibar tu unatushinda na wao wako chini ya million moja. Mnataka tuungane na kila nchi tunayopakana nayo ili iwe nini? Once a killer you will always be.

Tumewasaidia sana majirani zetu na shukrani ya punda ni mateke, huwezi kumlazimisha punda kunywa maji kisimani. Kama wanataka kumalizana waachane wauane sisi sio kazi yetu, mbona Somalia wote ni kabila moja na hakuna nchi hivi sasa? Misingi ya amani Tanzania ilijengwa kwa gharama kubwa na siyo kitu kizuri kufikiria kirahisi rahisi kama wengi wanavyofikiria.
 
Dua,
Hii kali!
 
Analysis nzuri dua na wembe.Mimi naamini kuwa watu aina ya Nkunda wana sababu zao za kuendeleza vita Congo na ni kweli moja ya sababu hizo ni kuiba maliasili.Sasa kwa nini anaendeleza vita wakati bado kuna UN na wamemuaidi watawalinda banyamulenge?

Congo ni tatizo letu watanzania pia, nchi hii ikipata amani tunaweza kupata manufaa mengi kwa mfano umeme wa bei nzuri sana(inasemekana congo kuna potential a kupower africa nzima kwa umeme wa maji)isitoshe wacongo wengi wanaongea kiswahili,kwa hiyo biashara na tanzania inawezekana kabisa.Sasa kibaya ni kwamba utajiri wote wa congo unaenda/kuibiwa na wazungu na wachina ....timber cobalt, uranium n.k.

Kazi ipo.
 
Nini kifanyike ili ndugu zetu Wakongo wajisikie wako kwao?
Jenerali Nkunda ni mtu mbaya sana pamoja na host wake Rwanda wanasababisha maisha ya wakongo kuwa ktk hali mbaya sana. UN forces wapo pale nao ndio wajinga wakutupwa. Majeshi ya serikali yanauwezo wa kupiga huyo Nkunda lakini tatizo kubwa ni UN forces (MONUC), Kabila akitaka kumpiga Nkunda hao MONUC wanasimama katikati kwamba wanahitaji maelewano ya mezani wakati Nkunda akiwavizia anafanya kweli. MONUC anatetea kazi yake pale kuwepo kwake mkono unaenda kinywani na kazi yake inaonekana kama kuna fujo kama hizo. Kabila kama si kuzuiliwa na MONUC angelikuwa ameshamaliza kazi siku nyingi maana ana uwezo wote, na sababu ya kumpiga anayo_Operation yoyote ya serikali dhidi ya Nkunda si ya siri inatangazwa ili watu wajiandae hivyo wakisikia MONUC wanawahi kusimama katikati ili kuzuia majeshi ya serikali kumpiga Nkunda na kuowaomba wakae waongee si kwa fujo lakini Nkunda mwenyewe akitaka kufanya shambulio hasemi na anashtukiza na kusababisha vifo vingi vya raia. Fujo zote hizo unasikia bado zinaendelea ni kwa sababu ya MONUC.
 
Du sasa basi ndo jawabu Nkunda is to sport him by satellite- na kumtungua kama Savimbi! Haiwezekani miaka nenda rudi bado tunabembelezana na Nkunda.

Then DRC iwe invited to join EAF- after all Kabila (Jr) alikulia Dar na anajua thamani ya amani! DRC nao wataelewa tu taratibu!
 
Tanzania tumekuwa na amani sio kazi ndogo ambayo Mwalimu aliifanya tena single handed leo hii mnataka miungano mingine mbona huo wa Zanzibar tu unatushinda na wao wako chini ya million moja. Mnataka tuungane na kila nchi tunayopakana nayo ili iwe nini? Once a killer you will always be.

Tumewasaidia sana majirani zetu na shukrani ya punda ni mateke, huwezi kumlazimisha punda kunywa maji kisimani. Kama wanataka kumalizana waachane wauane sisi sio kazi yetu, mbona Somalia wote ni kabila moja na hakuna nchi hivi sasa? Misingi ya amani Tanzania ilijengwa kwa gharama kubwa na siyo kitu kizuri kufikiria kirahisi rahisi kama wengi wanavyofikiria.

Dua, suala la kuwasaida hawa lina mantiki kubwa sana na muhimu. Hawa jamaa wakianza kupigana wanakimbilia huku kwetu na tunawalea kama wanetu, kwani UNHCR hawana msaada mkubwa kwa hawa wakimbizi. Sasa basi, kama kwao hawa jamaa kutatengemaa basi na sie tutapungukiwa na mzigo wa kuwalea hawa wakimbizi. Fikiria suala la Somalia, wakimbizi wao toka miaka ya sabini hadi leo bado wako pale Chogo, Muheza, na wengine wanaendelea kumiminika kila leo. Wakongo bado wako Rukwa na Kigoma, hali kadhalika Warundi na Wanyarwanda. At least tukiwaunganisha Wanyarwanda na Warundi na wabongo angalau watapunguza vurugu kwao na wataungana na Watanzania kuishi kwa amani, kwani hata sisi tutakwenda kushi kwao na kusaka maisha.
Suala la Zanzibar nadhani kada mpinzani atafafanua vizuri, kwani mie bado mpaka leo nashindwa kuelewa mazingaombwe ya chaguzi za Zenji na mambo ya kutumia dola kupachika watu madarakani.
 
Where does Nkunda get arms to fight? What happens is spotted and killed like what happened to Savimbi? Will this lead to peace to prevail?

Huyu Nkunda anapata silaha kutoka kwa kagame. Lengo ni kuwamaliza Interahamwe waliokimbilia kongo kujipanga upya ili kumuondoa kagame madarakani. Mhutu anasema hawezi kutawaliwa na "cockroach" (i.e., mtutsi. Mtutsi naye anadai hivyohivyo. Ndio maana hawa Interahamwe wameingia msituni kongo ili kuweza kuikomboa nchi yao kutoka kwa watutsi. Kumbuka hata kagame alivyotwaa madaraka alisema ameikomboa rwanda kutoka kwa wahutu. Akabadilisha kabisa hata bendera ya rwanda.Yaani ukifuatilia siasa za hapo rwanda, utalewa bila kunywa!!!Kagame ana wasiwasi wa kufanyiziwa kama alivyomfanyizia habyarimana.
 
Unajua kuna baadhi ya watusti wanasema kuwa wao ni moja ya makabila ya wana wa-Israeli yaliopotea na wanaamini kuwa wao ni superior kuliko wengine?
 
Unajua kuna baadhi ya watusti wanasema kuwa wao ni moja ya makabila ya wana wa-Israeli yaliopotea na wanaamini kuwa wao ni superior kuliko wengine?

Hawa Watusi- kaazi Kweli Kweli!
With EA Fed. Watutsi watakuwa huru kwenda popote- na mawazo yao yatapanuka beyond the borders of Rwanda!
 
Ni kweli Kagame anaishi kwa tahadhari kubwa kupindukia. Mie nilitembelea Rwanda mwaka jana, ukipita karibu na mtaa unaoelekea kwenye barabara inayoelekea huko ikulu kwake, ulinzi unatisha. Askari wamesambazwa toka mbali sana na ikulu, wako na automatic guns za kisasa, yaani katika mkao wa action saa yoyote. Si kama kwetu Bongo unaweza kuzunguka ukuta wote wa ikulu bila kukutana na askari mwenye silaha hata mmoja. Bongo askari wenye silaha utaanza kuwakuta main gate, lakini barabara zote zinazozunguka utakutana tu na machinga wanaouza karanga na pipi, na kama ni alfajiri au jioni utakutana na wale tumbili.

Sasa ukutane na msafara wa Kagame akielekea airport. We! Utadhani ni kikosi cha kivita kinahamishwa, wanaume wako kwenye magari ya wazi na mavazi rasmi ya kivita (yale ma-camouflage), machine guns zinachungulia kila upande. Hapo mwanaume Kagame anakwenda kupanda ndege, wacha mchezo bwana!
 
Mkuu Kithuku, uko sahihi kabisa kwa maelezo yako.
Kama jamaa alichukua nchi kwa mtutu unadhani hakuna anayewaza kufanya hivyo hivyo kwa Kagame? Lazima awe na tahadhari. Hali kadhalika, hali hii inachagizwa sana na yeye kushtakiwa Ufaransa kwa kashfa za makosa dhidi ya ubinadamu, kwa hiyo anahofu kuwa anaweza kukamatwa wakati wowote na kupelekwa huko, kwa hiyo lazima akae 'Mkao Wa Tahadhari'. Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.
Ila mie namshauri Kagame kuwa, 'Kipimo unachowapimia wenzio, nawe utapimiwa hicho hicho, ila cha kwako kitashindiliwa na kusukwasukwa', kwa hiyo hata kama atajilinda namna gani, kuna siku atapatikana tu. Akumbuke ya akina Mobutu, Kabila, Taylor na sasa tunamsubiri babu Mugabe.
 
Haya hizi Rwanda batalions zilipelekwa just fews weeks ago kumsaidia Gen. Laurent Nkundabatware(Nkunda)soma attachement ya kwanza.

Halafu hiyo attachement ya pili ni jinsi majeshi ya Rwanda (RPF) yalivyowauwa wakongo na wahutu mwaka 1997 wakati majeshi yao yakipigana along side na yale ya Laurent Kabila...Je nao(RPF) wapelekwe kwenye mahakama za umoja wa mataifa kujibu mashitaka ya mauji ya wakongo???? maana nayo ni genocide vilevile.
 
Attachments

  • DOC_FDLR_PAGE04_0000000387.pdf
    54.3 KB · Views: 90
  • DOC_FDLR_PAGE05_0000000393.pdf
    10.1 KB · Views: 78
Kule Angola bwana Jonas Savimbi alihangaisha sana maisha wa wanaangola lakini baada ya vita ya mda mrefu bila kuchoka aliuawa na ndo ukawa mwisho wa matatizo kule Angola. Hata DRC inabidi wafanye kweli kama walivyofanya Angola, watumie makomandoo wanaoweza kumfikia huyu nduli mwuuaji nkunda na kumakamata na kumumalizia kwa mbali, ameshaleta shida nyingi sana kwa watu wasio na hatia, siku zake zinahesabika.
 
Kule Angola bwana Jonas Savimbi alihangaisha sana maisha ya wanaangola lakini baada ya vita ya mda mrefu bila kuchoka aliuawa na ndo ukawa mwisho wa matatizo kule Angola. Hata DRC inabidi wafanye kweli kama walivyofanya Angola, watumie makomandoo wanaoweza kumfikia huyu nduli mwuuaji nkunda na kumakamata na kumumalizia kwa mbali, ameshaleta shida nyingi sana kwa watu wasio na hatia, siku zake zinahesabika.
Pia vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa vingekaa mpakani kati ya DRC na Rwanda maana huko ndo anakopatia siraha na mahitaji yake mengine.
 
Back
Top Bottom