Kweli kabisa. Suala hili la Computer inatakiwa tuelimishane, kuna mambo mengi hatuyafahamu nikiwemo mimi mwenyewe. Kwa hiyo naomba nielimishwe kuhusu yafuatayo:
1. Nasikia kuna vitu kama Antivirus, Firewall. Je kazi ya vitu hivi ni nini?
Kwa uelewa wangu Antivirus inafanya kazi ya kuzuia virus wasiingie kwenye Computer, vile vile Firewall inafanyakazi kwa kusaidiana na Antivirus kuzuia Virus.
Naomba mwenye elimu zaidi kuhusu vitu hivi atuelimishe, maana sisi tunatumia tu Cmputer kwenye mtandao na pengine hatujui namna ya kuilinda hasa kutokana na virus.