Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,181
- 5,321
THE BOOK OF THE DEAD ni jina linalo-mislead ukweli fact ni kuwa hili ni jina la kubambikiwa tu na lilianza kutumika katika karne ya 19, vitabu au kurasa za maandishi haya yalikuwa yakiandikwa kwenye msahafu au scrolls na kuwekwa pembeni ya wafu wanapokuwa wamepumzishwa katika nyumba zao za milele (chanzo cha kuitwa vitabu vya wafu),
Tunatambua kuwa wenzetu walitumia sana mapiramidi kuzika watawala wao ambao ndiyo hasa walikuwa walengwa wa maandishi haya kwa nia ya kujitwalia maisha mazuri soon wakifika huko afterlife waendako wapokelewe vyema na wenyeji wao.
Iliaminika kuwa nguvu za uovu(power of evil) uwinda roho za wafu pindi wawapo njiani kuelekea kuzimu katika ufalme wa mtawala wa huko yaani mungu OSIRIS.
Miungu wakuu hata wao waliofia kukumbwa na uovu huu hivyo nao walijilinda dhidi yake kwa manuizi (spells) na magical names pamoja na maneno yenye nguvu ambayo yalibuniwa na kuandikwa na mungu THOTH.
Iliaminika kuwa mungu jua Ra (the sun god Ra) alikuwa na neno la siri alilopewa na THOTH ambalo halilitumia kupambana kipindi cha machweo ya jua kuyakabili mapepo hayo au great devil hili kuweza kuleta nuru yake mchana.
Book of the Dead iliwezaaminika kuwa ingeweza kumpa mwanadamu uwezo wakushinda duniani na katika ulimwengu mwingine, itamwakikishia usalama na kupenya kwa urahisi kuzimu(underworld) na itampa Uhuru wa kuingia na kutoka kuzimu na kumzuia kufa mara ya pili, hili liliwezekana tu kwa mwanadamu huyu kuweza kuyaelewa na kurecall maneno yote yaliyopo ndani ya kitabu hiki kabla na hata baada ya kwenda huko aendako akifa.
Na hili kufanikiwa ilipaswa kujitakasa kwanza kwa kutoshiriki tendo la ndoa na wanawake, usile samaki wala nyama na uhakikishe unakuwa msafi kimwili na kiroho.
MIUNGU WAKUU
Amen Ra "King of the gods" Mungu wa miungu, "The lord of all the gods" Bwana wa Mabwana"
Osiris " the giver of evalasting life" huyu ndiye mungu mtoa uhai na mpaji.
THOTH mwandishi na mtunzi wa kitabu cha wafu; kimisri wanamtambua kama Tehehuti au Tehuti.
Kitabu cha Wafu inahaminika kuwa ni moyo na akili ya muumba, pia huitwa Pautti na wenyeji huku wageni wakikitambua kama Ra.
THOTH pia ni ulimi wa muumba usemao kwa sauti juu ya kusudio lake na kuamua kila kilicho juu ya mbingu na nchi vipate tokea. Thoth aliumba vyote vya angani na duniani ikiwemo jua, mwezi,maandishi, designs, Sanaa, mahesabu na milinganyo yake.
Kupitia sifa yake ya utunzaji wa kumbukumbu za Mungu aliitwa pia "Recording Angel" yeye ndiye inventor wa physical and moral law inayompa personification of JUSTICE (mtenda haki) na hili linatokea kufuatia kundi la miungu mbinguni, duniani na sehemu zingine za ulimwengu kumtawadha/kumtunuku uwezo wa kusema na kutekeleza juu yao na hakika Neno lake halitiwi shaka wala kuulizwa kama liko sahihi maana hakika ni kweli na ukweli mtupu.
"They appointed him to weigh the words and deeds of men, and his verdicts were unalterable, he become more powerful in other world than Osiris himself."
Osiris alijitwalia ushindi wa nguvu dhidi ya Set katika ukumbi mkuu wa hukumu ya miungu kupitia msaada wa Kinywa cha busara na hekima cha THOTH kama wakili au advocate na pia kwa ushawishi aliokuwa nao kwa miungu wa mbinguni.
Na kila amfatae OSIRIS hana budi kumwamini THOTH ili kuwa salama na kujiepusha na adhabu kali siku ya hukumu na kuhakikishiwa makazi ya milele katika ufalme wa OSIRIS.
Kama ambavyo THOTH aliweza kumtetea OSIRIS katika kesi yake na akashinda vivyo hivyo wamisri pia utegemea atawatendea vivyo hivyo pindi wakitangulia mbele ya haki.
OSIRIS mungu wa taratibu na kanuni(sheria), uzazi wa Nile, alikuwa incarnate(alizaliwa tena) duniani kama mtoto wa GEB, "mungu wa dunia" na NUT "mungu mke wa anga" Ana dada zake wawili ambao ni ISIS na NEPHTHYS na kaka yake mmoja SET.
OSIRIS alimuoa ISIS na SET alimuoa NEPHTHYS. GEB akamteua OSIRIS kukaa kwenye kiti cha ufalme wa misri na akafanikiwa kutawala kwa ustadi na ubora uliotukuka kiasi kwamba nchi ikastawi na kuwa yenye furaha kipindi chote cha utawala wake.
SET kwa kuliona hili akaingiwa na wivu dhidi ya kaka yake na akatamani kumchinjilia mbali ili haweze kujitwalia kiti cha ufalme na ISIS ambaye reputation yake kama mke mwaminifu na mwenye mapenzi ya dhati kwa mumewe na mwangalizi yaliujazia sifa utawala wa mumewe OSIRIS. Hivyo kwa namna moja au nyingine suala la kumwangamiza lilikuwa haliwezi kuzuilika jambo ambalo SET alilifanikisha kwa kumuua nduguye kwa kumzamisha majini.
Stori nyingine katika kisa hiki hiki yadai kuwa ISIS akisindikizwa na dadaye NEPHTHYS walienda huko Nefat, wakafanikiwa kuuchukua mwili wa OSIRIS na kwa msaada wa ANPU, kijana wa mungu jua Ra. Walifanikiwa kumrejeshea uhai temporary kabla ya kufa tena na mkewe ISIS akatumia nafasi hiyo kujipatia mimba na akamzaa mwanae ajulikanae kwa jina HORUS.
Ilikumwepuka SET ambaye katika kesi moja aliwahi muua HORUS kwa kumtumia scorpion amng'ate, mama yake yaani ISIS alitumia muda mwingi sana kukimbia huku na huku akiwa pande za huko delta hili asiingie mikononi mwa adui.
Kwa kipindi chote hiki ambacho ISIS na mwanae HORUS wakitaabika bila furaha ni THOTH ndiye aliyekuwa akiwasaidia katika magumu yote, akiwapatia neno lenye nguvu na faraja iliyomrejeshea HORUS uhai wake nakuvuka baadhi ya vikwazo vya mamba na viumbe vya ajabu huko delta.
HORUS alivyokuwa mkubwa akaahidi kulipiza kisasi kwa kum-revenge baba yake OSIRIS. Siku ilipowadia akakutana na SET vita ikapiganwa haswa mpaka SET akazidiwa akiwa katika zile hatua za kuangushwa chini akawahi na kumchana katika jicho la kulia HORUS hivyo akalitunza na kuondoka nalo.
Hata baada ya vita hivi HORUS alikuwa na maumivu makali na akuweza kupata tena nguvu ya kumdhibiti SET hivyo SET akamchukua ISIS lakini THOTH akaingilia kati na kumfanya SET arudishe jicho la HORUS ambapo THOTH aliamua kulipachika katika paji la uso wa HORUS na kuliamuru lirejeshe nuru yake kama awali.
Kupitia maelekezo ya THOTH, HORUS aliambatana nae kwenda kuzuru alipozikwa baba yake(OSIRIS) na akamfufua. Katika kumfufua huko lile jicho la HORUS likang'olewa tena na kupewa OSIRIS baba yake alimeze na mara baada ya kufanya hivyo akawa na nuru ndani yake huku akiibuka na cheo cha ushindi dhidi ya kifo na kuwa Lord of the Dead and King of the Underworld "BWANA WA WAFU NA MFALME WA KUZIMU"
Hivyo kupitia hili OSIRIS akawa type na symbol of resurrection (ufufuo) kwa jamii ya wamisri kwa miaka yote, kwa sababu yeye ni mungu ambaye kiasili ni Immortal kwa kufufuka kutoka katika mauti.
NB: Ni imani yangu kuwa nje ya kuburudika na simulizi hili, kuna jambo au baadhi ya mambo umeyang'amua na yamekupa picha fulani au majibu juu ya maswali ambayo umekuwa ukijiuliza juu ya imani yako.
Nikusii usikose sehemu ya mwisho ya masimulizi haya marefu ambayo nitajitahidi kuyafupisha kwa kadri niwezavyo hili usikose uhondo na mtiririko muruwa wa stori hizi muhimu za kale.