The Bold Bulletins

The Bold Bulletins

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
6,557
Reaction score
25,748
Sasa, unaweza kupata nakala za Kitabu changu cha "NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI".
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-

Pia waweza kupata kitabu changu cha "OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI"
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-

Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457

Au bofya link hapa chini kunitumia ujumbe moja kwa moja whatsApp


Huu utakuwa ni uzi wangu maalumu ambao nitakuwa naweka maandiko mafupi mafupi (bulletins). Makala ndefu zitaendelea kama kawaida kwenye nyuzi nyingine lakini hapa nitakakuwa naweka vitu kwa ufupi sana na mara kwa mara.

Karibuni.


Bulletin # 1

VIWANDA VYA KUCHAKATA TAARIFA.??


46ac0456a109a87d1c23d723fe407d24.jpg


dd650842a9d42b5edb5aa35187d6426c.jpg



Kama mtu akikuuliza maswali yafuatayo, unajisi majibu yako yatakuwa ni yapi?
1. Jengo la picha namba moja unahisi linahusiana na nini?

2. Jengo la picha namba mbili ni nyumba ya kuishi au hoteli?

Nina amini kabisa majibu mengi yatakuwa kama ifuatavyo…
1. Jengo namba moja ni kiwanda… na inawezekana ni kiwanda kinachohusiana na masuala ya nishati au kemikali.

2. Jengo kwenye picha namba mbili ni aina ya hotel ya nyota tano.


Majibu mengi yatakuwa yanafanana na hayo hapo juu na kwa kawaida utakuwa sahihi kabisa… isipokuwa tu hautakuwa umepatia hata nusu ya jawabu.

Picha zote mbili ni picha za kituo data (data center).

Katika karne ya 18, 19 na 20 wafanyabiashara wenye mitaji mikibwa na makampuji walikuwa wanajenga majengo makubwa ya viwanda. Na wale ambao walikuwa mahiri kwenye uanzishaji na uendeshaji wa viwanda ndio ambao walikuwa wanashamiri kwa kipato na hatimaye kuwa matajiri.

Matajiri wote wakubwa wa miaka hiyo… toka kwa wanasayansi na wagunduzi kama Thomas Edison mpaka kwa mabepari kama John D. Rockefeller... utajiri wao ulitokana na umahiri wao wa kuanzisha na kuendesha viwanda.

Lakini katika hii karne yetu ya ishiri na moja… utajiri unatengenezwa kutokana na umahiri wa mtu au kampuni kuchakata na kutumia taarifa.

Leo hii kampuni zenye mitaji mikubwa zaidi ni zile ambazo zinahusika na masuala yanayogusa taarifa. Mfano leo hii tukiangalia kampuni kumi yenye mitaji mikubwa zaidi duniani… kampuni tano za kwanza zote zinahusika na masuala ya taarifa.

1. Apple
2. Google
3. Microsoft
4. Facebook
5. Amazon

6. Berkshire Hathaway
7. Exxon Mobile
8. Johnson & Johnson
9. JPMorgan Chase
10. Tencent Holdings

Kampuni hizi za teknolojia za mawasiliano umahiri wao na ubunifu wao wa kuchakata taarifa ndio umewafanya kuwa 'giants' wa biashara za karne hii ya ishirini na moja.

Lakini swali moja muhimu ambalo mara myingi haliangaliwi ni namna gani kampuni hizi zinaweza kuhimili ukubwa na wingi wa taarifa hizi zinazopita mikononi mwao kila sekunde.

Kwa mfano Facebook ina watumiani bilioni 1.37 kila siku. Watu hawa wanatumiana jumbe za maandishi, picha, video na pia wanatumia kitufe cha "Like" na kadhalila. Ni namna gani ambavyo Facebook inahimili ukubwa huu wa watumiaji na data kila siku??

Picha hizo hapo juu ni moja wapo ya majengo ya Facebook ambayo yanahifadhi 'server' za facebooks (Data Center). Kampuni ya Facebook ina Data Center kama hizi kadhaa maeneo mbali mbali duniani. Kwa mfano hii pekee pichani iliyoko Priveville, Jimboni Oregon nchini Marekani imegharimu kiasi cha dola za kimarekani Milioni 450 (kama shilingi Trilioni moja ya Kitanzania) kuijenga mpaka kukamilika.

9692a43ddf0a3065d5c18867b46f8d8b.jpg


Jengo hili lililojengwa kwenye shamba lenye ukubwa wa futi za mraba 350,000 (kama viwanja vitatu vya mpira wa miguu) hapa ndipo kila kitu ambacho unakifanya kwenye mtandao wa Facebook kinahifadhiwa.

Jengo hili linatumia umeme wa Megawatt 30 na ina majenereta makubwa ya umeme wa akiba 14 ambalo kila moja lina uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawatt 3 kama ikitokea umeme wa kawaida ukizimika.

Jengo hili limejengwa kwa mfumo maridhawa ili kuwezesha ufanisk wake wa kutenda kazi. Kwa mfano, jengo lenye server kubwa kiasi hiki lazima litakuwa linazalisha joto kubwa kutokana na server hizo kufanya kazi. Kwa hiyo lazima kuwa na mfumo maridhawa wa kuratibu kiwango cha joto katika jengo kama hili.

Kwa mfano kompyuta ya kawaida inaratibiwa joto lake na 'hit sync' yenye ukubwa wa kufanana na kasha la kiberiti. Jengo hili la Facebook joto lake linaratibiwa na mfumo complex wa uliopo kwenye paa la jengo ambao una mfumo wa hewa wa kutosha vyumba saba vikubwa.

Hewa inanyonywa kutoka angani, kisha inachujwa na kuwekwa ubaridi mkali na baada ya hapo inaingia kwenye 'chumba' maalumu ambacho inapashwa tena joto na kuongezewa/kupunguzwa unyevu kidogo mpaka kufikia kiwango ambacho ni sahihi kuingia kwenye 'hall' lenye severs.

Upande mwingine kuna 'feni' kubwa ambazo zinapuliza muda wote ili kuondoa hewa hii ilivyoingia kila baada ya muda fulani ilinkupishwa hewa nyingine 'fresh' kuingia.

Kutoka na ukuaji wa haraka kila siku wa mtandao huu… server mpya zinawasili kwenye vituo hivi kila siku. Facebooks wenyewe wanaeleza kuwa kwa sasa kwa mfano kituo hiki cha Prineville pekee kina hifadhi zaidi ya Pentabyte 700 za picha na video za watumiaji wa facebook (Pentabyte moja ni sawa na Terabyte 1000 kwa hiyo hii ni sawa na kusema kuchukua Terabyte 1000 zidisha kwa 700).

208cf03590c21679dd5b2d26e643234b.jpg


Moja ya Jenereta 14 za Disel za umeme wa dharura... kila jenereta ina uwezo wa kuzalisha 3 Megawatt za umeme

aec734ebb923e0e0bb88b371fe78d4f5.jpg


Sehemu ya mfumo wa feni zinazotumika kusukuma hela iliyonyonywa kutoka angani na kuipeleka kwenye hall lenye servers.

6370bc71513f96db20b88ca7816f4772.jpg


Hapa ndipo ambapo hewa inachujwa na kuongezewa/kupunguziwa unyevu kabla ya kuingia kwenye hall lenye servers

be45f63599ed19754e8858c696369cba.jpg


Sehemu ya rows za Server... ukibofya tu "facebooks.com" au "instagram.com" au "whatsapp.com"kwenye simu yako au kompyuta... probably taarifa hiyo inafika hapa na kisha kuaccess 'profile' yako ambayo imehifadhiwa kwenye moja ya hizi servers... na hii yote inatokea ndani ya muda mfupi kuzido hata theluthi ya sekunde

dd1eef05cf46a894046e6cf32a44c9c1.jpg


Jengo lingine jipya linajengwa hapa hapa Prineville kwa ajili ya kuhifadhi server nyingine kutokana na ukuaji wa haraka na mkubwa wa watumiaji wa mtandao huu wa kijamii

Nyongeza....

2abe55bbe7ed807f811fd321a1f248ca.jpg


Hii ni data center ya kampuni Apple

f1382aa367c1235304abd2a982768441.jpg


2fd4ae3429ca6e9de32d02df79d46476.jpg


Hii ni Data center ya kampuni ya Google

Huo ndio ulimwengu 'wao'... na huku tulipo ndio ulimwengu wetu. Wakati sisi tunahangaika kujenga viwanda vya kutengeneza panado... wenzetu wanasugua bongo namna ya kujenga "viwanda" vya kuchakata na kuhifadhi taarifa. Na huko ndiko utajiri na kushamiri kunakopatikana katika karne hii ya ishirini na moja.


Jiunge na Group langu la WhatsApp kusoma simulizi mpya kila siku. Kuna malipo ya 5,000/- kwa mwezi. Wasiliana nami 0759 181 457



Siku njema chiefs,
Habibu Anga alias The bold - 0718 096 811
To Infinity and Beyond


Follow, Subscribe and WhatsApp


BULLETIN # 2 COMMENT YA 30
 
Asante sana mkuu. Hakika maandiko yako hayachoshi. Kama hutojali naomba uwe unani tag.
 
Huku tupo bize kutunga sheria za kudhiti uhuru wa kutumia mitandao ya kijamii na kuifungulia kesi JF, unakuta sizonje anatamani na anasema hadharani natamani malaika watelemke waifungie mitandao ya kijamii, Hivi ni vituko
 
Asante japokua nilishasoma kwenye group lako ambalo watu wanalipia kiingilio Tsh 5000 na unaweka story tatu kwa mwezi mzima na buku tano inaishia hapo na bado vipolo kibao. Ukiambiwa unakua mkali na unakimbilia ku remove watu wanaokweleza ukweli. Plz Jirekebishe.
Cc: Habibu B. Anga.
 
Asante japokua nilishasoma kwenye group lako ambalo watu wanalipia kiingilio Tsh 5000 na unaweka story tatu kwa mwezi mzima na buku tano inaishia hapo na bado vipolo kibao. Ukiambiwa unakua mkali na unakimbilia ku remove watu wanaokweleza ukweli. Plz Jirekebishe.
Cc: Habibu B. Anga.

Duuh!!........Watu mnalipia kuwa member wa group za wasap?
 
Back
Top Bottom