The best.....enzi za form two hizo

Tulikuwa seminary pale moshi tunapelekwa kibosho galz na mapadre kwa debate only nikifika pale mbele nasahau hata na motion ilikuwa inasema nini, siunajua tulikuwa hatuna hata mwalimu mwanamke?

Hahaha.. usinikumbushe Kibosho Girls aisee. Unajua wale wadada walikua na tabia nzuri sana. Mkimaliza debate pale wanaweka viburudisho. Wengine wanacheza music wakiigiza kama wanaume,nakumbuka mmoja alijipaka masizi kidevuni. Last time nakumbuka waliimba music wa Boys II men.
Wengi wao tulikutana Mlimani pale,kuna wengi walikua wakisoma Sheria na mwalimu wao yule pia nilimwona Mlimani,i.e early 2000!
 
Ulikuwa Maua nn!??Maana wale kwa debate hatari kabisa..walitutisha..nakumbuka tulienda tukiwa form 1...na mimi ndo nilikuwa speakeer wa mwisho. aah kwa jinsi walivyokuwa wanainterrupt..nikagoma kuongea!
utasikia;"To open the eyes of the speaker"
au;"To bring the speaker back to the navel of the motion."..afu basi tu kukuintimidate!chairpesron anawaambia;"denied!"
duh the auld lang syn-good old days!!!!!

Hehehe!! Inawezekana enzi hizo na wazee tulikuwemo bado hatujamaliza. Akina John Mnyika ndio O'level,shughuli mtupu!
 
Mnazikumbuka Reverse call lakini????,mimi watu wa posta walishanizoea na hii maneno
 
Best Car- 'Pijo' 504 :D
Best Touser- 'Mchele-mchele'
Best song- TRAPPED- Colonel Abrams

...ngoja nikapekue makabrasha, huenda nikakutana na 'autograph' za miaka hiyo :)
bana eh... nilinunua nchele-nchele kwa khimji aisee wakati niko fomu wani na viatu vya "wet-looking"... Yaani ile picha kila nikiiona nacheka!!
 
hivi hizi ndo zile unapiga wewe afu unayempigia ndo analipa au???

Yap...unapiga home halafu shirika la posta na simu wanamalizana na home masuala ya bill(malipo),ilikuwa inatusaidia sana tukiishiwa,maana hakukuwa na mobile phones wala internet,ni mwendo wa barua tu au kugombana na maopareta wa TPTL kwa hii ishu ya Reverse call
 
Mnazikumbuka Reverse call lakini????,mimi watu wa posta walishanizoea na hii maneno
Mkuu kuna siku kiliniwakia aisee... nimepiga reverse call tena kwa jirani halafu hom hakuna mtu na jirani akanichomolea kwamba hailipii hiyo reverse call

Pale simu arusha nilipaona kama central aisee
 
Mkuu kuna siku kiliniwakia aisee... nimepiga reverse call tena kwa jirani halafu hom hakuna mtu na jirani akanichomolea kwamba hailipii hiyo reverse call

Pale simu arusha nilipaona kama central aisee

The same happened to me mara kibao tu,nilikuwa nagombana sana na maopareta wa TPTL pale Moshi town,maana unakuta una shida(EMO hujaisikia siku nyingi) unamuomba opareta akufanyie utaratibu wa Reverse call home halafu home wazee hawapo,kucheki kwa jirani anatoa nje na kusema halipii hiyo Reverse call.....dah....Asante sana Nguli kwa hii useful thread
 
surely this is a wonderful thread... sijamsoma Geoff sijui vipi leo kwenye hii thread!!

Kuna siku tulikua tunaenda mziki nikatumiwa TMO pale posta arusha aisee ya kama 3,000/- unfortunately walikuwa wanafunga mapema nikafungiwa nje... suruali zenyewe kwa term nzima mbili; mtihani na ufupi wangu nikaazima trousers za mshikaji nilikunja kama pindo tatu hivi... ilikuwa kama zile katuni za masudi kwenye tisheti zake

The good old days, when love was true
gone are those days, when friends were true
i miss those days, when life was true:(

Gone are those days...
 
Bwana wee,mi huwa nikikumbuka my school days nakuwa nahisi kama naangalia movie flani hivi,I wish ningeyarekodi matukio yote niliyoyafanya O-level na A-level

[ame="http://http://www.youtube.com/watch?v=7K_FYtAIBS8&feature=PlayList&p=1344E79C729A7798&playnext=1&playnext_from=PL&index=26"]http://http://www.youtube.com/watch?v=7K_FYtAIBS8&feature=PlayList&p=1344E79C729A7798&playnext=1&playnext_from=PL&index=26[/ame]

[ame="http://http://www.youtube.com/watch?v=H7lNZsvoY8U&feature=PlayList&p=4B73821C55A78FD1&playnext=1&playnext_from=PL&index=3"]http://http://www.youtube.com/watch?v=H7lNZsvoY8U&feature=PlayList&p=4B73821C55A78FD1&playnext=1&playnext_from=PL&index=3[/ame]
 
Nakumbuka nikiwa 4m 2 nilikokota tunda orchad nikala padre akanikama aksema ur smelling something NGULI nikasema YES.... but before all good morning no gud day sir no priest no I mean father, Iam devoted to be priest ...nilichemka nilijua shule imekwisha, nikamwambia satan has tempted me and I have tested the fruit/chungwa .....akaniambia ur a liar...go home and return with the orange enough to feed the whole school....basi kwa vile form one hadi 6 tuko 150 nikaenda after a day nikaja nayo nikasamehewa.

Siku ya concert na kibosho gals a month before naosha raba zangu nyeupe na kutokuzivaa zisichafuke matope ya moshi. Wadada walikuwa wanapenda kuperform wimbo wa one swt day....... na nyimbo za lost boys.....I miss those days.
 
Mkuu unakumbuka enzi za ubabe wa secondary moja huko Rombo ya wavulana tu? jina limenitoka kidogo.....walikuwa wanajiita wagumu.

Heheeeeeeeee,unawazungumzia KILI BOYS nini mazee,hawa jamaa walikuwa na vurugu kimtindo bila kuwasahau Umbwe Dume
 
Heheeeeeeeee,unawazungumzia KILI BOYS nini mazee,hawa jamaa walikuwa na vurugu kimtindo bila kuwasahau Umbwe Dume

Ha ha ha excactly Yes! walikuwa wakija mjini wanafunga mlege mpaka miguuni na mapanki ya kufa mtu na wajamaa walikuwa wachafu.
icon10.gif
 
Heheeeeeeeee,unawazungumzia KILI BOYS nini mazee,hawa jamaa walikuwa na vurugu kimtindo bila kuwasahau Umbwe Dume
hahaaaaa... Kili Boys walikuwa wagumu kimtindo ila waligeuzana wale... na umbwe ni ganja na "piwa" mtindo mmoja
 
HESHIMA MBELE WAKUU,naona hizi zilikuwa za watoto wa boarding au ni mambo ya early 80 ambazo nilikuwa vidudu??
 
ebwanaeeee! lol si mchezo uminifanya nirudi nikikumbuka beck benchaz

hahaha Bek benchaz walikua wanajiona magangwe kuliko wote darasani. Umenikumbusha jamaa mmoja alikua mfupi kuliko wote darasani kwetu ila alikua anapenda sana kuwa miongoni mwa bek benchaz.
 
Wakuu hii hata mimi imenikumbusha those good old days.Nilikuwa Milambo, disco la mchana likiwa T.girls ( Warsaw) wanaume siku nzima inakuwa maandalizi tu.Wale mabitozi tulikuwa hatupandi lori la shule, tulikuwa tunachanga pesa na kukodisha Cab,basi hapo watoto wa warsaw walikuwa wanatuzimia na walikuwa wanatufahamu .Mara nyingi jamaa wa T.boys walikuwa wanatoswa na watoto, basi hapo disco likiisha tu mzee shughuli inakuwa pevu maana jamaa wanaanza vurugu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom