The beginning of the end of the IPTL!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The beginning of the end of the IPTL!?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jul 21, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,641
  Likes Received: 82,289
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]IPTL could lose Sh200bn after liquidation order
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 20 July 2011 22:51
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  By Ramadhan Semtawa
  The Citizen Reporter
  Dar es Salaam. The liquidation of Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ordered by the High Court last week could see the Malaysian firm lose over Sh200bn.The amount is held in an escrow account at the Bank of Tanzania (BoT) and would now be administered under the Registration, Insolvency and Trusteeship Agency (Rita).

  IPTL has had a controversial power generation history since its establishment more than a decade ago, and was sued in 2002 by a local minority shareholder who sought dissolution citing conflict with the Malysian partners.

  Judge Semstocles Kaijage granted the prayers of VIP Engeneering and Marketing Ltd against Mechmar Corporation Berhad and the receiver manager. The development introduces yet another twist that could herald the final operation days of the private firm whose multibillion shillings 100MW power supply contract with Tanesco was dogged by corruption allegations throughout.

  Sources at BoT indicated there was currently a total of Sh207bn in the escrow account. IPTL was receiving Sh3bn in deposits every month, largely in capacity charges.When reached for comment yesterday, central bank Governor Prof Benno Ndulu said he could not issue any information on the matter as they were yet to receive the court orders. He said however the bank would enforce any directives as contained in the judgment.

  The same position was echoed by the Rita chief executive Mr Philip Saliboko as reported in a section of the media yesterday. The official confirmed they have been appointed liquidators and would embark on the job as soon as appropriate. Speaking from Dodoma, Kigoma North MP Mr Zitto Kabwe who is the chairman of the Public Organisations Accounts Committee said the ruling was a welcome relief.

  “That is the beginning and the end of the IPTL story. My committee commends BoT for sticking with a resolution not to spend the escrow accounts money.”The MP challenged Rita to hasten the liquidation process, fearing that the Malysian owners could rush to open an appeal at the International arbitration court.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  End of an era!!!!! sounds good if real!
   
 3. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  IPTL iki-collapse basi itaanika uchafu wa ufisadi wa vigogo including JK ambao watanzania hawatokaa wusahau daima. Hiyo ya Lowassa ama Jairo ni chamtoto. Ngoja tusubiri
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,641
  Likes Received: 82,289
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Serikali yaanza hatua kufilisi kampuni IPTL [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 03 August 2011 23:01 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Fredy Azzah
  Mwananchi

  UAMUZI wa Mahakama Kuu kutaka kufilisiwa kwa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), umeingia katika sura mpya baada ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita), kufungua milango kwa watu wenye madai kwa kampuni hiyo ama pingamizi la kufilisiwa, kuwasilisha taarifa zao kwa wakala huyo.
  Kufilisiwa kwa IPTL kuna kuja kipindi ambacho mkataba wake umetajwa kuwa kitanzi kwa Serikali kwa kuigharimu kiasi cha Sh3 bilioni kila mwezi, huku mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, akitaka mchakato huo uharakishwe.

  Akizungumzia uamuzi huo wa mahakama jijini Dares Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Philip Saliboko alisema tayari wakala huyo ameanza hatua ya awali ya utekelezaji wa hukumu hiyo, kwa kutaka wadai au watu wenye pingamizi kuwasilisha maelezo yao rasmi.

  Tayari Rita jana ilitoa tangazo lake ambalo katika moja ya maelezo yake linasema, "Kwa amri ya mahakama iliyotolewa na mheshimiwa Jaji Kaijega, Julai 15, 2011 katika mahakama Kuu ya Tanzania kwenye shauri namba 254, la mwaka 2003 na shauri namba 49 la mwaka 2002, mpokezi rasmi ameteuliwa kuwa mfilisi wa kampuni tajwa (ITPL) bila ya kamati ya uchunguzi."Akifafanua zaidi kwa njia ya simu Saliboko alisema wakala huyo baada ya kupokea maelezo ya wadai au watu wenye pingamizi itaweza kuingia katika hatua ya pili.

  "Hii ni hatua ya awali, tulikuwa tunasubiri hukumu sasa hivi tumeshaipokea. Tunachosubiri sasa hivi ni kupata malalamiko ya wadai au watu wenye pingamizi," alisema na kuongeza.

  " Maana kuna mtu anaweza kuwa amelala ghafla akasikia kumbe IPTL inafilisiwa loo, naidai au mwingine akasema napinga, hapana hili sikubaliani nalo."

  Alifafanua zaidi, baada ya hatua hiyo ya kwanza kinachofuata ni kutafuta kampuni ya uchunguzi moja au zaidi ya mbili kwa ajili ya kutafuta mali za IPTL.

  Julai 15 mwaka huu, Mahakama Kuu chini ya Jaji Semstocles Kaijage, ilitoa uamuzi huo katika kesi ya madai namba 254 ya mwaka 2003 iliyofunguliwa na Kampuni ya Vip Engeneering and Marketing Ltd dhidi ya IPTL, Mechmar Corporation (Malaysia) Berhad na Mfilisi.

  Katika hukumu hiyo, Jaji alifafanua kwamba kutokana na ombi lililowasilishwa Februari 25, mwaka 2002, na Kampuni ya Vip Engeneering and Marketing ambayo ni mmoja wa washirika wa IPTL na baada ya kupokea maelezo ya mawakili wake kwa njia ya maandishi na ombi hilo kuchapishwa na Gazeti la Serikali Oktoba 10,2003, aliamuru kampuni hiyo ifilisiwe.
  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, hadi sasa hivi fedha zilizomo kwenye akaunti maalumu ya IPTL zilitarajiwa kuwa ni zaidi ya Sh207 bilioni zilizopo kwenye akaunti BoT.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 5. l

  luckman JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ni saa 11.50 nikiwa nyumbani kwangu, nafikiri na kufikiria, nawaza na kuwazua, najiuliza ila sipati jibu sahihi lenye kuridhisha uma wa watanzania na lenye kulete ukweli mwangani toka giza bandia lililotengenezwa na walanguzi wa nchi chini ya kivuli cha uanasiasa, nafikiria wanachi wangu ambao kipato chao ni shs 770,000.00 kwa mwaka, wanaorundikiwa mzigo wa ugumu wa maisha bila hatia yoyote, nchi ya tanzania sio maskini, NAKATAA SIO MASKINI ILIA VIONGOZI NDO WANAOIFANYA IWE MASKINI,
  UTAJIULIZA SHWALI HILI, why Tanzania is a richest country below the ground but poorest country above the ground??

  Ebu fikilia, ni nani alisaini mkataba wa IPTL ambao unaifanya nchi inunue unit moja toka kwao hadi grid ya taifa kwa shs 700.00 hali TANESCO hiyo unit wanaiuza shs 95 na sasa +40.29%, tzs 600.00 zinatoka wapi? hali tanesco inaendeshwa kwa ruzuku na kimsingi ruzuku ni pesa za wanachi yani kodi??? ni nani alisaini huu mkataba na kwa minajili ipi na kwa faida ya nani, Nchi kama mlaji wa mwisho?Tanesco ka shirika? au yeye mwenyewe na boss wake. na je mwanasheria mkuu kipindi hicho alikuwa nani na kasomea wapi, je ana elimu ya sheria kweli? na je wachumi wa nchi wako wapi na walitoa ushauri gani kwenye huu mkataba.
  Suala la ugumu wa maisha na kupanda kwa bei za umeme ni kwa sababu ya hawa watu, tanesco wanaingizwa mkenge kwa kulipa mabilioni ya pesa kwa upumbavu wa watu wachache wenye kuangalia matumbo yao na mwisho mzigo unarudishwa kwa wananchi kama walivyofanya.

  Nakumbuka, rais alikuwa Alhasan Mwinyi
  waziri wa nishati na madini alikuwa Jakaya mrisho Kikwete-ambaye sasa ni rais

  Je wakati wa mchakato wa urais, waliokuwepo hamkumkumbusha huu mradi na ni vipi atawakwamua watanzania katka dimbwi la unyonyaji huku ashawazika kwenye huu mradi wa kinyonyaji?hamkumuuliza na kwa nini hamkufanya hivyo? Mlipata mgao? Usalama wa taifa kazi yao nini siku hizi hali taifa la tanzania si sehemu salama kwa sasa? Ona viongozi wanaotuletea, ona mali za taifa zinaibiwa na wapo, ona watu wanatehwa sumu na wanajua, ona siri za nchi zinavuja.

  Nadhani kuna umuhimu sana wa kuangalia hili suala kisheria, alisaini kabla hajawa rais, lazima huko mbele hili suala liangaliwe.
  IFIKE MUDA TUAMUE KUWEKA UONGOZI THABITI WENYE KUFUATA MISINGI YA UTAWALA BORA NA SHERIA, WENYE +IMPACT KWA WANANCHI WOTE!UGUMU WA MAISHA UTALETA MAJIBU SAHIHI VICHWANI MWA WATANZANIA!

  akhsante sana!
  luckman-yes we created rich
   
 6. l

  luckman JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160

  Ni saa 11.50 nikiwa nyumbani kwangu, nafikiri na kufikiria, nawaza na kuwazua, najiuliza ila sipati jibu sahihi lenye kuridhisha uma wa watanzania na lenye kulete ukweli mwangani toka giza bandia lililotengenezwa na walanguzi wa nchi chini ya kivuli cha uanasiasa, nafikiria wanachi wangu ambao kipato chao ni shs 770,000.00 kwa mwaka, wanaorundikiwa mzigo wa ugumu wa maisha bila hatia yoyote, nchi ya tanzania sio maskini, NAKATAA SIO MASKINI ILIA VIONGOZI NDO WANAOIFANYA IWE MASKINI,
  UTAJIULIZA SHWALI HILI, why Tanzania is a richest country below the ground but poorest country above the ground??

  Ebu fikilia, ni nani alisaini mkataba wa IPTL ambao unaifanya nchi inunue unit moja toka kwao hadi grid ya taifa kwa shs
  700.00 hali TANESCO hiyo unit wanaiuza shs 95 na sasa +40.29%, tzs 600.00 zinatoka wapi? hali tanesco inaendeshwa kwa ruzuku na kimsingi ruzuku ni pesa za wanachi yani kodi??? ni nani alisaini huu mkataba na kwa minajili ipi na kwa faida ya nani, Nchi kama mlaji wa mwisho?Tanesco ka shirika? au yeye mwenyewe na boss wake. na je mwanasheria mkuu kipindi hicho alikuwa nani na kasomea wapi, je ana elimu ya sheria kweli? na je wachumi wa nchi wako wapi na walitoa ushauri gani kwenye huu mkataba.
  Suala la ugumu wa maisha na kupanda kwa bei za umeme ni kwa sababu ya hawa watu, tanesco wanaingizwa mkenge kwa kulipa mabilioni ya pesa kwa upumbavu wa watu wachache wenye kuangalia matumbo yao na mwisho mzigo unarudishwa kwa wananchi kama walivyofanya.

  Nakumbuka, rais alikuwa
  Alhasan Mwinyi
  waziri wa nishati na madini alikuwa
  Jakaya mrisho Kikwete-ambaye sasa ni rais

  Je wakati wa mchakato wa urais, waliokuwepo hamkumkumbusha huu mradi na ni vipi atawakwamua watanzania katka dimbwi la unyonyaji huku ashawazika kwenye huu mradi wa kinyonyaji?hamkumuuliza na kwa nini hamkufanya hivyo? Mlipata mgao? Usalama wa taifa kazi yao nini siku hizi hali taifa la tanzania si sehemu salama kwa sasa? Ona viongozi wanaotuletea, ona mali za taifa zinaibiwa na wapo, ona watu wanatehwa sumu na wanajua, ona siri za nchi zinavuja.

  Nadhani kuna umuhimu sana wa kuangalia hili suala kisheria, alisaini kabla hajawa rais, lazima huko mbele hili suala liangaliwe.

  IFIKE MUDA TUAMUE KUWEKA UONGOZI THABITI WENYE KUFUATA MISINGI YA UTAWALA BORA NA SHERIA, WENYE +IMPACT KWA WANANCHI WOTE!UGUMU WA MAISHA UTALETA MAJIBU SAHIHI VICHWANI MWA WATANZANIA!

  akhsante sana!
  luckman-yes we created rich

   
 7. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kaazi kweli kweli!
   
 8. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Naionea huruma Tanzania
   
Loading...