The beatiful ones are not yet born | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The beatiful ones are not yet born

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BRUCE LEE, Oct 11, 2011.

 1. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  Habari za majukum ndugu zangu wana jamii? Ni muda mrefu umepita bila kujumuika na nyie katika kutoa mada pamoja na kuchangia. Natumia nafasi kutoa maoni yangu kuhusu mtitiriko mzima wa maisha ya watanzania na wafrika kwa ujumla. Kisiasa nimekua najiuliza maswali mengi kwa mfano chama gani au ni mwana siasa yupi mzalendo wa kweli ambae yupo kwa maslahi ya taifa?

  Mtazamo wangu naona vyama vyote kuanzia tawala na upinzani na wanasiasa wao woote wapo kimaslahi binafsi zaidi. Serikali inatumia gharama kubwa kuwalipa mishahara wanasiasa pamoja posho mbalimbali, wanasiasa wanakua matajiri wakati wananchi wao wanazidi kua maskini. Wafrika tupo zaidi ya milioni 400 zaidi ya watu milion 200 wanaishi chini ya dola moja kwa siku yaani wamevuka hata mstari wa umasikini.

  Mashirika mbalimbali ya kimataifa kwa zaidi ya nusu karne yamekua yakitoa misaada mbalimbali pamoja kuchangia bajeti za nchi zetu ila chaajabu umasikini ndio unazidi kuongezeka. Je wapinzani na ccm wanamchango gani? Kuna faida gani yakua na serikali ambazo haziwajibiki ipasavyo?nashindwa kuelewa faida ya rasilimali tulizonazo na sioni mchango wake ktk kuboresha maisha.

  Uchu wa madaraka kugombea vyeo na majungu ndio nacho kwa wanasiasa wetu. Naanza kuamini kua wafrika tumepoteza muelekeo na tunaeleke kupoteza asili na tamaduni zetu. Sioni waandishi mashuhuri kama akina chinua achebe, ngugi, aikwei, elech amad, shabani robert na mwlm nyerere, tunaishi kwa kuiga tamthilia za ulaya na marekani.

  Sioni ukombozi wa kweli nahisi wazuri ktk siasa hawajazaliwa. Wito tuwe makini na tusishabikie vyama bila kutafakari na ku wa asses wanasiasa wa vyama hivyo.

  Asanteni sana
   
 2. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Fikiri kabla ya kuandika, wapo wanasiasa wenye moyo wa kweli wa kuipeleka nchi kule tunapo pataka lakini wewe ni mmoja wa watu msiotaka kuwapa nafasi, fikiria tena tena upya na kwa umakini utagundua kitu.
   
 3. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  Nisaidie wewe ndugu ni wakina nani na wamefanya nini? Tashkuru kwa mchango wake nielimishe mkuu(mbogo)
   
Loading...