THBUB: Tukio la Vijana wa Darajani Zanzibar kupigwa na wanaodaiwa ni Polisi lina taswira ya uvunjifu wa Haki za Binadamu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Screenshot 2025-07-09 094855.jpg

Screenshot 2025-07-09 094907.jpg
TAARIFA ZA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA TUME KUHUSU MALALAMIKO YA KUPIGWA KWA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO LINALODAIWA KUFANYWA NA ASKARI WA MAMLAKA WA MJI MKONGWE ΚΑΤΙΚΑ ENEO LA DARAJANI, WILAYA YA MJINI, MKOA WA MJINI MAGHARIBI, UNGUJA - ZANZIBAR BAINA YA TAREHE 26 NA 27 JUNI, 2025

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni Idara huru ya Serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura 391. Katika kukidhi matakwa ya Kikatiba kwa upande wa Zanzibar, Baraza la Wawakilishi liliridhia Tume kufanya kazi Zanzibar kwa kutunga Sheria Extension Act No. 13 ya mwaka 2003.

Malalamiko ya awali ~ ACT Wazalendo: Tunalaani kutekwa kwa Vijana Wanne Wafanyabiashara Darajani na Askari wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar

Miongoni mwa majukumu ya Tume yaliyoainishwa katika Ibara ya 130 (1) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ni kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu na wajibu wa jamii kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Pia na Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura 391 Kifungu cha 6 (1) (a) ni kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa, kukuzwa na kuhifadhiwa nchini.

Kwa msingi huo, hivi karibuni THBUB ilipata taarifa kupitia vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii pamoja na lalamiko lililowasilishwa Tume na walalamikaji waathirika na tukio hilo, taarifa hizo zimeeleza kwamba wafanyabiashara ndogo ndogo walikamatwa na kupigwa baina ya tarehe 26 na 27 Juni, 2025 na wanaodaiwa kuwa ni askari wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wakishirikiana na askari wa Idara Maalum za SMZ Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

THBUB inaona kuwa tukio hilo lina taswira ya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kutokana na wafanyabiashara hao kulalamika kufanyiwa vitendo ambavyo vinavunja na kudhalilisha utu wao ikiwemo kukamatwa, kupigwa na kuingizwa kwenye pipa la maji machafu, vitendo vilivyowasababishia maumivu makali na majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao.
1111.png

Screenshot 2025-06-28 170235.jpg
THBUB inaendelea kusisitiza juu umuhimu wa kuheshimu na kulinda haki za binadamu nchini, na kuviomba vyombo vinavyohusika na usimamizi wa haki jinai na Mamlaka nyingine zenye mamlaka ya ukamataji kisheria kuzingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora wakati wa utekelezaji wa majukumu yao. Kadhalika, Tume kupitia Tamko hili inawajuilisha wananchi kuwa itafanya uchunguzi wa lalamiko hili kuanzia tarehe 8 Julai, 2025 ili kuweza kubaini ukweli wa tukio hili.

Mwisho, THBUB inawashukuru wanahabari kwa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo kupitia vyombo mbalimbali vya habari na inatoa pole kwa wafanyabiashara hao na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu waweze kupona haraka.

Imetolewa na:
Khatib M. K. Mwinyichande
Kamishna
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
04 JULAI, 2025
 
Vipi kuhusu Waumini wa Gwajima?

Vipi kuhusu Wafuasi wa Chadema waliohudhuria kesi ya Lissu?

Hii Tume ni ya hovyo sana ndo mana TLS wanafanya majukumu yao vizuri kuliko hata wao wanavyoyafanya wakati yapo kikatiba.
 
Back
Top Bottom