GAga yaani unatupa mfano mzuri sana wa jinsi kuwa Panapo Nia pana njia: Ukiamua ndoa yako idumu itadumu. Ubarikiwe sana mpendwa na MUNGU akushibishe kwa mema yote ya nchi.
Hongera sana kwa kudumisha ndoa kwa miaka 17! Nina imani wengine wameshaoa/kuolewa na kuachika mara kadhaa ktk miaka 17. Bid up, Gaga.
Ila endelea kuzikabili changamoto za ndoa na usibweteke na miaka 17 kwani Al Gore na mkewe wameachana mwaka jana baada ya ndoa ya zaidi ya miaka 30. Mwombe Mungu akusaidie muishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha.
On top of that sio vibaya ukitumegea siri ya ndoa yenu kuwa imara
Hongera Gaga, najua kila ulipojitokeza uchungu ulistruggle kurudisha raha.
Mungu akujalie paradiso njema duniani na mwisho wewe na mumeo mumuimbie yeye milele.
Asante kwa ushuhuda na hadithi nzuri kuwa yote yanawezekana.