Mkuu
figganigga, niko hapa, kwanza heri ya mwaka mpya 2013, naamini kwa uwezo wa Mwenye Enzi unaendelea vizuri sana. Huwa napenda sana maswali mchanganyiko kwani humu jamvini ni kisima cha hekima. Dada yangu
gfsonwin naamini pia unaendelea na majukumu ya kuwahudumia mabosi wako, wote watatu.
Nimshukuru Mungu wetu pia kwa mipango ya kufahamiana tarehe 26 kwenye ile kitu yetu (White Party). Nafurahije kukutana na marafiki? kweli niko happy ile mbaya.
Kuhusu jina hili la Thanda wala lisikupe tabu yeyote. Unajua makabila yana majina mengi sana, na kila jina lina maana yake. Kwa mfano utakuta mtu ni mchaga na anaitwa Mboroo. Kwangu mimi hili ni tusi lakini kwa wenzetu ni jina tena la heshima sana.
Tuna rafiki yetu ni Mjapan katika mradi wao wa maendeleo wa JICA, jina lake labda mtu ani-PM ila hapa public hapana.
Kule Zambia tu mwambie mtu akutajie muda. Yaani aseme saa hizi ni saa.........si tu utashangaa ila utajiuliza mara mbili mbili kama ni kweli au anatania. Hata kwetu kuna majina ambayo ni tata sana. Kwa mfano maana ya jina langu ni asali. Sasa utajiuliza kwanini tu wasiniite moja kwa moja Asali.
Kwa kabila la Thanda, maana ya hilo jina ni Love. Sasa unaweza kujiuliza kwanini wasimuite Love kwa kiingereza?. Hilo kwao ni jina la heshima sana. Tena wao ukilikosoa wanakushangaa sana na kuona kama unautukana utamaduni wao.
Neno kaka (brother) nchini Mauritius ni kituko sana. Ukisikika umetamka kaka kila mtu anakushangaa sana. Maana ya kaka ni (mavi makubwa na yanayonuka vibaya).
Kwa hiyo tuwe waelewa kuwa kuna makabila na makabila na kila kabila lina utaratibu wake, utamaduni wake na mila zake.
Kwa maelezo haya machache naamini wapendwa wangu wote mtakuwa mmenielewa,
Arushaone,
Smile Madam B gfsonwin,
Mtambuzi,
watu8 na wengine wote.
Heshima mbele Wakuu.
Mimi nilikuuliza hivi kwanini ulijiita love? sababu siku za nyuma ulikua na id nzuri tu ya kiume na inayo eleweka. Mimi kilicho nishutua ni baada ya kuona umebadili jina la kiume na kujiita jina la kike la upendo ka tyson. mawazo yangu nikawa nafikilia labda mambo ya cameron yameingia jf. hujanijibu isipokuwa umefafanua jina lako.-nakuuliza tena kwanini uliamua kuachana na jina la kiume na kujiita jina la kike?.tunaomba ufafanuzi.cc
Arushaone,
Smile,
Madame B,
Thando,
Mtambuzi,
watu8. mia