Thamani Yangu Mbele za Mungu

Thamani Yangu Mbele za Mungu

Joined
Sep 10, 2018
Posts
7
Reaction score
3
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Yohana 3: 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. 20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. 21 Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

Wafilipi 2: 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. 14 Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano, 15 mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, 16 mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure. 17 Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.

Taka sana kutoka moyoni kuwa mtoto wa Mungu na kutenda matendo mema katika maisha yako ili Mungu wetu mwema ajivunie wewe/mimi kwa shetani kama alivyojivunia mtumishi wake Ayubu.
Mungu hana upendeleo na hajawaji kuwa na upendeleo. Anatupenda wote hachagui wala habagui ila sisi binadamu tunajitenga mbali sana na Mungu.
Sema eeh Yesu Nataka mwanzo mpya katika mwaka huu 2019 ukawe mwaka wa kukujuwa wewe na kutembea na wewe. Naomba unirehemu, unisamehe,unitakase na unigeuze katika Jina la Yesu Kristo Amen.
 
Ujumbe mzuri.
Kuna faida nyingi sana za kua mwana wa Mungu.
Ili somo liwe zuri zaidi ungeorodhesha faida za kuwa mwana wa Mungu.
Na hasara za kutokuwa mwana wa Mungu/kutokukubali kuwa mwana wa Mungu.
Somo lishibe.
 
Back
Top Bottom