Thadei Ole Mushi: Hili la mimba mashuleni tulijitakia wenyewe

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
HILI LA MIMBA MASHULENI TULIJITAKIA WENYEWE.

Na Thadei Ole Mushi.

Benki ya Dunia imetunyima mamilioni ya Shilingi kutokana na kuwazuia wanafunzi wenye Mimba kuwaondoa shuleni.

Naweza kusema tumejitakia wenyewe, Kwa kuwa toka Zamani wanafunzi ambao hupata Mimba mashuleni huwa wanaondolewana na world Bank hawakuwahi kutunyima mikopo. Walikuwa hawatunyimi mikopo kwa kuwa tulikuwa hatujawahi kusimama jukwaani tukatoa kauli kuwa wanafunzi wa kike watakaopata Mimba mashuleni tutawaondoa shuleni.

Balaa limekuja rasmi baada ya Mh Rais kutoa kauli ya kuwaondoa mashuleni wanafunzi wote ambao watapata Mimba mashuleni. Toka siku hiyo jumuiya za Kimataifa zilianza kutoa kauli za kulaani kauli hiyo. Sasa World Bank nao wametoa msimamo wao na watatunyima fedha hizi. Lakino hapo Kabla tulikuwa tukiwaondoa na hatukuwahi kunyooshewa kidole na jumuiya ya kimataifa.

Sasa aidha turasimishe warudi shuleni au tukubali masharti na vigezo ya jumuiya hizi za Kimataifa. Hata Suala la Ushoga kwetu sio utamaduni na Mashoga walikuwa wakilifahamu hilo kitendo cha Kiongozi kulitamka tu tuliona madhara yake imebidi Waziri wa mambo ya Ndani kutoa kauli ya kuwalinda.

TUNAJISAHAU WAKATI MWINGINE

Kabla viongozi wetu hawajatoa kauli wapitie mikataba ya Kimataifa ambayo tumesaini ili isituathiri katika maamuzi.Tanzania imeingia mikataba mingi ya kimataifa ambayo inazungumzia haki ya kila raia kuapata elimu na umuhimu wa elimu hiyo. Hapa nitatoa mifano michache:-

#UN declaration kuhusu Human Rights, tarehe 10/12/1948 nchi 58 zilisaini kuhusu tamko la haki za binadamu. Tanzania nayo ni Miongoni mwa nchi zilizosaini tamko hili baadaye. Kwenye tamko hili lenye Article 30 article ya 26 inazungumzia kuhusu elimu kama haki ya msingi ambayo kila nchi mwanachama anapaswa kuipata.

Kwenye kipengele hicho ambacho kimegawanywa kwenye section tatu kinazungumzia kuwa elimu ya msingi inapaswa kutolewa bure na ile ya vyuo vya elimu ya juu iwe Accessible yaani kila mtu mwenye kuihitaji aipate kwa vigezo vinavyotakiwa (on basis of merit). Haya yanazungumzwa kwenye section ya kwanza ila section ya pili inazungumzia malengo ya elimu yenyewe. Ambapo tamko lile linataka elimu itakayotolewa iwe ni elimu inayoweza kumjenga mtu aweze kuhifadhi na kutunza haki za binadamu wengine, imjenge personality yake awe raia mwema, imjenge mtu awe mvumilivu, mwelewa na aweze kushirikiana na watu wengine ambao wapo tofauti kidini na hata kirangi. Section ya Mwisho inampa uhuru mzazi kuchagua aina ya Elimu ambayo mwanawe ataipata.

#Ukisoma tamko hili utaona kuwa Tanzania kama nchi ilisoma na kuona manufaa makubwa ya Raia wake kupata elimu. Ukimnyima mtu Elimu umemnyima kitu kikubwa sana... ni sawa na kumtoa kwenye ulimwengu huu na kumfungia mahali kwenye Giza. Naamini viongozi wetu hawakushinikizwa kusaini tamko hili walilisaini baada ya kujiridhisha kuwa lina manufaa kwa raia wake.

Hawa mabinti inatupasa tuwadhibiti kwa hali na mali kuhakikisha wanaifaidi haki yao hii ya msingi na kuwafungulia njia. Elimu ni kama Tochi kwao penye giza waitumie kumulika na kusonga mbele. Siungi mkono Mimba mashuleni lakini kwa Maslahi mapana ya Jamii na umuhimu wa Elimu tunapswa kulifikiria hili mbeleni.

#Tamko la pili ambalo nalo tumelisaini ni lile la International Covenant on economic, social and cultural Rights.Tamko hili lilisainiwa tarehe 16/12/1966. Tamko hili likitolewa kupima utekelezaji wa tamko lililotangulia la UN. Tamko hili lilianza kutumika tarehe 31/1/1979 kwenye tamko lile lilikuwa na article 30 ila article ya 14 na 13 ilihusu elimu. Tanzania nayo imesaini tamko hili.

Kwenye tamko hili hakuna kilichobadilishwa toka tamko la mwanzo la UN. Malengo, na manufaa ya elimu yalikuwa yake yale. Na kwa utashi wa viongozi wetu walilisoma na kukubaliana na tamko hilo ndio maana walilisaini kwa niaba ya watanzania.

#Tamko la tatu ambalo Tanzania imeingia ni lile la UNESCO Convention against Discrimination in Education. Tamko hili lilitolewa tarehe 14/12/1960 likaanza kutumika 1962.

Kwenye tamko lile linasema kwenye elimu kusiwepo na Ubaguzi wa aina yoyote ile iwe ni kwa rangi, Jinsia, Lugha, Itikadi za siasa, utofauti wa kiuchumi, nk. Yaani elimu iwe ni kwa watu wote bila kujali makandokando yao.

#Kwa hawa watakaopata Mimba tukiwafukuza moja kwa moja hatuoni kuwa tutakuwa tunakiuka tamko hili tulilosaini wenyewe? Nadhani kama njia sahihi zitafutwa bado kutakuwa na uwanja wa majadiliano namna bora ya kulimaliza tatizo hili.

#Tamko la nne ambalo nalo tumelisaini kama taifa ni lile la Convetion on the elimination of all forms of descrimination against women. Hili ni tamko la mwaka 1979 ambalo lilianza kutumika 1981. Kwenye article ya kumi kwenye tamko lile kuna kipengele kinachohusu elimu. Kwenye article ile yamewekwa masharti kuwa kwa jinsi mwanamme anavyochukuliwa katika kupata elimu basi na kwa wasichana pia kufanyike hivyo hivyo.

#Mvulana anayempa msichana Mimba na huyo mvulana ni mwanafunzi huwa tunamfanya nin? Sijui ila tamko hili pia tumelisaini kwa kuwa tuliamini kuwa mwanamke anapitia mazingira mengi katika kupata elimu yake. Ndio maana nasisitiza umuhimu wa kutafuta njia sahihi ya kutafuta ufumbuzi.

#Tamko la Tano ambalo tumesaini ni lile la UN kuhusu haki za watoto 1989. Ambalo linamtambua mtu ambaye yupo chini ya miaka 18 kama mtoto.

Article ya 28 na 29 kwenye Tamko lile linahusu elimu. Linazungumzia kuwa elimu ya msingi iwe compulsory na iwe free. Wameelezea sana umuhimu wa Elimu kwa mtoto. Na viongozi wetu walisoma na kukubalina na tamko hilo wakasaini badala yetu.

#Tamko la sita ni lile la world conference on Education la mwaka 1990. Hili nalo tumesain ni tamko lilihusu kuondoa ujinga kwa watu wazima.

Mule ndani yamezungumzwa mengi na viongozi wetu walisain badala yetu kwa kuwa waliona umuhimu wa Elimu.

#Tamko la saba ni lile la Dakar Declaration la mwaka 2000. Tamko hili tumekisaini na lilikuwa na lengo la kuufikia 2015 watoto wote wake kwa waume wawe na uwezo wa kumaliza elimu ya msingi.

#Tamko la nane ni lile la Jakarta declaration hili lilikuwa la mwaka 2005. Kwenye tamko hili walitaka nchi zote zilizorudhia na kusaini kutamka kwenye kwenye katiba zao kuwa elimu ni haki ya msingi kwa kila raia.

Tanzania ilisaini na ikaingizwa kwenye katiba yetu. #Changamoto tuliyonayo sasa ni hili kundi tunalotaka kuliacha njiani kundi la wanaopata Mimba wakiwa mashuleni.

#Tamko la tisa ni lile la African Charter lililofanyika Nairobi Kenya 1986. Kwenye ibara ya 17 ya tamko lile lilisema kila Raia ana haki ya kupatiwa Elimu. Viongozi wetu wakalisoma na posho za kuhudhuria wakachukua na wakaona ni sahihi wakasaini.

NATAKA KUSEMA NINI?

Kwanza kabisa viongozi wetu wapitie mikataba na matamko ambayo tumeiridhia kama nchi. Ili tusisigane na jamii za kimataifa ni sharti tukubalianae na Mambo ambayo tulisaini kimataifa.

Pili kuna utamduni mwingi wa Kale katika maisha na Sheria zetu. Kwa pamoja tunapinga suala la Mimba mashuleni lakini hatujawekeza vya kutosha kumlinda mtoto wa kike.

Tatu mazingira yetu sio Rafiki sana kwa watoto wa kike. Niliwahi kufanya utafiti kuhusu shule za Kata wilaya ya Kisarawe, nilikuta kuna wanafunzi wa kike wanatembea hadi km 5 Kwenda shule hivyo wanafunzi hawa walilazimika kupangisha Magetho katika hali kama hii tunawezaje kuweka Sheria kali kama hizi?

Vipi kuhusu wale wanaobakwa? Hawa tunawaweka katika kundi lipi?

Hapa itatubidi kutengua Kauli kama tunazitaka hizi fedha kama tulivyoamua kutengua ya Mashoga.

Bado nchi za Afrika haziwezi kujitawala kutokana na utegemezi wa Kiuchumi. Mambo mengi yatakwama.

Hatuwezi kujiamulia Mambo kirahisi hivyo wakati bado tunategemea Pochi ya mzungu.

Ole Mushi
0712702602
 
Tanzania ni nchi tajiri sana na kwa sasa uchumi wetu unaongoza ktk jumuia ya sadec hatuna sababu ya kutegemea misaada kutoka nje tuna miradi mikubwa inajengwa kwa tsh zetu hakuna hela ya Mzungu.
 
Ni pale unapoaminisha watu kuwa sisi ni matajiri wakati sisi tunategemea misaada asilimia ya %40 ya budget yetu yote, ni pale unaposema una billion tano usd as a country ukaona ni nyingi sana wakati as a country ni ndogo sana, ni pale unapokopa ktk kila ptojects kubwa ila ukawaminisha watu kuwa unalipa cash! Na bado yajayo yanafurahisha zaidi.
 
Madhara ya kukurupuka na kuropokaropoka km vichaa....Mambo Mengine wangemsikilizaga JK na kauli yake tu kua ni "Upepo utapita" Mwanafunzi aliekua anapata Mimba kwanza kabisa 90% walikua wanaacha shule na 10% walikua wakishazaa wanafanya ustaarabu mwingine kwenye private schools sasa unashangaa Kiongozi na mzima anataka kuleta ubabe kwa vi adolescents kwanzaaaa sio vyote vinajua Mimba ata inaingia aje,vingine shida za nyumbani,vingine vinabakwa nk nk Ebu fanyeni sensa kidogo mjue mabinti wanaoingia kidato cha kwanza siku hizi 90% wana Umri wa miaka 12 hadi 13 hawa ni wadogo kiakili wapo ktk Rika la kuujaribu mwili wao kulingana na mabadiriko yanayoanza kuchochea hormone ktk miili yao sio matamanio yao ila ni Nature tu
 
Serikali ya CCM iache ujanjaujanja, Watoto wa Kike wanaopata mimba kuruhusiwa kuendelea na masomo imo katika Ilani yao ya uchaguzi, Serikali itekeleze ilani yake!
 
Hatuwezi pigamagoti kwa mambo ya kipumbavu.
 
Haya washawishi na chadema wenzio muwaruhusu watoto wenu wadungwe mimba alafu warudi shule ili kuliwezesha taifa kupata mkopo huo.
 
Wazungu wakishabanwa maslahi yao huwa hawakosi sababu za kujifichia. Moja ya vitu ninavyompendea JPM ni misimamo isiyoyumbishwa na yoyote yule. Watabana hizo pesa ila mwisho watatoa na hakuna mtu atakayewalamba miguu.
 
Mleta mada (au mwandishi Thadei Mushi) kwa hiyo unataka maadili ya nchi yetu tuyapuuze kisa msaada wa wazungu? Unataka utamaduni wetu uangamie sababu tu tunataka kuwafurahisha makaburu?
Vipi kuhusu hao unaowaita wazungu na mikopo yao, je nchini kwao wasichana wanapata mimba mashuleni?

Zingatia pia kwamba sasa hapa duniani hakuna cha bure, ule si msaada, ni mkopo kama mikopo mingine. Mkopo si kitu cha kukimbilia au kujivunia hata siku moja. Bora wahenga walinena kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi, na akunyimae kunde kakupunguzia mashuzi.
 
sema apone
 
Back
Top Bottom