Thabo Mbeki aongelea ujaji wa Magufuli, ICC na EPA, Msikilize tafadhali!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Huyu ni mmoja kati ya viongozi ninaowakubali hapa Duniani, Thabo Mbeki, tafadhali msikilize kwa makini sana kama ukipenda, anaongelea kujivua gamba kwa CCM na ulazima wa Raisi Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM, ICC na uhusiano wake na Afrika pamoja na EPA (Economic partnership agreement) ambapo anaongelea kwa nini Kenya wameamua kusaini EPA ni kwamba walishinikizwa, sasa kwanini Wazungu wawashinikize kama ni swala la kwa faida ya wote?

Kwa wasiofahamu Thabo Mbeki ndiyo muanzilishi wa Black economic empowerment AK ambapo lengo lake lilikuwa ni kutoa fursa sawa kwa Waafrika huko AK, programu iliyoibua mabilionea kama Toyko Sexwale n.k

Tafadhali chukua muda wako msikilize mpaka mwisho kama ukipenda, kuna mengi sana ya kujifunza ktk kwa Thabo Mbeki!

Unaweza kuanzia dakika ya 3:00 kama ukipenda!
 
Unaweza kuanzia dakika ya 3:00 kama ukindepa!

Thank you.
 
Kwenye suala la Bagbo huyu mbeki sikubaliani nae..... bado ana fikra za mwaka 47.... na njia hii anayo pendekeza inawapa viongozi wetu jeuri ya kuua na kukataa matokeo ya uchaguzi bila sababu....
 
Barbarosa,
Umetuletea video ya maana sana kutusaidia ktk uchambuzi wa mahusiano ya chama tawala na mihimili mingine ya uendeshaji nchi kama mahakama na dola (serikali kuu) kupiga vita rushwa/ufisadi kwa nguvu kubwa bila woga kuwa huyu ni "kigogo" na umuhimu wa kuleta mabadiliko ktk vita dhini ya rushwa.

Suala la vipi nchi zinaimba wimbo wa nchi kuwa za viwanda lakini nchi za kiafrika zinashindwa kufiki tamanio hilo pia kwa miaka, miongo yote hiyo.
 
Rushwa kwenye chama tawala,ameifafanua kidogo ,kama mnafatilia mambo ya dunia huyo aliyekuwa mkuu wa security ya chama na state baada ya kustaafu amefungwa maisha.Mke wake ameukumiwa Mei kutumikia kifungo cha miaka 10,mtoto wao amehukumiwa miaka 12 jela.wanatakiwa kulipa faini ya mabilioni ya yen.kwa Tanzania ni untochables
 
Wewe jamaa mbona unakuwa mjinga hivyo

kwa nini unadanganya wazi

ni dakika ya ngapi amemtaja huyo bwana wako?
 
Wewe jamaa mbona unakuwa mjinga hivyo

kwa nini unadanganya wazi ni dakika ya ngapi amemtaja huyo bwana wako?

Si lazima amtaje ila kama umesikiliza kwa makini utakuwa umeelewa nini anamaanisha kwa nchi zetu za afrika na ulimwenguni kwa ujumla. Chama tawala watu wake wengi wanakuwa wala Rushwa lakini ni vigumu serikali kuwachukulia hatua na ndiyo msingi mkubwa ulioongelewa wakati wamealikwa kule China.
Kuhusu EPA, amesema baadhi ya nchi zilishinikizwa kusaini, akatolea mfano ni Kenya japokuwa hakuhitaja Tanzania kwa kuto kusaini EPA. Sasa hapa wazungu wansema Connect the dots utaelewa
 
Hakutaja Tanzania kwa sababu alikuwa anaongelea awamu ya kwanza ya EPA ambapo nchi zote za AM pmj na Kenya yenyewe waligoma kusaini ndiyo EU wakawaambia Kenya kama hamsaini basi tunaongeza kodi kwenye bidhaa zenu mnazouza EU kama Maua na hapa ndipo Kenya wakashinikizwa kusaini, hiyo ilikuwa ni hatua ya kwanza na Kenya walifanikiwa pia kuwashawishi nchi nyingine za AM ikiwemo yetu wkt wa Kikwete kusaini hivyo AM kama Jumuiya ilishasaini makubaliano ya mwanzoni, ila sasa hivi ndiyo hatua ya mwisho ya kusaini hayo makubaliano ndipo Tanzania yetu chini ya Uongozi mpya imegoma kusaini na ndiyo maana Wakenya wanahaha na wanashindwa kuelewa kwa maana mwanzoni waliweza kuwashawishi nchi zote kusaini lkn sasa hivi TZ imegoma, na mimi binafsi naungana na Serikali ya Tanzania kwenye hili!
 
Rushwa kwenye chama tawala,ameifafanua kidogo ,kama mnafatilia mambo ya dunia huyo aliyekuwa mkuu wa security ya chama na state baada ya kustaafu amefungwa maisha.Mke wake ameukumiwa Mei kutumikia kifungo cha miaka 10,mtoto wao amehukumiwa miaka 12 jela.wanatakiwa kulipa faini ya mabilioni ya yen.kwa Tanzania ni untochables
Hawa ni wachina. Sema mamilioni ya Yuan na siyi Yen.
 
Back
Top Bottom