jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Wanajamvi,
Kuna habari zimekuwepo kuhusu nchi za EU kuanza kutoa misaada mara baada ya nchi hizo kusimamisha misaada hiyo kwasababu ya ukosekanaji wa demokrasia nchini. Lakini kuna makala moja nimekutana nayo ambapo inaonyesha Mh. Rais ameshaanza kubadili msimamo kuhusiana na mkataba huo wa ushirikiano wa kibiashara na mataifa ya Ulaya, ama “Economic Partnership Agreement”(EPA). Mkataba ambao mwanzoni rais alisema ni wa kinyonyaji na kikoloni. Na ukapingwa vikali hadi bungeni.
Mkataba huu ulipoletwa mwanzoni, Magufuli aliuita kuwa ni “mkataba wa kikoloni”, kwasababu unaenda tofauti na malengo ya serikali yake ya viwanda. Na bunge lilifuatia kwa kuupigia kura ya “Hapana”. Point yao ikiwa ni kwamba hatuwaweza kufanikisha sera ya viwanda kwasababu hatuwezi kushindana nao, na pia tunategemea kodi za mapato kutokana na bidhaa zinazoingizwa kutoka kwenye mataifa hayo.
Rais Magufuli aliuponda sana mkataba huo mbele ya rais Museveni wa Uganda. Mkataba huo ni wa kuondoa ushuru kwenye bidhaa baina ya mataifa hayo ya Africa na Europe.
Hadi kufikia mwaka jana, Rwanda na Kenya tayari walikwisha usaini mkataba huo. Mkataba huu ulitakiwa usainiwe na mataifa yote ya EAC. Baadhi walisaini na baadhi hawakusaini tukiwemo sisi, Uganda na Burundi.
Kwenye makala hii, mwandishi anaonesha kuwepo na uhusiano kati ya serikali kuonyesha dalili za kubadili msimamo kwenye mkataba be serikali kunyimwa msaada na mataifa hayo kwa kukandamiza demokrasia.
Sasa nilikuwa nikijiuliza ni kipi kimefanyika wakabadili mawazo? Ndipo nikakutana na hii.
Kwa kifupi, mwandishi anaonyesha uwezekano wa “quid pro quo”, yani mkataba unasainiwa na vikwazo vinaondolewa bila kujali kama sababu zilizofanya vikwazo hivyo vikawekwa zimekwisha kufanyiwa kazi!
Je, hapa tunajifunza nini? Je, kuna kingine ambacho Magufuli akiwapa basi watafumbia macho yote waliyokuwa wakiyakodolea mimacho hapo mwanzoni? Mfano uminywaji wa demokrasia?

The European Commission is close to invoking Article 96 of the Cotonou Agreement and cutting off all financial support and political relations with the Tanzania government, EURACTIV understands. The EU’s ambassador Roeland Van de Geer was expelled from Tanzania in November after raising concerns about democratic freedoms and human rights.
‘He (Magufuli) has managed to completely destroy relations between the EU and Tanzania. The mood upstairs [in the Commission] is very ugly,’ one Brussels official told EURACTIV.
Several EU countries, including Denmark, Sweden and Belgium, have already cancelled bilateral aid programmes worth around €50 million, but invoking Article 96 would strike down the €100 million the Commission gives Tanzania in budgetary support each year.
In signs of a new rapprochement in recent weeks, Magufuli’s office released photographs in early February of the Tanzanian president meeting with Van de Geer’s successor, Charles Stuart.
But Brussels is still waiting for substantive negotiations on the EPA to re-start. There are also few signs that Tanzania is opening up its trade policy. At the Trade Policy Review of the East African Community on 20 March, the EU noted that Tanzania and Burundi had failed to ratify the WTO Agreement on Trade Facilitation.
EU waits for Tanzania to back up change of heart on stalled trade deal
An Economic Partnership Agreement (EPA) between the EU and six East African countries has been stuck for several years. When President John Magufuli’s Tanzanian government suddenly announced it was reviewing its position on the EPA with a view to endorsing it, EU officials were taken aback.
www.euractiv.com