TGNP walaumu millioni 50 za Magufuli kuwa mkopo kwa vijiji

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
maggg.jpg


Wanaharakati wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameikosoa bajeti ya mwaka 2016/17 kutokana na kuzifanya Sh50 milioni zilizoahidiwa na Rais John Magufuli kwa kila kijiji, kuwa za mkopo badala ya kutolewa kama ruzuku.

Katika tamko lao, wanaharakati hao walisema Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato ili iweze kutoa ruzuku kwa vikundi vya wanawake kwani walio wengi tayari wana mikopo wliyopewa na taasisi za fedha na hivyo wana mzigo wa madeni.

Akisoma tamko hilo, Janeth Mawinza alisema wanawake wana madeni mengi ambayo wameshindwa kulipa kwa sababu ya kukosa elimu ya kufanya biashara.

“Tuwape unafuu sasa kwa kuwapa ruzuku, vinginevyo tutawasababishia msongo wa mawazo kwa kudaiwa na taasisi mbalimbali za fedha,” alisema.

Alisema mpango huo wa mikopo bila kuwapa elimu ya biashara unaweza kusababisha vifo kwa baadhi yao.

“Tumeshuhudia wanawake wananyang’anywa samani zao na kusababisha msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa elimu ya biashara, tutawaua,” alisema.
 
Wanaharakati wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameikosoa bajeti ya mwaka 2016/17 kutokana na kuzifanya Sh50 milioni zilizoahidiwa na Rais John Magufuli kwa kila kijiji, kuwa za mkopo badala ya kutolewa kama ruzuku.

Katika tamko lao, wanaharakati hao walisema Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato ili iweze kutoa ruzuku kwa vikundi vya wanawake kwani walio wengi tayari wana mikopo wliyopewa na taasisi za fedha na hivyo wana mzigo wa madeni.

Hawa TNGP ni kituko.Kwa hiyo walitaka hizo pesa serikali iwape wakalipie madeni wanayodaiwa?
Kukopesha vijiji kunasaidia mzunguko wa hela kuwafikia watu wengi zaidi.Mfano kijiji kikikopeshwa kikanunua trekta na kuanza kulikodisha kwa wakulima pesa za mkopo zikarudishwa zaweza tena kopeshwa kwa shughuli ingine.

Hata ukiwa na ndugu akikuomba hela ya mradi anaotaka kuanzisha usimpe bure mkopeshe ndipo atachacharika ukimpa bure atazira sababu humfuatilii.Mkopo una ufuatiliaji wa karibu
 
Hivi milioni 50 inasaidia nini kwenye kijiji chenye watu zaidi ya 1000? Barabara? Kujenga hospital? Kununua madawati?
 
Hivi milioni 50 inasaidia nini kwenye kijiji chenye watu zaidi ya 1000? Barabara? Kujenga hospital? Kununua madawati?

Hizo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kijiji.Ni kwa ajili ya mitradi ya kuingiza pesa ya kijiji.Waweza fungua duka la kijiji au kununua mashine ya kusaga na kukoboa nk ili kijiji kipate pesa.
Wakifungua duka watu 1000 ni soko kubwa
 
Uwape watu ruzuku wakanywee Chibuku hao TGNP wajitathmini hawajui Pesa ya dezo haina uchungu, ukijua ni mkopo utafanya la maana.
 
TNGP wanaishi mjini kwa mfumo wa kibakuli na wanachokifanya ni kupigania mfumo huo wa kibakuli uwe kwa nchi nzima. Ifike mahali Watanzania tutambue madhara ya kuishi kwa kudeka. Tough love is what we need.
 
Amakweli watanzania alie tuloga alisha kufa aiseeee.....
Ilipo toka ahadi, tulipinga kwamba haitawezekana 50 milioni kwa kila kijijini.
Leo imethibitika kupatikana hiyo 50 milioni kwa kila kijiji, tumekuja na maneno mapya kwamba oohhh hazitoshi....mara ohhhh zitakua mizigo kwakua wamama/ vikundi wana madeni kwenye taasisi za kifedha.
SASA SIJUI WATANZANIA TUNATAKA NINI aiseeee
 
Katika hili nafiiri nitofautiane na TGNP.
Kwanza kama pesa hizi zikifika kweli kwenye vijiji na zikawekewa usimamizi na ufuatiliaji mzuri zinaweza kusaidia. Milioni 50 zinatosha kabisa kwa kuanzia kulingana na hali ya serikali yetu na changamoto za nchi yetu

Nashauri hapo ianzishwe miradi ya VSLA(Village Savings and Loan Association). Pesa hizo zitakopeshwa kwa labda tuseme kina mama kisha wanarudisha ili kuwe na sustainability (Uendelevu). Pesa hizo zinakuwa hazirudishwi serikalini bali zinakuwa zinarudishwa katika acc ya mradi.
Kunakuwa na awamu za kukopa mfano mtu akishakopa labda mara tatu anagraduate kwa kutokukopa tena kwa labda miaka miwili.

Tukisema pesa hizi wapewe bure ni upuuzi, kwani hazitawasaidia lolote na zitaleta uhasama mkubwa vijijini.

Serikali ipeleke wataalamu wa kufundisha vikundi jinsi ya kung'amua fursa zilizopo kijiji husika na jinsi ya kuzifanya kwa tija.
 
Hivi hawa wanaanza wapi kutetea bajeti badala ya haki za wanawake. Haya ndo moja ya Mashirika ya kufutwa kwa kufanya siasa.

Kama watetezi mbona kuna matatizo sana na hatujawahi ona wanatoa hata msaada? Kuna hospitali, njaa na matizo kibao hawasemi ila siasa.
 
Watu walipiga kura nyingi ccm kwa sababu ya ml 50 ambazo waliambiwa ni bure. Kwa sababu hiyo wazilete ziwe mkopo au vp tutazipokea maana baba hawezi kutufunga atasamehe tu.
 
Mwanzoni mlidai hilo la mil 50 kwa kila Kijiji haliwezekani, jamaa wametekeleza Leo mnasema hazitoshi!! Tz ni shida!
Yaani shida si kidogo yaani hilo tu la kuwezekana ni big up. Ilionekana kama ni ndoto lakini inatimia ndani ya mwaka mmoja ( chini ya mwaka) kwa kweli Mh. magufuli heshima yako!
 
Back
Top Bottom