TGIF: Cheka nami.. this is funny (Kutoka Dodoma)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Niko katika harakati za kulobby kamati fulani ya Bunge ili waweze kulidaka hili la Usalama wa Taifa na wakuu wa upepelezi n.k ili wajue wao walijua nini kuhusu wizi wa mabilioni, na walijua nini, na walifanya nini.

Mwenyekiti wa mojawapo ya hizo kamati baada ya kupokea Simu na kusabahiana akaniuliza;

"Nani mwenzangu bwana"

"Mwanakijijiji hapa, nazungumza toka Marekani Mheshimiwa" Nilisema kwa heshima zote na taadhima.

"Duh Mwanakijiji, wewe tunayekusoma huku?" Akaniuliza huku akiangua kicheko kidogo..

"Naam mzee, poleni na shughuli na kazi ya kulitumikisha Taifa letu (niliponyoka ulimi)" Nikamuambia huku nikifiria nilichokisemwa 'kwa bahati mbaya'

"Sasa Mwanakijiji nikusaidie nini? au nina kakashfa gani bwana, msijekuniandika nina "vijisenti"" Akasema huku akiuliza kama ananitega na akaangusha kicheko.

Nilishindwa kujizia na mimi nikaangusha kicheko.... mazungumzo yakaendelea.

I hope you laughed too...
 
yakaendeleaje?au ulinyamazishwa kama kina livingston luhere?just joking but tell us maana umeamua kutuambia sasa yanini usimalizie?
 
Mheshimiwa bila shaka kale ka mradi ka pembeni kenye sura ya ufisadi fisadi kamekwishagundulika.
Hawa watu usidhani ni bure. Si ajabu kweli alistuka kweli!

hapo ungemstua zaidi kwa kumwambia, 'ndio mzee, ndio sababu nimekutafuta nikutahadharishe mapema.' Simu ingezimwa haraka sana.
 
No asingezima simu ila angeanza kusema.

"Eheee unajua kijana ehee inabidi tuongee hii issue ni serious maana nyie vijana wa jambo forums hamna dogo. Mimi vijisenti vyangu ni kidogo sana lakini nafikiri tutagawana kidogo"

Then he would wait for your response
 
it wasn't funny after that...

It was funny coz najua ulimwambia nini huyo muheshimiwa ilikuwa kama hivi

"Nani mwenzangu bwana"

"Mwanakijijiji hapa, nazungumza toka Marekani Mheshimiwa" Nilisema kwa heshima zote na taadhima.

"Duh Mwanakijiji, wewe tunayekusoma huku?" Akaniuliza huku akiangua kicheko kidogo..

"Naam mzee, poleni na shughuli na kazi ya kulitumikisha Taifa letu (niliponyoka ulimi)" Nikamuambia huku nikifiria nilichokisemwa 'kwa bahati mbaya'

"Sasa Mwanakijiji nikusaidie nini? au nina kakashfa gani bwana, msijekuniandika nina "vijisenti"" Akasema huku akiuliza kama ananitega na akaangusha kicheko.

Nilishindwa kujizia na mimi nikaangusha kicheko.... mazungumzo yakaendelea...

"enhe Mwanakijiji ulikuwa unasemaje?"

"Mheshimiwa nimeamua nitupe jembe namimi nije mjini nitafute uongozi"

"Kwanini Mwanakijiji na sie tunawategemea nyie mlime sie tule suti zinatubana kwa ajili ya kilimo chenu"

Kicheko

"Sasa mhe kama 1 million dollar ni vijisenti yanini nishike jembe si bora na mie nije huko mjini nitafute uongozi?"

Kicheko mpaka mheshimiwa akashikwa na vichomi pumu na pressure juu.

Hivi ndivyo yalivyokuwa mazungumzo ya Mzee Mwanakijiji na Mwenyekiti wa mojawapo ya hizo kamati.
 
Back
Top Bottom