SI KWELI TFF yavunja bodi ya ligi na kuteua bodi ya mpito

SI KWELI TFF yavunja bodi ya ligi na kuteua bodi ya mpito

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
photo_2025-06-06_09-18-35.jpg
 
Tunachokijua
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ni chombo kilichoundwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ridhaa ya mkutano mkuu wake uliofanyika tarehe 24 hadi 25 Machi, 2012. Bodi hii imepewa mamlaka ya kuendesha na kusimamia Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, na Ligi Daraja la Pili chini ya Ibara ya 55 ya Katiba ya TFF.

Machi 08, 2025 ni Siku ambayo bodi ya ligi iliuhairisha mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, baada ya Simba kutoa taarifa ya kutoshiriki mchezo huo kutokana na walivyoviita vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya timu yao kwa kunyimwa haki ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamini Mkapa kinyume na kanuni.

Baadaye klabu ya Yanga ilitoa taarifa iliyoweka bayana msimamo wao juu ya tukio hilo, ikiwemo kutoshiriki mchezo namba 184 kwa tarehe yoyote itakayopangwa, kudai haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi, vilevile ilionesha kutokuwa na imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo, hivyo kuliomba Shirikisho la Mpira wa miguu - TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wengine.

Taarifa inayosambazwa mtandaoni

Kutokana na mwenendo huo, ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni kuwa TFF imeivunja bodi ya ligi na kuteua bodi ya mpito ikielezwa kuwa ni kutokana na kushindwa kutafsiri vyema kanuni katika kuhairisha mchezo kati ya Simba na Yanga Machi 08, 2025.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani TFF haijavunja bodi ya ligi, bali taarifa hiyo imetengenezwa na wapotoshaji. Kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) imebainika kuwa haikuchapishwa katika kurasa rasmi za TFF.

Barua yenye taarifa hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanayoitofautisha dhidi ya barua rasmi ambazo hutolewa na TFF. Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na matumizi ya mwandiko (Fonti) ambao hautumiwi na shirikisho hilo katika barua zake.

Hata hivyo TFF kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii imeikanusha taarifa hiyo na kwamba haina ukweli wowote.

Kwa mujibu wa tovuti ya bodi ya ligi inaonesha kamati ya uongozi. rejea hapa.
screenshot_20250604_113408-jpg.3355554
Back
Top Bottom