Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 918
- 1,994
Salaam watu wa soka,
Za masiku?
Naendelea kuwapatia taarifa muhimu kuhusu timu yetu ya Singida Big Stars na leo taarifa kubwa ni kuhusu uamuzi wa TFF kutufutia adhabu ya kutosajili dirisha dogo mwezi Desemba kama walivyotangaza awali.
Uamuzi wa TFF ulitokana na shauri lililowahi kupelekwa na Polisi Tanzania kwa kile walichodai tulimsajili mchezaji wao, Metacha B. Mnata, akiwa bado na mkataba nao, jambo ambalo tulikuja kulimaliza kwa makubaliano ya pande zote mbili japo kwa bahati mbaya shauri lililofikishwa TFF lilikuwa bado halijafanyiwa kazi hivyo kuja kuamuliwa tukiwa tayari tushamaliza mgogoro na Polisi Tanzania.
Kwa umakini mkubwa, Wakili wetu pamoja na jopo la wanasheria wetu walilazimika kuomba review (mapitio) ya adhabu ya TFF na hatimaye kupata nafasi ya kwenda kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji na kuwasilisha hoja nzito za utetezi zilizopelekea kutenguliwa kwa adhabu hii.
Niwahakikishie mashabiki wetu, Benchi la Ufundi la Singida Big Stars limeandaa ripoti maalum inayoainisha maeneo au safu ambazo tutaenda kuziboresha kwa kuzifanyia usajili makini punde tu dirisha dogo litakapofunguliwa mwezi Desemba.
Tunaishukuru TFF na Bodi ya Ligi kwa kusikiliza shauri hili na kutupatia haki yetu. Bodi na Menejimenti ya Singida Big Stars itaendelea kufanya kazi kwa weledi zaidi na kuhakikisha tunaleta ushindani wa kweli ili kuongeza ubora wa Ligi yetu.
Taarifa si inatosha?