TFF na Bodi ya ligi Tanzania huwa hamuoni aibu marefa wa nchi nyingine kuitwa kwenda kuchezesha michuano ya kimataifa?

NALIA NGWENA sidharau marefali wetu lakini napatwa na ukakasi sana MTU anapotamka kuwa "ligi yetu ni ya Tano kwa ubora Africa''

Angalia Kenya na Uganda ligi zao zinatoa marefa kwenda kuchezesha michuano ya kimataifa lakini ukija Tanzania hata michezo ya ndondo hakuna refa aliyeitwa kwenda kuchezesha.

TFF na Bodi ya ligi ifikie hatua ione aibu Sasa na itengeneze mfumo mzuri na mfumo endelevu utakao kuwa unazalisha marefa wenye uweledi katika utendaji wa kazi.

TFF na Bodi ya ligi jifunzeni/igeni kutoka kwenye nchi jirani wanafanyaje fanyaje mpaka marefa wao wanakua Bora kuliko wa kwetu mpaka wanaitwa kwenye michuano ya kimataifa.

Mbona vitu vingine tunaiga Kama kuwafundisha ball boys kuchelewesha mipira na kurusha mipira miwili uwanjani kama tulivyofanya kwenye mchezo wa Taifa stars dhidi ya Niger.

Kuna uwezekano mkubwa hao wanaotuambia ligi yetu ni ya Tano kwa ubora Africa ni wanatukejeli tu maana huwezi kuwezi kuwa na ligi Bora halafu marefa wako hawatambuliki.
Nadhani lugha za mawasiliano ni ziro kwa Marefa wa Tz....na uwezo mdogo
 
Back
Top Bottom