TFF mna nia nzuri mnakosa sera

Mbegu Jr

Senior Member
Sep 23, 2020
137
160
Tff ndie mdau wa kwanza wa mpira nchini kwetu hamna sera yeyote ile hata kutueleza nia yenu siku moja hatujawahi kusikia kuhusu sehemu za kuchezea yaani pitch. Inasikitisha kwakweli kwa taasisi kubwa kama hii inashindwa hata kutoa maelekezo kwa klabu na wamiliki wa viwanja wanunue mbegu za nyasi kwa ajili ya viwanja vyao.

Huu utani tunao uona timu zetu zikiwa zinacheza ni aibu kubwa na kibaya zaidi ligi yetu inazidi kupata mileage kila uchwao
Nyasi zilizopo sidhani ni maalum kwa ajili ya mpira leveling ni kama ilifanywa na greda kila siku timu zinalalamikia viwanja vibovu wakati huo mmetulia tu ofisini kusubiri kiwanja cha kukifungia baada ya Gwambina.

Mnapaswa kuwa wabunifu kwenye suala hilo Kama mifuko yenu haitoshi kununua mbegu bora pamoja na kuajiri watu wa kutunza ombeni msaada watu wanapenda mpira sana lakini uangalia mpira siku moja huwezi kuja tena mvuto wote wa mpira unakosekana
Mmefanya vizuri kwa uwanja wa Mkapa lakini viwanja kama.

Majaliwa=lindi
Namfua =singida
Sokoine=Mbeya
Ushirika=Kilimanjaro
Ccm Kirumba
Majimaji =Ruvuma

Na vingine vingi ambavyo sijavitaja ninyi ndio wanufaika wakubwa wa hivyo viwanja ligi yenu ndimo inapofanyika. Wanunulieni Bermuda seeds kila uwanja angalau kilo 20 au mbegu zingine zilizo bora, muwasaidie kuweka level sawa ya sehemu ya kuchezea wao mbegu zipandwe wao wabaki na kazi ya kuzimwagilia ambayo klabu nyingi zitaiweza.

Itasaidia kuongeza mapato kutokana na wafuatiliaji wa uwanjani. Viwango vya wachezaji vitakuwa vya uhakika
Hapo ndipo mageuzi ya soka yanapoanzia
Hapo ndipo thamani ya ligi ilipo
Hapo ndipo ilipo burudani


Samahani kwa mwandiko mbaya
 
Wazo zuri aisee,
Hivi gharama za kutengeneza pitch quality ya Benjamin Mkapa ni sh ngapi?

Nataka ni chungulie fursa
 
Back
Top Bottom