Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
TFF ni dhaifu kwa kutumia kanuni ambazo zinaruhusu kutengua matokeo ya mpira jambo ambalo ni kudhoofisha mpira wa miguu.
Endapo TFF wangekuwa waadilifu kanuni zao zingeipatia TFF mamlaka ya kutangaza ni mechi zipi mchezaji mwenye adhabu hapaswi kucheza na timu zote kulijua hilo ikiwemo marefa na kuweka utaratibu wa rufani kupinga maamuzi kabla mechi haijachezwa. Utaratibu huu uliopo ulipaswa urekebishwe na timu zote husika ziwajibike kuhakikisha maelekezo ya TFF yanatekelezwa kabla na wala siyo baada ya mechi.
Baada ya mechi, kanuni zitamke wazi maamuzi ya refa ni ya mwisho hakuna ushindi kuusaka mezani.
Na taarifa zote za mechi za TPL ziwemo kwenye TOVUTI ya TFF kuleta uwazi na uwajibikaji.
Timu wahanga wadai haki kwa refa kabla na siyo baada ya mechi kwani matokeo kutobadilika baada ya mechi.
Haiwezekani Kagera Sugar F.C waifunge Simba khalafu kwa sababu zozote zile matokeo yachakachuliwe na kamati mezani.
Timu itakayochezesha wachezaji au mchezaji aliyefungiwa kucheza mechi husika timu hiyo kunyang'anywa pointi tatu za musimu ujao bila kuathiri matokeo ya mechi iliyochezwa.
Hivi kwa kanuni zilizopo kama Simba ingeliwashinda Kagera Stars huku mathalani walichezesha mchezaji batili adhabu yao ingelikuwa ni nini?
Tuache kushusha mpira kwa kujiwekea kanuni zinazoruhusu siasa badala ya mpira kuamua maendeleo ya soka nchini
Manara kauli zake za vitisho au ushawishi wakati rufaa bado hazijaamuliwa ni kuingilia uhuru wa vyombo vya kutoa haki na hilo hakuna ubishi ni kosa ambalo ni la utovu wa nidhamu.
Manara ni lazima TFF imchukulie hatua vinginevyo TFF ndiyo inavuruga soka nchini.
Haiwezekani Kiongozi wa Simba anahoji maamuzi ambayo hayajafanyika na kukosoa uongozi wa TFF nje ya utaratibu khalafu TFF ikanywea! Hii ni kashfa sasa.
Kama TFF wanajiona hawaijui kazi yao au wamechoka au hawaitaki wachukue hatua ya kubwaga manyanga.
WAKATI NI HUU: NYOENI AU SUKENI enough is simply enough!