TFF: Hatutambui mabadiliko ya uongozi Coastal Union

TFF: Hatutambui mabadiliko ya uongozi Coastal Union

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
[h=1]SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya klabu ya Coastal Union ya Tanga yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni.[/h][h=1]Kwa mujibu wa TFF, uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao wanautambua na wataendelea kufanya nao kazi, na sio kiongozi mwingine yoyote.[/h][h=1]"Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu," alisema Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura.[/h][h=1]Alisema tayari wamepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake.[/h][h=1]"Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi," alisema.[/h]

Chanzo: Majira
 
Back
Top Bottom