TFF haikutenda haki kwa Yanga

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,754
WIKI iliyopita kulikuwa na msuguano baina ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na klabu za Yanga na Simba.

Msuguano huo ulitokana baada ya mechi ya Yanga na African Lyon kuonyeshwa kwenye runinga.

Kana kwamba haitoshi nusura mechi ya Simba na Majimaji nayo ioneshwe, kama si uongozi wa Simba kuwa ngangari basi nayo ingeoneshwa ‘live’ kama ilivyokuwa kwa wenzao Yanga.

Uongozi wa Yanga ukalalama kwamba TFF imefikia makubaliano ya kuonesha mechi hiyo bila ridhaa yao na siku chache TFF ikakiri kufanya hivyo na kuahidi kwamba halitajirudia.

Sasa Yanga inadai fidia, lakini kuna habari za kusikitisha kidogo kutoka TFF kwamba hilo halitafanyika.

Haikatazwi kuonesha mechi za Ligi ‘live’ kwenye vituo mbalimbali vya runinga nchini, lakini kwanini hilo lifanywe na TFF pekee?

Hakuna asiyejua masharti ya kuonesha mechi live, ni kwamba lazima pande zote tatu kwa maana ya chama husika, klabu na kituo zikubaliane na kufikia muafaka.

Hilo ni lazima lifanyike kwa vile kuna malipo yanafanywa, TFF ilikubaliana na nani kuonesha mechi hizo, na kama kuna malipo yametoka yameenda wapi?

Kwa ninavyoona, TFF haikustahili kufanya hivyo na hata kama hakuna malipo labda, nani ataamini wakati kila kitu ilifanya yenyewe bila kuzishirikisha klabu?

Kuna hasara ambazo klabu inapata pale mechi zinapooneshwa ‘live’ kwenye runinga, na TFF inalifahamu hili lakini sijui kwanini ilichukua uamuzi huo.

Mechi inapooneshwa live ina maana kuna mashabiki wengine wa soka hawatoingia uwanjani na badala yake watakaa majumbani mwao kutazama mechi kwenye runinga, kwanini klabu zisije juu kama kuna kitu kama hicho halafu hawaoni malipo?

TFF inatambua kwamba klabu zote za Ligi kuu zinajiendesha kwa mapato yake ya viingilio milangoni, sasa inapoamua mechi ioneshwe kwenye runinga bila klabu kupata senti yoyote inategemea nini?

Hilo ni kosa TFF imefanya ambalo nadhani ni busara lisirudiwe ili kuondoa dhana potofu dhidi ya shirikisho hilo kutoka kwa wadau wa soka.

Ni vema wakati mwingine kunapokuwa na kitu kama hicho klabu husika ziwekwe wazi, mbona katika mechi nyingine hufanya hivyo, safari hii kimeshindikana nini?

Shirikisho hilo linatakiwa kujua kwamba ndio msimamizi mkuu wa soka nchini, haipendezi likifanya mambo yasiyo na kichwa wala mguu ambayo mwisho wa siku yanazua maswali mengi kwa wananchi na wadau wa soka kwa ujumla.

Source: Gazeti la Habari Leo

My Take

Hivi inawezekanaje ITV kuonesha mechi moja kwa moja(live) bila ridhaa ya TFF na Yanga???,inakuwaje TFF wanalikalia kimya hili na kuipiga mkwara Yanga kwa kudai fidia ya 70 mil??..Ni kwa nini linapokuja sualala hela(hasa mgawo wa mapato) kwa klabu TFF wanakuwa si waaminifu???,TFF mbadilike katika hili,pia ITV inakuwaje mkaamua kuonesha mechi moja kwa moja bila ridhaa ya TFF na vilabu husika??.Soka yetu ya Tanzania inashindwa kuendelea kuotkana na ubabaishaji na kukosa uaminifu kulikojaa TFF..Yani nyie TFF akili yenu yote iko kwenye hela tuuuu...Inakera sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom