Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,755
Katika pambano la juzi la Simba na Yanga Jumla ya mashabiki 50,455 walishuhudia pambano hilo na kuingiza sh 390,568,000, huku Yanga na Simba kila moja ikiambulia sh 93.3 milioni.
Watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh 5,000, sh 7,000, sh 10,000, sh 15,000, sh 20,000 na sh 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh 59,578,169.49.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh 240,000, kamishna wa mechi sh 250,000, waamuzi sh 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh 2,000,000.
Umeme sh 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh 400,000, ulinzi wa mechi sh 5,860,000 wakati tiketi ni sh 7,327,000. Gharama za mchezo sh 31,115,183.05, uwanja sh 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh 12,446,073.22.
Huu ni wizi wa mchana kweupe.....Haiwezekani mechi iingize Tshs. milioni 390 halafu zenyewe zipewe nusu ya fedha hizo milioni 196 na nusu nyingine iende kusikojulikana.......Makato yanakuwa mengi mpaka yanakera.......TFF pamoja na kupata mabilioni ya fedha toka VodaCom, TBL na NMB bado tu hawatosheki na kuendelea kuvikamua na kuvinyonya vilabu........
Haiingii akilini kwa TFF kufanya malipo ya usafi,ulinzi, maandalizi ya mechi, waamuzi, kamisaa na gharama za tiketi kwa kutegemea mapato ya mechi......Vipi kama mashabiki wangesusia mechi hiyo,gharama hizo angelipa nani?......Inashangaza kuona eti mamilioni ya pesa yanakwenda kwa Kamati ya ligi, FDF na DRFA wakati hakuna chochote wanachokifanya kuendeleza soka......Huu ni WIZI.......Tena WIZI na UNYONYAJI wa mchana kweupe...
Inasikitisha sana.........