TFDA imara yenye watendaji Makini ni muhimu

TFDA imara yenye watendaji Makini ni muhimu

thirteen06

Senior Member
Joined
May 17, 2021
Posts
137
Reaction score
120
Hivi karibuni Naibu Waziri wa Afya alipokuwa akijibu swali kuhusu Umuhimu wa kurudishwa kwa TFDA alitoa majibu Yenye kuleta matumaini juu ya kurudishwa kwa taasisi hii muhimu ambayo ni mahususi kwa ajili ya usalama chakula. Kwa kuwa tayari tuna taasisi ya TMDA. Binafsi naona taasisi hii ambayo serikali imeonesha kukubali Umuhimu wake na kufikiria kuirejesha nafikiria iitwe TFA,, Yaani ijihusishe na bidhaa za vyakula tu.

Mathalan, hivi karibuni imebainika 43% ya chumvi inayotumika Tanzania haina madini joto. Madini joto Ni muhimu kwa ukuaji wa mwili na afya ya akili. Ukosefu wa madini haya hupelekea kupata ugonjwa wa goita, udumavu wa mwili na akili, na pia tatizo la kujifungua watoto njiti kwa akina mama wajawazito. Hivi Sasa ugonjwa wa goita umekuwa ukiongezeka miongoni mwa jamii ya watanzania siku baada ya siku.

Je Ni kwa kiasi gani jamii itaweza kuepukana na Uwepo na matumizi ya bidhaa hizi ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiingizwa kinyemela sokoni?
Hapo ndipo Umuhimu wa taasisi hii imara itakayowezeshwa kwa vitendea kazi madhubuti vinavyoendana na wakati unapoonekana.
IMG_20220309_203617_415.jpg
Screenshot_20220309-203738.jpg
IMG_20220309_205359.jpg
 
Mada muhimu sana hii lakini haitapata wachangiaji wengi kwsbb hujataja ''Tako'' wala ''Papuchi''

Serikali izingatie hilo.

Good luck then....!
 
Mada muhimu sana hii lakini haitapata wachangiaji wengi kwsbb hujataja ''Tako'' wala ''Papuchi''

Serikali izingatie hilo.

Good luck then....!
Hahaha,, kweli mkuu hii inashangaza kidogo.
 
Hakukua na tija yeyote ya kuhamisha udhibiti wa chakula na vipodozi kutoka TFDA kwenda TBS, zaidi zaidi tu wametengeneza loopholes kibao za wapigaji Kwa sababu ya uwezo mdogo wa TBS kwenye area hio.
 
Hata tbs uwezo wao pia unatia mashaka Sana,najua Wana kazi nyingi na nzito ila wakaongezewa na Mambo ya vyakula daaah ndo kabisa,mbona ilikuwa haina haja hata ya kubadilisha TFDA,wangekuwa serious mbona wangefanikiwa tu,mitaani huku watu wanatumia bidhaa za vyakula ilimradi tu siku ipite ila kiuhalisia bidhaa nyingi hazina tija kiafya kwa kweli,Kama wataamua kuiweka peke yake mamlaka inayosimamia bidhaa za vyakula Basi wahakikishe kweli waonekane wamepania kufanya kazi la sivyo itakuwa ni porojo za kisiasa za kuhamishahamisha hovyo majukumu ya taasisi hii na kupeleka huko Mara kuvunja hiki ilimradi tu ionekane kashkash za uhamishaji usio na tija kwa taifa hili,Mimi binafsi sijawahi kuona kazi nzuri kihivyo katika usimamizi wa afya za walaji wa bidhaa za vyakula hasa hizi za viwandani hasa kutoka nje ya nchi...
 
Siku hizi tunakula kuongeza siku tu bila kujali viwango vya vyakula hivyo
 
Ni wakati wa kuirudisha TFDA mana TBS imeshindwa kusimamia masuala mazima ya ukaguzi na udhibiti wa ubora wa chakula na vipodozi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom