MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Trump amteua Bolton kuwa mshauri wake mpya wa usalama
> Rais wa Marekani Donald Trump amemuondoa mshauri wake wa usalama wa taifa H.R McMaster na kumteua katika nafasi hiyo John Bolton, mtu mwenye msimamo mkali na aliyewahi kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.
=====
Hizi teuzi za Donald Trump zinanifanya nifikiri sana,
Maana watu ambao anawaweka kwenye nafasi nyeti ni wale ambao wanaiangalia dunia katika mtizamo wa tofauti kabisa. Kwanza ni wale Wazalendo sugu yaani wao wanaamini dunia nzima ni Marekani tu. Wapenda vita na vurugu na hata chembe chembe za diplomasia hazipo kwenye kauli zao kabisa...
Haya Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi CIA na amesikika wazi kabisa akisema yeye atawashughulikia maadui wa Marekani kama Iran, Korea na ambao wanajitegemea kama Wiki-Leaks. Haya kamchagua mama mwingine Gina Haspel kuwa Mkurugenzi wa CIA, huyu mwanamama ni mtata sana na historia yake inafahaika vizuri sana.
Sasa ya leo kali sana,
Bwana John Bolton kuwa Mshauri Mkuu wa mambo ya Usalama.
Hili linjemba lipo tangia enzi za Ronald Reagan, Bush Mkubwa na Bush Mdogo.
Yaani ni libalozi lakini halina hata chembe ya lugha ya staha..Kama alivyofanya Collin Powel kumsingizia Saddam Hussein kuwa na silaha za maangamizi, basi hili linjemba nalo lilikuwepo kwenye hiyo orodha ya watu walioshabikia sana Uvamizi wa Iraq.
NB 1: Kitu kimoja ambacho hawa wateule wa Trump wanacho ni chuki dhidi ya Uchina na Urusi.
Mataifa ambayo Marekani amesema dhahiri kwenye Mkakati wake wa Ulinzi (The National Security Strategy) kwamba wanafanya kazi kuharibu maslahi yake ya kiulinzi na Kibiashara.
Balozi Bolton aliwahi kusema kwenye Fox News kwamba Raisi wa Urusi Vladmir Putin ana akili sana na hilo ndilo linamwogopesha. Upande wa pili huyu jamaa naye anafahamika kwa kushutumu sana Uchina kama ambavyo Steve Bannon anasema kwamba Uchina imeshiriki kuharibu Uchumi wa Marekani. Yeye Bolton anasema Uchina anaiba teknolojia ya Marekani na hivyo ashughulikiwe tu. Kuhusu Korea Kaskazini Balozi huyu anasema jeshi litumike tu.
NB 2: Marekani ni taifa kubwa sana hapa duniani ambalo maamuzi yake yanaweza kuwa na madhara makubwa sana Usalama wa dunia pamoja na hali yake ya kiuchumi. Kipindi hiki chote mambo ambayo yanazungumzwa kuhatarisha usalama wa dunia ni:
Mwaka 2003 Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jemedari James Mattis aliwaambia hivi wanajeshi wa Sadam Hussein: I come in peace," didn't bring artillery. But I'm pleading with you, with tears in my eyes: If you https://jamii.app/JFUserGuide with me, I'll kill you all.".......(Sasa mtu kama huyu leo ndiye waziri wa Ulinzi unategemea nini ???)
Dr. Henry Kissinger, Zbigniew Brzezinski na George F Kennan na ubabe wao wote wa kushabikia vita walifika kipindi wakawa na uelewa kwamba wakicheza vibaya siasa za kimataifa basi Marekani inaweza ikashindwa Vita Baridi japo ina Uchumi mkubwa na nguvu kubwa sana kijeshi, wakaka mezani kufanya mazungumzo ndiyo dunia ikapata matokeo kama Detente, SALT na AMB Treaty: Diplomasia ndiyo ilipelekea hadi Raisi Ronald Reagan kumaliza vita baridi kwa amani mwaka 1989.Zamani kucheza siasa za kimataifa zilikuwa Rahisi sana kwasababu Mataifa mawili ndiyo yalikuwa na sauti (Urusi na Marekani). Lakini siku hizi mataifa yenye silaha na nguvu kijeshi yamekuwa mengi tupilia mbali makundi binafsi ya magaidi au makundi binafsi yanayofanya mashambulizi ya mtandaoni......
Ukweli mchungu ni kwamba,
Mahasimu wa Marekani kama Uchina, Urusi, Iran na Korea Kaskazini wana nguvu kipindi hiki kuliko kipindi chochote kuwahi kutokea huko nyuma. Nilikuwa naangalia The Munk Debate wanazuoni wa Marekani kama Prof. Stephen Cohen, Dr Henry Kissinger walikubali kwamba Marekani ina changamoto kubwa sana kiusalama kuliko wakati wowote ule kwenye historia yake.
Gideon Rachman wa chuo cha Cambridge ameandika kitabu "Easternisation: War and Peace in Asina Century", Prof. Graham Allison wa Harvard University amendika kitabu "Destined for War: Can America and China escape the thucydides Trap (Kilizungumziwa hadi kwenye Bunge la Marekani) ?" wamezungumzia hizi changamoto za Kiuslama za Marekani na kwamba akicheza vibaya imekula kwake. Wengine kama Prof John Mearshimer na Prof. Noam Chomsky waliongea kwenye Council for Foreign Relation na Vyuo mbali mbali vikubwa duniani kwamba Kipindi hiki mambo yamekaa vibaya sana kwa Marekani.
Je, unadhani hawa wateule wa Raisi Trump wanaweza kuitoa Marekani hapa ilipo kwa mabavu kama ambavyo tumeona Marekani ikifanya kwa miaka ishirini iliyopita. AU ndiyo wanaweza wakawa ndiyo chanzo cha uvunjivu wa amani hapa duniani na kuanguka kwa Marekani ?????
Updates:
Haya ni baadhi ya maneno ya wanasiasa wa Marekani baada ya huu uteuzi
Bernie Sanders mgombea Uraisi kwa kupitia Democratic Party anasema hivi:
Senator Jeff Merkley naye ameshangazwa na uteuzi huu akasema hivi:
Senator Ed Merkley naye alisema haya:
NB: Nimesoma hizi tweets kupitia mtandao wa RT News nikagundua kwamba siyo mimi peke yangu ninayeogopa, tupo wengi mno. Nahisi kama kuna vita kubwa sana inakuja huko mbeleni maana huu mwendo siyo mzuri kabisa na haujakaa kirafiki kwenye amani ya dunia:‘Trump lining up war cabinet’? Bolton’s elevation to NSC adviser fuels alarm
CC: Palantir , Iceman 3D , SirChief , Dotworld , Chief , Bukyanagandi , chige, JokaKuu , Nguruvi3 , zitto junior , Da'Vinci , ze kokuyo, Prof, izzo, TUJITEGEMEE , MASAMILA, Consigliere , haa mym , Red Giant, Bavaria, neo1, Bilionea Asigwa , jay-millions, Hussein Melkiory

- Mkakati wa nyuklia wa Korea Kaskazini,
- Mkataba wa nyuklia wa Iran,
- Hali ya amani nchini Ukraine,
- Hali ya amani kwenye Bahari ya Uchina na Taiwan,
- Hali ya Uchumi na Usalama Barani Ulaya,
- Hali ya Usalam nchini Syria,
- Hali ya Usalama nchini Israel na Palestina (kuhusu Yerusalemu)