Tetesi: Wizi wa Mamilioni ya Pesa Jijini Mwanza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tetesi: Wizi wa Mamilioni ya Pesa Jijini Mwanza.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndebile, Jun 8, 2012.

 1. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,635
  Likes Received: 1,992
  Trophy Points: 280
  Pesa zilizokuwa zimetolewa na benki kuu kama fidia ya kuzihamisha ofisi za makao makuu ya Idara ya afya ya jiji la Mwanza kutoka eneo la Makongoro (maarufu kama Kliniki) zimetafunwa na mkurugenzi wa jiji, daktari wa jiji na watumishi wa jiji wasio waaminifu. Ubadhilifu huo ulibainiwa na benki kuu hasa baada ya kuona zoezi zima la kuamisha ofisi za afya linasuasua na hasa zengwe la idara ya afya kukataa pendekezo lililotolewa awali na benki kuu la kuwajengea ofisi ambapo idara ilidai wapewe pesa taslimu ili wajenge wenyewe.

  Maofisa wa benki kuu walishtukia wizi huo hasa baada ya kuona idara ya afya ikihamishiwa kwenye majengo chakavu ya idara ya zimamoto yaliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Nyamagana, ndani ya ofisi hizo 'mpya' watumishi wanafanyakazi kama vile wamo kwenye ghala za pamba.

  Hatua iliyochukuliwa na benki kuu ilikuwa ni kuripoti wizi huo ambapo wajumbe kamati ya CHMT ya waliswekwa ndani na kutolewa baada ya muda mfupi.

  Uchunguzi wangu binafsi:
  Wakazi wa jiji wameanza kukosa imani na CHADEMA na hasa watumishi wa kada za chini kama walimu, manesi nk kwani mategemeo yao hasa baada ya jiji kuongozwa na chama hicho.
  Kuna wizi wa kutisha wa fedha za serikali hapa jijini, mamilioni ya fedha za mapunjo ya mishahara ya watumishi zimeliwa na mkurugenzi( chanzo cha habari hii ni cha uhakika)

  Hivi najiuliza, madiwani wa chadema mpo? Mbona Kabwe na wenzake wanatafuna raslimali za jiji nyie mpo!
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa tatizo liko wapi..kwani kuna lipi jipya kuhusu watu na kula pesa za umma
   
Loading...