Tetesi: Ufisadi chuo kikuu mzumbe

reg edit

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
402
496
katika pita pita zangu kwenye mitandao mingine ya kijamii nasikia wanafunzi wa chuo kikuu mzumbe mwaka wa tatu wanalalamika pesa zao kwa ajili ya mazoezi ya vitendo (field) zimechakachuliwa, wanadai badala pesa iwe calculated kwa siku 120 wao (department inayohusika na mikopo hapo mzumbe) wame-calculate kwa siku 104. Ikumbukwe kuwa kwa wanaopata mkopo 100% wanapata 10000 kwa siku kwa ajili ya hiyo field, maana yake ni kuwa kwa siku hizo 14 walizochakachua ni 140,000 kwa kila mwanafunzi wamechukua. Si hilo tu bali mbaya zaidi nasikia pia ambao wamepata supplementary hawajapewa mikopo yao mpaka leo kwa kigezo kwamba mpaka wakisha-clear hizo supplementary ndio watapewa mikopo yao.
 
hii kali ni nowma waache ukiritimba hawa si ndo wanajiita havard of africa vipi tena?:target:
 
Wacha mambo ya kusikia, toa uthibitisho wa unayoyasema. Kama ni tetesi tu usilete hapa JF. Pata kwanza uhakika wa unachosema, hapa ni grear thinkers sio mahali pa tetesi.
 
Back
Top Bottom