TENNIS: Australian Open AO 2020

Papaa Gx

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
10,085
15,664
Michuano mikubwa ya Tennis kwa upande wa Gland Slam imeanza kutimua vumbi hii leo huko Australia katika jiji la Melbourne. Michuano hiyo mikubwa inatarajiwa kufika ukomo hapo tarehe 2 ya mwezi wa pili 2020.

Wakongwe katika mchezo huo Roger Federer, Novak Djokovic pamoja na Rafael Nadal wanatarajia kushiriki katika michuano hiyo. Bigwa mtetezi Novak Djokovic anatarajia kutetea ubingwa wake.

Kwa upande wa wanawake bigwa mtetezi Naomi Osaka itampasa apambane ili kutetea ubingwa wake huku akisaka Gland Slam ya tatu.

Kwa upande wa mgao wa fedha kwa mwaka huu ni asilimia 13.6 zilizo ongezeka katika jumla ya fedha ya mgao. Mshindi ataibuka na kiasi cha dola 2,853,079 sawa na Tsh 6,562,081,700 huku mshindi wa pili akiibuka na kiasi cha dola 1,431,002 sawa na Tsh 3,291,304,600.

Wadau wa mchezo huu pedwa kina Victoire niah Mgagaa na Upwa Penison Ole BAK na wengineo wote karibuni hapa tujadili yanayo endelea huko Australia.
 
Coco gauff leo kaendeleza ubabe wake kwa kumchapa venus william,naomi osaka na serena nao wameshinda
 
Safi sana mkuu nami ni mpenzi sana wa Tennis,my money kwa ladies Serena Williams;nimefumba macho na kuyafungua mara pap Dar es Salaam nayo inaandaa moja ya Gland slam ya Tennis na F1 Grand Prix!!!!,Lewis Hamilton,Sebastian Vettel,Max(kichaa sana huyu),mzee kim R;wanatua pale JNIA tayari kwa Dar es Salaam Grand Prix!!!
 
Nimesikitika sana kusikia Bianca Andrescu kukosa kushiriki michuano hii ananikosha sana yule binti teenager tatizo injury za goti humsumbua sana, otherwise my favorite player for men side Rafael Nadal i wish aondoe gundu AO baada ya kucheza fainali 5 na kushinda moja tu
 
Hahahaa mkuu unaota?
Safi sana mkuu nami ni mpenzi sana wa Tennis,my money kwa ladies Serena Williams;nimefumba macho na kuyafungua mara pap Dar es Salaam nayo inaandaa moja ya Gland slam ya Tennis na F1 Grand Prix!!!!,Lewis Hamilton,Sebastian Vettel,Max(kichaa sana huyu),mzee kim R;wanatua pale JNIA tayari kwa Dar es Salaam Grand Prix!!!
 
Selena Williams atupwa nje michuano ya Australian Open, mwanadada kutoka Uchina Wang Qiang ameweza kumshinda mkongwe huo kwa seti 6 4, 6 7, & 7 5.
 
Coco Gauff Victory against Naomi Osaka - Highlights | Australian Open 2020 Round 3
 
Selena Williams atupwa nje michuano ya Australian Open, mwanadada kutoka Uchina Wang Qiang ameweza kumshinda mkongwe huo kwa seti 6 4, 6 7, & 7 5.
Hahahahahahahahah Enough is Enough,Ni muda wa ku retire atulie nyumbani and try to make another Baby.
 
Hahahahahahahahah Enough is Enough,Ni muda wa ku retire atulie nyumbani and try to make another Baby.
Yeye anajihisi bado ana uwezo....mwili unakataa....inabidi wapumzike kwa heshima...yeye na ndugu yake....umri umeenda....hawana kasi tena.
 
Coco Gauff: "Today was a huge boost in confidence!"
Australian Open 2020 R3 Press Conference
 
Serena ameshaanza kuzeeka sina hakika kama grabd slam ya 24 anayoitafuta kwa ajili ya kunfikia Margareth Court kama ataipata. Amepoteza 3 consecutive grand slams alizofika fainali.

Mimi toka Coco Gauff amwangushe Venus kwenye Wimbledon mwaka jana nimeanza kumfuatilia huyu kinda. Nina imani ana potential ya kufika mbali iwapo asipoumia au kupata vipigo vitakavyomtoa confidence. Coco ana game flan kubwa sana kuliko umri wake na hata serves zake zina nguvu. Akikomaa kuanzia mwakani atakapokuwa anaelekea miaka 17 lazima atachukua grand slam moja.
 
Kwenye doubles za Wanaume nimesikitika sana team yangu ya Lukasz Kubot na Marcelo Melo kutolewa. Pamoja na Kina Jamie Murray/Neal Skupski na top seed Pierre-Hugues Herbert/Nicolas Mahut pia kutolewa naona hakuna mwelekeo atakayetwaa doubles kwa wanaume. Wazee pacha Bob na Mike Brian bado wanaendelea lakini mwaka huu ni mwaka wao wa mwisho kushiriki Tennis maana watastaafu. Kiukweli yamekuwa ni exciting tournaments.
 
Wow. Tatizo mechi zinachezwa asubuhi. Any way kesho na keshokutwa nitaangalia fainal.
Im rooting for Muguruza. Kwa wanaume nipo na Thiem,mimi ni shabiki wa Nadal though katolewa namtakia afya njema awe tayari kwa French Open.
Im rooting for Thiem though najua kabisa Djikovic ni kinga wa Australian open.
Let the best win.
 
Mwenzenu nilikuwa kijijini na umeme ulikatwa hivyo hata simu sikuwa nayo. Nimerudi nakuta Serena, Nadal na Federrer wameshapigwa. Tusubiri final ya wanawake leo.
 
Huyu dogo anaitwa Domic Thiem kaniudhi sana. Ubingwa ulikuwa wake kazingua kinoma noma.
 
Inst-image-7.jpeg
 
Back
Top Bottom