Australia: Mahakama yatupilia mbali rufaa ya Djokovic kupinga Visa yake kufutwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Mahakama ya Shirikisho la Australia siku ya Jumapili Januari 16 ilikataa rufaa iliyoletwa na Bingwa wa Tennis duniani Novak Djokovic dhidi ya kufutwa kwa visa yake na kufukuzwa nchini.

Mahakama inaamuru kwamba rufaa itupiliwe mbali kwa gharama ya mlalamikaji," umebaini uamuzi huo ulioidhinishwa kwa kauli moja na majaji watatu, katika mkesha wa kuanza kwa michuano ya Tennis ya Australian Open.

Mserbia huyo alikuwa amenuia kutafuta taji la 21 la Grand Slam katika michuano hiyo inayopigwa nchini Australian.

Majaji watatu wa Mahakama hiyo walisikiliza kwa saa nne hoja za wawakilishi wa Bingwa huyo wa Tennis duniani na zile za serikali, kabla ya kuondoka katika chumba cha mahakama kwa minajili ya kuchukuwa uamuzi.

Katika hitimisho lake alilowasilisha Jumamosi mbele ya Mahakama, Waziri wa Uhamiaji Alex Hawke alibaini kwamba kuwepo kwa Djokovic nchini "kuna uwezekano wa kusababisha hatari ya afya".

Amesema kumkubalia Novak Djokovic kubaki nchini humo na kushiriki michuano hii itaongeza"hisia za kupinga chanjo" na inaweza kuwazuia Waaustralia kupata chanjo zao za nyongeza wakati kirusi kipya cha Omicron kinaendelea kusambaa kwa kasi nchini kote.
 
Safi sana. Sheria ya michuano imeweka bayana kuwa washiriki wawe inoculated. Wewe Jokovich hutaki sasa Australia ifanyeje? Ina hali ya kulinda raia wake.
 
Safi sana kwa Australia kuonyesha ni jinsi gani wanalinda borders zao na kuishi kwa misingi ya kisheria,ukija kwangu ni LAZIMA uvue viatu kuingia sitting room,hii ndio sheria yangu kama hukubaliani nayo usije kwangu!
 
Huyu jamaa ni pumba sana,
Watu na inchi yao unakata na rufaa?
Haya enda huko ukacheze na wajinga wenzako
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom