Tengeneza "WHY" kisha "HOW" zitajipanga

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,836
#TAECOLTD

Tarehe 11 February mwaka 1990 katika jiji la Tokyo, Japan kulitokea tukio ambalo lilijenga historia duniani. Hii ilitokana na pambano kubwa la masumbwi lililofanyika kati ya Mike Tyson na Buster Douglas.

Wakati pambano hili linafanyika Tyson alikuwa ni bondia wa kuogopwa na wa kutisha ambaye alikuwa akishinda kwa KO katika kila pambano lake lililopita, hivyo kila mtu hakuwa na shaka kuwa Tyson angeibuka mshindi kabla raundi tatu hazijamalizika kama iilvyokuwa kawaida yake.

Mara baada ya kuanza pambano kama kawaida Tyson alitumia uwezo wake na nguvu zake kumshambulia adui yake kwa nguvu na kwa masumbwi makali akitarajia kumuangusha na kumshinda katika raundi za mwanzo. Cha kushangaza hadi raundi ya nane inafika mpinzani wake alikuwa bado amevumilia na bado anaendelea kupigana.

Ilipofika raundi ya 8 Tyson alimpiga ngumi ya katafunua (Uppercut) mpinzani wake na alianguka kwa anguko ambalo hakuna mtu alitarajia atainuka tena.

Lakini wakati Tyson anaanza kufurahia kuwa ameshinda, akashangaa Buster Douglas anainuka na akaja na nguvu mpya na ilipofika raundi ya 10 akamshinda Tyson kwa KO na kuweka historia kuliko matarajio ya watu wengi.

Miaka 25 baadaye, Douglas alihojiwa na kuulizwa ni nini kilimfanya ashinde pambano lile, majibu yake yanatoa funzo kubwa sana.

Anasema wakati amesaini kupigana na Tyson mama yake alikuwa anaumwa sana na kabla tu ya pambano alifariki na kabla hajafariki alimwambia kuwa zawadi kubwa anayoweza kumpa ni kumshinda Tyson. Lakini pia, kipindi anaenda kupigana na Tyson alikuwa ametoka kuachana na mke wake wa ndoa.

Lakini pia maisha yake ya kifedha yalikuwa yameyumba. Alikua na hali ngumu sana kiuchumi, hivyo kumshinda Tyson ilikuwa ni fursa muhimu kwake kubadilisha maisha yake kiuchumi.

Hivyo ushindi wake ulianzia kwenye “SABABU” hizi. Douglas anasema ili ufanikiwe hata pale watu wanapofikiri hauwezi kufanikiwa, kitu cha kwanza ni kuwa na sababu(why) yenye nguvu kuliko kuanza kuwaza utafanikiwa kwa namna gani(How). Ili mradi sababu yako(Why) ina nguvu basi namna(How) lazima itapatikana.

Lakini pia wakati ameanguka chini na akaona kuwa kama ameishiwa nguvu kabisa za kuinuka tena, maswali mengi yalipita ndani yake. Je,niendelee? Lakini mbona nimeishiwa nguvu? Hata hivvyo nimejitahidi nimepigana hadi raundi hii nikiacha hapa nimefanikiwa pia

Lakini mara baada ya kukumbuka sababu yake (why) akaamua kuamka kuendelea bila kujali atashindaje (how).

Douglas anasema mara baada ya kuamka aliona macho ya Tyson yakikata tamaa kwani hakuamini kama anaweza kuinuka tena; na kwa maelezo yake anasema hapo ndipo alipomshinda Tyson. Alimpiga mfululizo na kufika raundi ya 10 Tyson akaishiwa nguvu hivyo akamshinda kwa Knock Out (KO
See You At The Top.!

TAECOLTD
8b61a9f0d32991a787852ff2bf22e386.jpg
 
darasa zuri lakini umenikumbusha machungu ya siku ile tyson alivyopoteza pambano hilo watu tulikesha kusubiri pambano halafu mchizi akapigwa inaniuma sana!
 
Kwa msemo wa Kiswahili tunasema 'Penye nia, kuna njia'
 
Back
Top Bottom