Kuna wakati waziri mmoja wa michezo wa Cameroon aliwahi kuikejeli FIFA, Cameroon wakafungiwa kushiriki hatua yoyote ya kombe la Dunia. Ilibidi Waziri Mkuu wa Cameroon aombe msamaha kwa FIFA na kusema kauli iliyotolewa na waziri wa michezo ilikuwa ni maoni yake tu na wala sio msimamo wa nchi, basi hapo ndio FIFA wakaondoa ban. Kwa mfano huo nadhani unaweza kuona nguvu za FIFA juu ya mamlaka ya nchi!