Tenga aula

Tenga aula

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
843
Reaction score
1,024
Ukitazama kwa ujumla mchakato wa uchaguzi wa Tff utagundua umejawa na kichefuchefu cha ukiukwaji wa kikatiba kwa muda mrefu. Ifahamike hiki ndicho walichopanda muda mrefu kwa kigezo cha kudumisha utawala bora Kama wanavyo jitaidi kunadi katika vichwa vya watanzania na si kwa kiwango gani wameweza kutuvusha katika harakati za Maendeleo ya soko katika Kuhama kwenye kung'ang'ana kwenye kupanda kwenye viwango vya FIFA na kusahau kushiriki kwenye mashindano makubwa mfano Afcon.

Kwa kusema hayo turudi kwenye Swala Zima la UCHAGUZI ni katiba gani iliyotumika kuitisha mchakato wa uchaguzi ? Hapa utagundua magumashi ya RAISI wa tff na kamati yake ya uchaguzi iliyojaa maswahiba wengi ambao Leo hii wametufikisha hapa tulipo kwa madudu ya kamati ya kishkaji.

Mara baada ya kuona hili serikali kupitia wizara yenye dhamana na michezo ikaona si busara mambo yakahalibika zaidi, wakaamua kutoa maelekezo nini cha kufanya TFF kwa kunusuru soka la bongo. Wizara ilielekeza mambo yafuatayo;

1. Tff kuitisha mkutano wa UCHAGUZI ifikapo mei 25, 2013.

2. Kufanya UCHAGUZI kwa katiba ya mwaka. 2006.

Hapa ndipo kunakivumbi Kati ya serikali na Tff kwa mtazamo wangu sioni Kama kunashida katika vipengere hivi kwa kiongozi anayelitakia Maendeleo soka la tanzania na si hawa wachumia matumbo(Tenga).

Ni Mara kumi FIFA kutufungia kuliko kulea manyamazongo katika soka la bongo.swala la kujiuliza tenga anaongea Kama nani wakati muda wake umekwisha kikatiba kuwa kiongozi wa tff Kama si kuatamia na kuhozi madaraka kwakutaka kulisishana Kama familia ya kifalme.

Ifahamike kwa watanzania TENGA ameudanganya umma wa watanzania kwamba wizara imekubali kukaa na viongozi we tff tarehe 19/3/2013 taarifa hizi si za kweli hakuna kikao kitakacho kaa tarehe hiyo Bali Tff imeagizwa kufanya Kama wizara ilivyoshauri katika mambo makuu mawili.

Hapa ifahamike kuwa vitisho vinavyotolewa na VIONGOZI wa tff juu ya kufungiwa kwa Tanzania Kama serikali itaingilia shughuri za Tff lakini ikumbukwe chama chochote cha Mpira duniani hakiwezi kupewa kibali na FIFA cha kushiriki na kuendesha mashindano yoyote Kama hakijasajiliwa kwa kufuata sheria za nchi husika, kwa hapa Tanzania mwenyemajikumu hayo kisheria ni Baraza la Michezo Tanzania (BMT) ambayo yote haya yapo chini ya wizara ya habari ,vijana,utamaduni na michezo. Ndio maana waziri husika alitoa ushauri kwa Tff ninichakufanya maana wamekiuka kanuni na sheria za BMT.

Aidha pia huu utakuwa muendelezo wa makusudi wa kiongozi Tenga kuendelea kuwatenga VIONGOZI wanao onyesha nia ya kuwasaidia na kuinua soka nchini kwa makusudio ya kuficha matapishi yake(uchafu). Sera yake ya kukaba roba demokrasia katika michezo haitamsaidia zaidi ya kustafu vibaya.
 
mm nasema na hapa nitamkumbuka sana mwl wangu SILLA SAID MZIRAY soka la tanzania linaendeshwa kibabe sana. na kwamba tenga si mzuri kama watu wanavyomshobokea.

nimethibitisha haya baada ya kuona tenga akibaka demokrasia na kumruhusu mgombea pekee wa uraisi awe mjomba wake NYAMLANI.

swali la kujiuliza kwan haya hayakutokea uchaguzi uliopita?? je wanafikiri wanaweza kumnyamazisha wambura just like this??inajulikana kwamba fedha za TFF hazina auditing lich aya kuwa na mapato mengi wanayoingiza. haya yote ni mambo ambayo tena anajua yanaweza kumfanya akawekwa kiti moto baadae
 
Mbona kichwa cha habari hakilingani na taarifa uliyoandika? Halafu Kama nina kumbukumbu sahihi haya siyo maagizo aliyoyatoa waziri mwanzo - aliagiza uchaguzi ufanyike kwa kutumia katiba ya zamani. Haya maagizo mapya yalitolewa lini au ni baada ya kukutana na TFF?
 
Back
Top Bottom