Tenga aridhia maelekezo ya serikali

Tenga aridhia maelekezo ya serikali

KESSY FRANCIS

Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
42
Reaction score
11
TENGA AKUBALIANA NA MAAMUZI YA SERIKALI

Watanzania sasa wanafahamu na Ulimwengu kuwa soka la Tanzania liko rehani kwa ajili ya uamuzi wa kiongozi wake TENGA kwa kuamua makusudi kuandika historia mpya ya kupambana na mabadiliko ambayo Watanzania na wapenda michezo wote, wangependa kuona soka la nchi hii linapiga hatua kubwa na kuwa kichocheo kikubwa cha vijana kujiajiri na kuongeza kipato, lakini yote hayo yamegonga mwamba chini ya uongozi wa KIFEDHULI wa TENGA.

Tenga alianza vizuri kidogo lakini anaondoka Madarakani huku akiwa amekandamiza demokrasia kwa kiwango cha juu sana kwani ametawala kiimla.

Mabadiliko ya katiba aliyofanya kwa kutumia waraka kubadilisha sehemu muhimu ya katiba haikuwa sawa, kwani alipaswa kikatiba kuitisha mkutano mkuu ili theluthi mbili ya wajumbe HALALI wapitishe mabadiliko, cha ajabu matakwa ya katiba hayakufuatwa na ushahidi upo.

Wapo WAJUMBE waliokata mchakato na kususia na wakaonekana wasaliti. Vitimbi vya kukaba roba demokrasia havikuishia hapo bali alienda mbali zaidi katika mchakato Mzima wa kuwapata viongozi wapya baada ya kudiriki kuwatupa nje wapinzani wake 2008 ( MALINZI) kwa vigezo vya kuwa hana uzoefu ( huku akiwa amesahau walivyochuana nyuma) n.k.

Hizi hoja zimekuja wakati ambapo Malinzi amekuwa tishio kwake na wagombea anaotaka kuwaweka, hatimaye Malinzi akakatwa jina vigezo vya kihayawani. Lakini mpaka sasa kikatiba kulipaswa kuwa na safu ya UONGOZI mpya maana kikatiba TENGA si kiongozi tena.

Ameweka kiongozi mmoja mmoja kugombea! Hiyo ndio demokrasia ya Tenga tunayemfahamu.
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo walieleza kuwa habari yao na TFF inaeleweka na halipotoshwi.

Kimsingi yapo mambo 4 Wizara ilisisitiza.

1. TFF wafuate kifungu cha katiba yao cha kufanya mabadiliko, maana hakikufuatwa

2. TFF wafuate sheria na taratibu za Baraza la Michezo kusajili katiba iliyorekebishwa kihalali, ambazo hawakufuata

3. Serikali haijaiingilia TFF wala FIFA, Bali inawasaidia wao kufuata utaratibu uliokubaliwa na wote.

4. Kuepuka migogoro isiyo ya lazima na kuheshimu sheria za nchi na zao.
Hii tabia ya Tenga kuvurunda kwa kutumia mwavuli wa FIFA kamwe haitampeleka mbali zaidi ya kuonekana anasaliti nchi yake kwa maslahi yake binafsi.

CHA kufanya ni TENGA kuitisha mkutano Mkuu ili moja wapitishe mabadiliko ya katiba na pili wafanye UCHAGUZI wao wa kikatiba.

Serikali isifumbie macho maovu ya Tenga kwani kukaidi maagizo ya serikali ni dalili ya kutaka taifa kufungiwa na FIFA na akumbule TFF aliikuta na ataiacha na ameandika historia CHAFU ambayo kizazi na kizazi watamlalamikia kwa uamuzi wake wa KIBINAFSI
.
 
Endelea na upuuzi wako. Tunasubiri TFF iongozwe na nyinyi vichwa vya panzi baada ya kutengwa na kujitenga na jamii ya soka ulimwenguni. Inawezekanaje Tenga afanye yote hayo huku mnamtazama hadi hali inakuwa hivi?

Wenye akili tunajua kilichonyuma ya pazia. Tenga amefanya vizuri kiasi, sasa angeachia kila kitu ili serikali hii dhaifu iinie mkenge inaoutafuta
 
Heading na content ni vitu viwili tofauti kabisa! Ngoja nikuache uendelee na porojo zako
 
Heading na content ni vitu viwili tofauti kabisa! Ngoja nikuache uendelee na porojo zako

Hata mimi nimeona hivyo hivyo mkuu, kinachoongelewa na kilichopo kwenye kichwa cha habari yenyewe havina mahusiano kabisa!
 
Tenga waachie dude lao warudi kule kule walikotoka full migogoro...mtu kama Malinzi kumwachia soka la Tanzania ni kutafuta KIYAMA cha mpira wa miguu ... !!
 
kama ilivyo ada viongozi wengi wa kiafrika 90% hugeuka na kuwa madikteta ndo maana hata simshangai Tenga na siasa zake
 
Hahahaha yale yale watu wa jf bhana wakwanza kucomment kwenye uzi ndo utoa mwongozo kwa wote watakaofuata,akiponda basi jua wote wataponda,akisifia hali kadharika,kama huna cha kuchangia kaa kmya sio kutukana tu,tutawatofautisha vipi na lameck wa ccm?kama huna hoja piga kimya sio kumshambulia m2 kwa matusi,hasa wewe..........anyway!
 
Tatizo la tenga ni magwanda yanamzuzua ngoja atakavyotoswa na DJ
 
malinzi alishindwa kuongoza timu ataweza kuiongoza TFF?Hebu acheni ubulicheka!

Malinzi anataka uongozi wa TFF ili kwenda kuiba na sio kwenda kuendeleza soccer kwani uwezo huo hana!! Sasa serikali isijiingize mkenge kwa kutaka kuwasaidia wezi kwasababu ya njaa ya naibu waziri Amos Makalla!!
 
Tatizo la tenga ni magwanda yanamzuzua ngoja atakavyotoswa na DJ

tumeingia kwenye siasa tena hv mambo ya ccm na chadema yatakwisha ln? tutanaka utaifa sasa HAIJALISHI WEWE NI CHAMA GANI ILA TUNAJUA WEWE NI MTANZANIA!
 
malinzi alishindwa kuongoza timu ataweza kuiongoza TFF?Hebu acheni ubulicheka!

Mkuu meningitis usisahau kwamba Malinzi kuwa na sifa za kugombea uraisi TFF ni kitu kimoja na kuwa na uwezo (binafsi) wa kuongoza ni kitu kingine!

Kama alishindwa kuongoza timu kinachotakiwa kufanywa ni kuwafahamisha wajumbe wapiga kura juu ya udhaifu huo ili wasimchague kama walivyofanya mwaka 2008 aliposhindana na Tenga. Lakini huu ujanja ujanja mnaotaka kuufanya haukubaliki hata kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Malinzi anataka uongozi wa TFF ili kwenda kuiba na sio kwenda kuendeleza soccer kwani uwezo huo hana!! Sasa serikali isijiingize mkenge kwa kutaka kuwasaidia wezi kwasababu ya njaa ya naibu waziri Amos Makalla!!

Ndinani issue hapa si Malinzi kwenda TFF kuiba ama vinginevyo, kama ni mwizi mbona hajawahi kushtakiwa mahali popote achilia mbali kutiwa hatiani na kufungwa. Chuki zenu kwa Malinzi zisiwafanye kuwa vipofu hata kwa mambo yaliyo wazi kiasi hiki.
Hapa tunazungumzia TFF kuifuata kikamilifu katiba yao iko wazi sana juu ya utaratibu wa kuifanyia mabadiliko hata mhitimu wa darasa la saba bajua utaratibu huo wa kikatiba wa namna ya kuifanyia marekebisho katiba ya TFF.

Hakuna kifungu kinachoelekeza kurekebisha katiba kwa waraka na hakuna mtu huru anayeweza kuthibitisha kwamba wajumbe waliokubali mabadiliko kwa njia ya waraka wanakidhi idadi(akidi)??
Mtu yeyote anayetetea huu uharamia unaofanywa na TFF ni dhahiri kwamba yeye ndiye anataka kutuibia watanzania kwa kutaka Nyamlani apate mteremko wa kuwa raisi.

Hivi nikiwauliza mnaogopa nini Nyamlani kushindanishwa na watu wengine mtanijibu nini???
 
TFF wana Rais wao na hilo ndo tatizo la yote haya
 
:closed_2::banplease: :banplease: :banplease: :banplease: :banplease: :banplease:
 
hata hivyo uzi huu ni wa jukwaa la michezo kivipi sasa uwe wa jukwaa la siasa?jamani greatthinkers ndo hii, hapa tuongee siasa na msitakabali wake kuna jukwaa la michezo mkalumbane na FAT yenu hko sijui ndolanga karudi?
 
Swala la muhimu hapa je TENGA alifuata utaratibu wa kisheria? Kama la kwa nini na kwa manufaa ya nani? Je mbona anaogopa Wajumbe walimchagua hapo awali??
 
Back
Top Bottom