Huyu naye kwa kujichanganya hajambo! Hawakumuuliza waliofanya fujo ni chadema au polisi! Kama ana hamu ya kufuta chama alete tupige kura kupendekeza chama gani kifutwe kama hatajikuta chama chake ndo kinatakiwakifutwe!
Itakua poa sana.Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.
Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyajati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.
Source:Habari Radio Tumaini.
Si ndio alibariki mauaji,kwa sababu yeye alitoa katazo kwa CDM lakini CCm kila mkoa walikuwa na shughuli ya hadhara kwa wananchi mwache ajidanganye ulivyosikiliza alilaani mauaji yaliyofanywa na polisi au amebariki polisi kupiga mabomu wananchi ndani ya ofisi ya vyama vyao
Ngoja mie nipite tuu maana siasa si fani yangu na wala sijui cha ku-comment hapa!
Dah!mungu akubariki sana mkuu.Ningekua kama wewe walahi ningenenepa balaa.Ngoja mie nipite tuu maana siasa si fani yangu na wala sijui cha ku-comment hapa!
Anazidi kuhalalisha kile nilichosema ktk ule uzi wangu wa sababu 3 zilizoko nyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema. Vifo hivyo, vinataka kuhalalisha jambo. Kama si kuchafua chadema, basi ni kuifuta chadema. Exactly, kama alivyosema rafiki yangu. Nijuavyo na niaminivyo, hilo halitawezekana.
Pili, kwa kuwa mjadala wote sasa umeelemea polisi kwa kubebeshwa lawama zote, Tendwa anataka kubadili mjadala uwe Chadema na vifo. Watz wa leo siyo wa miaka 50. Hawatafanikiwa.