Tendwa akiri kukurupuka aapa kutorudia tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa akiri kukurupuka aapa kutorudia tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Sep 23, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,772
  Trophy Points: 280
  Tendwa anywea Send to a friend Thursday, 23 September 2010 07:58 0diggsdigg

  Exuper Kachenje
  BAADA ya kupewa karipio na Tume ya Uchaguzi (Nec) kuhusu muda wa kumaliza mikutano ya kampeni, Msajili wa Vyama Siasa, John Tendwa jana hakuwa na majibu mengine zaidi ya kukubaliana na hoja za chombo hicho chenye dhamana ya kusimamia uchaguzi mkuu.

  “Kwa nini niwe na comment (maoni) kwa kauli hiyo ya Nec? Tume imesahihisha hilo," alisema Tendwa baada ya kuulizwa maoni yake dhidi ya tamko la Nec la kumtaka asivuke mipaka ya kazi zake.

  Tendwa, ambaye anashughulikia usajili wa vyama na kusimamia Sheria ya Gharama za Uchaguzi, alionekana kuichokoza Nec aliposema kuwa muda wa kampeni umeongezwa hadi saa 1:00 usiku badala ya saa 12:00 jioni kama ilivyokuwa awali wakati akifafanua madai kuwa mgombea urais waq CCM, Jakaya Kikwete anahutubia hadi saa 1:00 jioni.

  Nec, ambayo ndiyo inayoratibu shughuli zote za kampeni na kusimamia uchaguzi, ilimjibu kwa kueleza kuwa Tendwa amevuka mipaka kwa kutetea baadhi ya wagombea wanaofanya kampeni hadi saa 1:00 usiku, kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

  Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame alisema chombo chenye dhamana ya kupanga ratiba za mikutano ya kampeni na uchaguzi ni tume yake na si ofisi ya Msajili na kusisitiza kuwa muda wa mwisho wa mikutano hiyo ni saa 12:00 jioni.

  Jana, Tendwa, ambaye kwa kawaida ni mtu anayeonekana kujiamini, alisema: “Kwa nini niwe na comment kwa kauli hiyo? Tume imesahihisha hilo.
  "(Nec) Yenyewe inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria. Sasa kama imeliona hilo ni kosa na kusahihisha, ndivyo hivyo. Sina tatizo."

  Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amekuwa akishutumiwa na wapinzani kwa kuendesha mikutano ya kampeni nje ya muda uliowekwa na Tume, vikidai alifanya hivyo alipokuwa Arusha, Babati na Mbulu.

  Naye katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alisema sakata hilo ni malumbano baina ya viongozi wa vyombo hivyo viwili hivyo hawezi kuzungumzia, akisema "ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime".

  “Malumbano yao (Nec na msajili) ni ya kisheria, mimi ni mkubwa kwenye siasa. Saizi yangu ni malumbano ya kisiasa na vyama vingine," alisema Makame."Wao wote wapo kwa mujibu wa sheria wameteuliwa na wanatekeleza majukumu yao. Hayo ni makubwa nawaachia wenyewe, mimi ni mwana siasa."

  Katika hatua nyingine Tendwa amepuuza madai ya Chadema kwamba haina imani naye tena kwa sababu ameonekana kuipendelea CCM. Tendwa alisema hayo ni maoni ya chama hicho.

  Akihutubia mkutano wa kampeni, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Tendwa anatakiwa ajiuzulu baada ya Nec kueleza kutokubaliana na kauli yake kuhusu mabadiliko ya muda wa kumaliza mikutano ya kampeni.

  Dk Slaa alisema kuwa wanasheria wa Chadema wanalishughulikia suala hilo kwa kuwa Tendwa haaminiki na anatupeleka sehemu ambako hakufai kwa kuwa wananchi wamechoka sasa.
  Lakini Tendwa jana alisema: “Hilo ndio tatizo lao; waendelee hivyo hivyo kutokuwa na imani nami, lakini mimi nafanya kazi yangu.”

  CCM pia imejibu madai ya wapinzani waliodai kuwa ahadi zinazotolewa na Kikwete kwenye kampeni zake za urais hazimo kwenye ilani ya chama hicho.
  Makamba alisema wanaodai ahadi za Kikwete hazimo katika Ilani ya CCM wamepungukiwa na maarifa na hawakuisoma.
  “Tumetaja kuboresha usafiri wa anga, usafiri wa majini na nchi kavu, kuwezi kuboresha usafiri wa maji bila kununua meli,” alisema Makamba.

  UPUUUZI WAKO WA CHAMA CHA MAJAMBAZI USITULETEE WANANCHI OLE WAKO NINGEKUWA KARIBU NIKUCHAPA KIBOKO NA UZEE WAKO WENZAKO WANAZEEKA VIZURI WE UNAZEEKA NA UJINGA LOH!!WANAFAMILIA MUELIMISHEN BABA YENU ASIAIBIKE TENA
   
Loading...