Tendo la ndoa uzeeni.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendo la ndoa uzeeni....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dr. Chapa Kiuno, Dec 3, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Je, wazee wenye umri mkubwa bado huwa hamu kubwa ya tendo la ndoa? Utafiti wa sasa unaonesha kwamba jinsi mtu anavyozidi kuwa mzee uwezo wa kuonja, kunusa, kusikia na kuona hupungua. Pia uwezo wa kusisimuliwa kwa kuguswa hupungua pia.

  Kiasili uwezo wa kusisimuliwa kimapenzi na uwezo wa kufanya tendo la ndoa pia hupungua (libido)Pia Utafiti unaonesha kwamba uwezo wa kufanya mapenzi huweza kupunguza kutokana na umri kuwa mkubwa ingawa pia umri kuwa mkubwa hauwezi kuzuia kabisa hamu ya tendo la ndoa (terminate).

  Kuna ripoti kwamba wanaume na wanawake wenye umri wa miaka 50 hadi 80 bado wana hamu kubwa ya kufanya mapenzi (libido) na si kufanya tu bali kufurahia mno tendo lenyewe.

  Kuna imani potofu nyingi kuhusiana na tendo la ndoa katika umri mkubwa zifuatazo ni baadhi tu ya hizo imani; Kushindwa kushiriki tendo la ndoa ni matokeo ya umri kuwa mkubwa.Tendo la ndoa ni hatari kwa wazee wenye umri mkubwa. Uwezo au hamu ya tendo la ndoa (libido) hupungua kwa kadri mtu anavyozeeka.

  Yote hapo juu si sahihi kabisa. Hizo imani potofu zipo kwa muda mrefu na zimekuwa zikisababisha watu wenye umri mkubwa (wazee) kushindwa kufurahia tendo la ndoa au uumbaji wa Mungu.

  Je, mabadiliko ya mwili kwa wanaume wazee huathiri vipi tendo la ndoa?

  Kawaida wanaume wazee huhitaji muda mrefu ili kuweza kusisimka.

  Kile kilichokuwa kinahitaji sekunde chache hadi dakika chache katika umri wa miaka 19 huhitaji zaidi ya dakika 15 katika umri mkubwa kwa mwanaume.

  Wanaume wengi wenye umri mkubwa hupona ugonjwa wa Kukosa uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa kujifunza matokeo na athari za umri kwenda sana (Uzee) Katika umri ulioenda wanawake wazee wahahitaji kufahamu kwamba wanaume wazee huhitaji muda mwingi na wakutosha kuuandaa jogoo awike.

  Mabadiliko mengine ambayo hutokea kwa mwanaume mzee sana ni kupotea kwa uwezo wa kufika kileleni tofauti na wakati akiwa kijana.

  Hii ni kutokana na Kukosa hisia (sensation) za tendo la ndoa. Pia kiwango cha sperms anazotoa hupungua hivyo mwanamke mzee asiwe na mtazamo wa kudhani kuwa uwingi wa sperms ndio uzuri wa tendo la ndoa.

  Mnaweza kumtembelea kwenye Blogu yake: http://www.mbilinyi.blogspot.com/
   
 2. c

  chief kwanza New Member

  #2
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafurahia kuwa mmoja kati ya member wa jamii forum
   
 3. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Karibu kaka/dada, lakini naona umekosea njia kidogo.
   
 4. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Naomba utumie lugha sanifu tusije tukapoteza maana.... Karibu mwenzangu, ila post hii inapaswa kuandikwa katika introductions....:)
   
 5. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mmh!
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  tih tih tih :D

  eeh

  Karibu tupo hapa Chief

  Tukirudi kwenye maada tunaye senior citizen humu jamvini? Je anaweza kutusaidia hili?

  Zaidi ya kusoama maadnishi mie sijawahi kusimuliwa inakuwaje inapofikia umri huo; lakini pia njianai natana na watu wazima wa umri huo wakiwa ngangari na vibinti!
   
Loading...