GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,648
- 10,844
Sijui Kiswahili chake fasaha kama ni haiba au hulka, au silka, n.k, ila waliotuletea vitabu wanaiita TEMPERAMENT.
Kuna faida kujifahamu na kuwafahamu wengine. Kutakusaidia kuweza kushirikiana na wenye "temperament" tofauti na yako, na hata wakati mwingine, kujua aina ya mtu unayehitaji kushirikiana naye katika majukumu fulani.
Magufuli alikuwa CHOLERIC. Lakini nina mashaka kama yeye mwenyewe na wengi wa wasiaidizi wake walikuwa wanalifhamu hilo.
Nilipokuwa Chuoni, nilicheka sana nilipokisoma kitabu cha Saikolojia kilichodadavua hizo temperent. Nilijionea huruma kwa jinsi nilivyokuwa nikikwazwa na matendo ya "roommate" wangu ambaye alikuwa ni "Sanguine", lakini baada ya kukisoma hicho kitabu, sikupata shida tena.
Alipofanya "vituko" vya Kisanguine, sikukereka kwa sababu nilijia huo ni udhaifu wake kama na mimi nilivyokuwa na madhaifu yangu, ambayo hayakufanana na yake.
Ni viongozi wachache tu ndiyo ninaofikiri kwamba huenda ninafahamu "temperament" zao. Na ninaposema viongozi, ni pamoja na wa Kisiasa, biashara, kidini, wasanii, n.k.
Na haya ndiyo makundi yenyewe:
1. CHOLERIC
Nina uhakika hayati Magufuli na Benjamin Mkapa wapo kwenye hili kundi.
Kwa kawaida, Choleric ni viongozi kwa kuzaliwa. Wana tabia za kijeshi na wasioogopa upinzani. Wakati mwingine, huonekana kustawi zaidi penye upinzani. Wengine huwachukulia kama watu wakatili na wasiokuwa na huruma. Ni watu wanaosimamia kile wanachokiamini bila kujali misimamo na hisia za wengine.
Viongozi wengine wanaoweza kuwa ni Choleric ni pamoja na Tundu Lissu, Dr. W. P. Slaa, Bishop Benson Bagonza, hayati Edward Moringe Sokoinei, Job Ndugai, Dr. Josephat Gwajima, n.k.
2. PHLEGMATIC
Ni wanadipolmasia wa kuzaliwa. Hutafuta usuluhishi kwa gharama yoyote. Ingawa, mara nyingi hawajipendekezi kuwa viongozi, ikitokea fursa wakapewa uongozi, hufanya vizuri. Ni watu wajanja pia, ambao wana uwezo wa kuwatumia wengine kwa manufaa yao bila wao kujua kuwa wanatumiwa. Kwa kawaida, phlegmatic si mwepesi kugundulika anapokuwa kachukia au kafurahi. Ndilo kundi la watu ambalo ni rahisi kuishi nao. Miongoni mwa viongozi ninaofikiri wapo kwenye hili kundi ni pamoja na Dr. Jakaya Kikwete, Dr. Samia Suluhu Hassan, Ally Hassan Mwinyi, Salim Ahmed Salim, Bernard Membe, Jaji Joseph Warioba, Amani Abeid Karume, n.k.
3. SANGUINE
Hawa ni waongeaji sana. Wanapenda umaarufu, na ni wazuri sana kuhamasisha. Wana changamoto pia ya wakati mwingine kuongea bila kufikiria. Kutokana na uwezo wao wa kuhamasisha, anaweza akakuahidi kukununulia ndege ndani ya mwezi mmoja na ukamwamini kwa asilimia mia moja huku hana uwezo wa kujinunulia hata baiskeli.
Wana tabia ya kukuza jambo likaonekana ni kubwa kuzidi uhalisia wake. Wakati mwingine, "Sanguine" akikuambia jambo fulani ni zuri sana au baya sana, si kosa kulishusha kwa asilimia hamsini hivi ili kuweza kupata uhalisia wa alichokisema.
Miongoni mwa viongozi ninaofikiri wapo kwenye hili kundi ni pamoja na Godbless Lema, Yusufu Makamba, Paul Makonda (japo anaweza pia akawa ni Choleric), Joseph Kasheku Msukuma, Albert Chalamila, n.k.
4. MELANCHOLY
Wanajulikana kuwa ni wakimya na wana akili sana. Hawapendi umaarufu. Wana vipaji kuliko makundi yote lakini wana changamoto ya kutokujiamini.
Miongoni mwa viongozi ninaofikiri wapo kwenye hili kundi ni pamoja na Dr. Mohamed Gharib Bilal, Dr. Ally Mohamed Shein, Mwl Christopher Mwakasege, Dr. Philip Mpango, n.k.
Narudia tena, kwamba sijathibitisha kuwa hizo ndizo temperament zao, ila kwa walivyojipambanua katika shughuli zao, nimeshawishika kuamini kuwa huenda hayo yakawa ndiyo makundi yao. Hata hivyo, hayati Magufuli ni wazi kabisa kuwa yeye alikuwa "choleric"
Kuna viongozi kadhaa ambao mpaka sasa nimeshindwa kutambua "temperament" zao:
1. Julius Kambarage Nyerere
2. Freeman Mbowe
3. Edward Ngoyai Lowassa
4. Dr. Reginald Mengi
5. Mohamed Dewj
6. Said Salim Bakhressa
7. Profesa Issa Shivji
8. Profesa Kabudi
9. Profesa Ibrahim Lipumba
10. Dr. John Samwel Malecela
Karibuni kwa masahihisho, marekebisho, na nyongeza.
Asante.