Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 137,647
- 272,454
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Mh. Simbachawene amesema kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwa miezi 9 tu iliyopita zaidi ya ndoa 350 zimevunjika wilayani Temeke, kwa mujibu wa namba za kalenda za kidunia ni kwamba kila siku ndoa kadhaa zinavunjika kwenye eneo hilo linalosifika kwa vigodoro na sherehe zisizo na maana yoyote.
Kwa wasiojua na labda kwa wageni, Temeke ndio eneo ambako mtoto akipata mimba mama yake anaweza kufanya sherehe ili atuzwe khanga, vijora, madela na K Vant, ni eneo la ajabu ambako mtoto mchanga akikatika kitovu inaangushwa sherehe kubwa utadhani Yanga imetwaa ubingwa wa Afrika, achilia mbali sherehe ambazo hufanyika mtoto aliyezaliwa anapotimiza siku 40 au kutahiriwa ama kuvunja ungo.
Hii ni namba kubwa sana ya kuvunjika kwa mahusiano ya ndoa na inatia mashaka kama waoaji na waolewaji wanaandaliwa kabla ya kuoana. Nini kifanyike?