Tembo wanne watinga Chuo Kikuu Dodoma

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Tembo wanne wamekutwa ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma na kuvutia umati mkubwa wa watu.

TANAPA yasema jitihada zinafanyika kuwarudisha hifadhini.

My take: Naona Tembo nao wameanza safari ya kuhamia Dodoma, mpaka 2020 tutarajie wanyama wengi kutoka jamii mbalimbali nao watatinga mji huu mkuu (joke).

----------------------------------------
Habari kutoka Mwanachi Online
----------------------------------------

TEMBO WATINGA DODOMA

Dodoma ilikuwa mshikemshike leo alfajiri katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya tembo wanne kutinga chuoni hapo.

Watu wamefurika chuoni hapo kuwaangalia lakini polisi wamewazuia kusogea karibu na eneo walipo tembo hao.

Msemaji wa Tanapa, Paschal Shelutete amesema tayari wameshaita askari wa wanyapori kutoka Manyoni kwa ajili kuwaondoa tembo hao.

Shelutete amesema askari hao wanatarajiwa kufika wakati wowote kuanzia sasa.
 
Tembo wanne wamekutwa ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma na kuvutia umati mkubwa wa watu.

TANAPA yasema jitihada zinafanyika kuwarudisha hifadhini.

My take: Naona Tembo nao wameanza safari ya kuhamia Dodoma, mpaka 2020 tutarajie wanyama wengi kutoka jamii mbalimbali nao watatinga mji huu mkuu (joke).

Hongera Tembo wanaitikia wito wa kuhamia Dodoma! kwani ni watumishi wa serikali pekee wanatakiwa kuhamia huko? lazima pia kuwa na "zoo" ndogo!
 
Back
Top Bottom