sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,491
Tembo toka katika mbuga ya TSAVO nchini Kenya wamevamia makazi na kuharibu mazao katika baadhi ya maeneo yanayopakana na Kenya Wilayani Rombo.
Vijiji vilivyoathirika ni kama Kirongo Chini, Letto, Tangwa, Maweteta, Lotiro, Msaranga, n.k
Aidha mazao yaliyoharibiwa ni kama Mihogo, Mbaazi, Migomba, Alizeti, Mtama, n.k
Kwa miaka mingi sasa, tembo kutoka Kenya wamekuwa wakiharibu makazi, mazao na hata kuua watu katika maeneo hayo Wilayani huko, na hivyo wananchi hao wakipata hasa pamoja na kukumbwa na baa la njaa kutokana na uharibifu huo unaofanywa na tembo hao huku wakiwa hawana wa kuwasemea shida hiyo.
Rai kwa Serikali: Ni vema tembo hao wadhibitiwe kwani wanasababisha madhara makubwa kila mwaka na hayafiki sehemu husika. Kwa siku huingia hadi tembo 20 kwa msimu huu wa chakula hivyo huharibu kila kitu. Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii idhibiti hali hiyo na pia tembo hao hawana tofauti na wahamiaji haramu .
Nina imani suala hili litapata msukumo wa kukabiliana nalo mapema.